Watu 18 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahwewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo iliyohusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster imetokea leo Jumatano Aprili 15, 2020 asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.
Amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15 na majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.
0 comments:
Post a Comment