Mfanyabiashara Boniface Mwita (49), mkazi wa Tabata Kimanga na mkewe Rosemary Jenera (41), wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa maneno hatarishi kwamba hakuna corona, Serikali inadanganya.
Washtakiwa hao walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wankyo Simon.
Akisoma mashtaka, Wankyo alidai kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa kosa la kutoa lugha hatarishi ama yenye kushawishi jamii.
Akisoma mashtaka, Wankyo alidai kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa kosa la kutoa lugha hatarishi ama yenye kushawishi jamii.
Wanadaiwa Machi 20, 2020 ndani ya Dar es Salaam, wakiwa kwenye usafiri wa umma – daladala la kutoka Tabata kuelekea Muhimbili lenye namba ya usajili T 119 DKS aina ya Toyota Coaster, walitoa matamshi hatarishi.
Inadaiwa walisema: ‘Ugonjwa wa corona Serikali inadanganya, hakuna ugonjwa wowote na imefunga mashule kwa kuwa haina pesa na ada za kusomesha watoto bure’.
Jamhuri imeiambia mahakama kuwa matamshi hayo yangeweza kuleta hofu au hisia mbaya dhidi ya nchi yao ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wameachiwa kwa dhamana.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na itakuja tena Mei 6 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

0 comments:
Post a Comment