Friday, 17 April 2020

WAHUDUMU WA HOTELI WAAMBUKIZWA CORONA

...

Idadi ya visa vya waathirika wa Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia visa 246, baada ya hii leo kutangaza visa vipya 12, huku watano kati yao ni wakiwa ni wafanyakazi wa hoteli.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 17, 2020 na Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe, na kusema kuwa kwa kipindi cha masaa 24, nchi hiyo tayari imekwishapima sampuli za watu 450.

"Mpaka asubuhi hii ninavyoongea tayari ndani ya masaa 24 tumekwishapima sampuli 450 na kati ya hao tuliowapima tumepata wagonjwa 12, na siku yenyewe bado haijaisha na watano kati yao ni wafanyakazi wa hoteli" amesema Waziri wa Afya Mutahi Kagwe.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger