Waombolezaji wakibeba Jeneza lililobeba mwili wa Josephat Torner
Josephat Torner enzi za uhai wake
Mazishi ya Mwili wa Mwahaharakati wa kutetea Haki za watu wenye ualbino Josephat Torner Nkwabi (42) yanatarajiwa kufanyika kesho Alhamis Aprili 16,2020 katika kijiji cha Mwamwenge kata ya Imalamate wilaya ya Busega mkoani Simiyu alikozaliwa.
Josephat Torner Nkwabi amefariki dunia Siku ya Sikukuu ya Pasaka Aprili 12,2020 majira ya saa mbili usiku baada ya kugongwa na Hiace 'Daladala' akivuka barabara jijini Mwanza .
Mwili wa marehemu Josephat ulikuwa unahifadhiwa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza ambapo leo Jumatano Aprili 15,2020 umesafarishwa kwenda wilayani Busega kwa ajili ya mazishi kesho Alhamis.
Alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Utetezi wa haki za Watu wenye Ualbino iitwayo Foundation of Josephat Torner Europe Aid (FOJOTEA) awali ikijulikana Josephat Torner Foundation Europe lakini pia amewahi kuwa Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS).
Josephat Torner Nkwabi alizaliwa tarehe 15.04.1978 na kufariki dunia tarehe 12.04.2020 siku tatu kabla ya Kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa kwake.
Mwili wa Marehemu Josephat Torner ukiwa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza leo Jumatano Aprili 15,2020
Mwili wa Marehemu Josephat Torner ukitolewa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza leo Jumatano Aprili 15,2020 kwa ajili ya kusafarishwa kwenda wilayani Busega kwa ajili ya mazishi kesho Alhamis.
Mwili wa Marehemu Josephat Torner ukitolewa katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza leo Jumatano Aprili 15,2020 kwa ajili ya kusafarishwa kwenda wilayani Busega kwa ajili ya mazishi kesho Alhamis
0 comments:
Post a Comment