Saturday, 18 April 2020

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema apiga marufuku mikusanyiko kwenye baa....Aagiza Wanywaji Wanunue Wakanywee Nyumbani

...
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amepiga marufuku mikusanyiko kwenye baa zote wilayani humo kuanzia jana  Ijumaa Aprili 17 ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona. 

Amewataka waendesha baa hizo, kuhakikisha wanauza vinywaji hivyo lakini lakini mnunuzi akanywee nyumbani na kwamba atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua.

“Ni wajibu wa kila mmoja kuzingatia maelekezo haya kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwendeshaji wa baa na mtu yeyote atakayeonekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa,” amesema Mjema.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger