Mgombea urais wa chama tawala nchini Burundi Evariste Ndayishimiye ametangazwa mshindi leo kwenye kinyang’anyiro hicho.
Ndayishimiye ametangazwa kushinda baada ya kupata asilimia 68.72 ya kura zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi nchini Burundi ambayo imetangaza matokeo hayo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari nchini humo, imesema Agathon Rwasa wa chama cha National Freedom Council (CNL) ambaye ndiye mshindani mkuu wa Ndayishimiye amepata asilimia 24.19 ya kura.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, asilimia 87.7 ya wapiga kura waliojiandikisha walishiriki uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment