Tuesday, 21 April 2020

Muhimbili yasambaza vazi la PPE kwa kamati za dharura Jijini Dar es salaam ili Kuendelea Kukabiliana na Corona

...
Na Sophia Mtakasimba & Angela Mndolwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanza kusambaza  mavazi maalumu (coverall) ambayo ni sehemu ya mavazi ya watoa huduma (PPE) kuvaa ili kujikinga wakati wanatoa huduma wagonjwa wenye maambuki mbalimbali ikiwemo Covid 19 kwa kamati za dharura za Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jana, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Zuhura Mawona  alisema kuwa baada ya kujadiliana na Serikali bei elekezi itakuwa Tzs. 50,000 kwa kila vazi moja.

Manispaa ya Kinondoni imenunua mavazi 15 yenye thamani ya Tzs. 750,000, Ilala mavazi 20 yenye thamani ya Tzs. 1,000,000 huku Manispaa nyingine zikiendelea kulipia ili kupata mavazi hayo.

"Kwa sasa tunaanza na vituo vilivyopo katika Manispaa za jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine itafuata" alisema Bi. Mawona

Alisema kuwa mahitaji ni makubwa katika mikoa mbalimbali hivyo kwa sasa Muhimbili imejikita katika kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji.

Mapema wiki iliyopita Muhimbili ilizindua vazi hilo maalumu liloshonwa na wataalamu wa MNH kwa kutumia malighafi za ndani ya nchi lengo ikiwa ni kukabiliana na upungufu wa bidhaa hizo duniani.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger