Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha, zimesababisha vifo vya watu wawili wilayani Arumeru.
Akitoa taarifa za ya mwendendo wa mvua ambazo zimenyesha kwa siku tatu mfululizo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, alisema mvua hizo zimeleta madhara makubwa baada ya watu wawili kufariki jana katika Halmashauri ya Meru.
Muro aliwataja waliofariki kuwa ni Terevaeli Nasari (65) Mkazi wa kitongoji cha Meto Kijiji cha Mulala Kata ya songoro.
Alisema mtu huyo alifariki dunia asubuhi ya jana baada ya maporomoko ya udongo kutoka mlimani kuvunja ukuta wa chumba alichokuwa amelala na kusababisha kifo chake na kwamba mwili wake upo katika Hospital ya Mount Meru.
Alisema kifo kingine ni cha mtoto Tumaini Simon mwenye miaka miaka mitatu kutoka Kijiji cha Valeska Kitongoji cha Mwamko, ambaye amesombwa na mafuriko ya maji wakati akiwa katika harakati za kuokolewa na mzazi wake.
Alisema mzazi wa mtoto huyo, Mzee Simon alifanikiwa kuokoa mtoto mmoja na mwingine kufariki dunia na mwili wa mtoto aliyefariki umepatikana na taratibu za mazishi zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment