
Watu tisa zaidi wameambukizwa Virusi hatari vya Corona Nchini Kenya chini ya saa 24 zilizopita na hivyo kufanya idadi ya waliombukizwa virusi hivyo sasa kufika 225.
Saba kati yao ni wakenya, wengine ni raia toka mataifa mengine
Waziri wa Afya nchini humo Mutahi Kagwe, leo Jumatano Aprili 15, amesema mtu mmoja pia amefariki kutokana na virusi vya ugonjwa huo na kufanya idadi ya waliofariki kufika 10.
Amesema wagonjwa wengine 12 wamepona na hivyo kufanya idadi ya waliopona hadi sasa kufika 53
0 comments:
Post a Comment