China inasema itatoa mchango wa Dola Milioni 30 kwa Shirika la Afya Duniani WHO, kulisaidia kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, ugonjwa unaosubua ulimwengu.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje nchini humo Hua Chunying kupitia ukurasa wake wa Twitter amethibtisha hilo na kusema mchango huo unalenga kulisaidia shirika hilo kupambana virusi katika nchi zinazoendelea.
Aidha, amesema kuwa tayari China imetoa Dola Milioni 20, mchango uliotoa kwa WHO mwezi Machi.
China has decided to donate additional $30 million in cash to WHO to support its global fight against #COVID19, in particular strengthening developing countries' health systems. China already donated $20 million in cash to WHO on March 11.— Hua Chunying 华春莹 (@SpokespersonCHN) April 23, 2020
Hatua hii ya China imekuja wiki moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa nchi yake inasitisha mchnago Wake kwa Shirika hilo kwa madai ya kushindwa kudhibiti mapema virusi hivyo.
Hatua hiyo ya Marekani ilaaniwa na China na mataifa mengine ya Magharibi huku WHO ikisema huu sio wakati wa kusitisha mchango huo wa fedha.
0 comments:
Post a Comment