Thursday, 2 April 2020

Serikali ya Uganda kuwapatia chakula wananchi milioni 1.5 Walioko Majumbani kutokana na virusi vya Corona

...
Waziri mkuu wa Uganda Bw. Ruhakana Rugunda amesema serikali ya Uganda itawapatia chakula watu maskini walioko mjini kuanzia Jumamosi wiki hii, ili kupambana na virusi vya Corona.

Bw. Rugunda amesema wizara ya mambo ya maafa itawapatia chakula watu wasiopungua milioni 1.5 walioko Kampala na Wakiso, ikiwa ni pamoja na wazee, wagonjwa, na madereva wa taxi, ambao kila mtu atapewa kilo 6 za unga wa mahindi, kilo 3 za maharagwe na chumvi. 

Zaidi ya hayo, akina mama wanaonyonyesha na wagonjwa watapewa kilogram 2 za maziwa ya unga na kilo 2 za sukari.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda Jumatatu wiki hii alitangaza kuwa serikali itawapatia chakula madereva na wale wanaopoteza kazi kutokana na hatua za kupambana na virusi vya Corona. 

Serikali ya Uganda imechukua hatua za mfululizo katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, ikiwa ni pamoja na amri ya kutotembea usiku, kusimamisha usafiri binafsi na umma, kufunga mpaka wa nchi, na kupiga marufuku mikusanyiko yote ya watu.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger