Tuesday, 19 May 2020

Makamu Rais wa kwanza wa Sudani Kusini Riek Machar na mke wake Waambukizwa Corona

...
Makamu Rais wa kwanza wa Sudani Kusini Riek Machar na mke wake Angelina Teny wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Dkt. Machar alisema kwamba yeye na mke wake ambaye pia ni waziri wa ulinzi, wamepata maambukizi baada ya kutangamana na jopo la ngazi ya juu la kukabiliana na virusi hivyo nchini humo.

Machar amesema kwamba hana dalili zozote na hali yake ya afya iko sawa lakini atajiweka karantini kwa siku 14.

Wengine waliothibitishwa kuambukizwa ni walinzi kadhaa na wafanyakazi.

Mpaka sasa Sudan Kusini imerekodi waathirika 236 na vifo vinne


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger