Friday, 17 January 2020

Rais Vladimir Putin wa Urusi Ateua Waziri Mkuu Mpya Baada ya Baraza Zima la Mawaziri Kujizulu

...
Rais Vladimir Putin wa Urusi amemteua Mikhail Mishustin kuwa waziri mkuu mpya wa Russia. Mapema jana baraza la chini la bunge la Russia lilipitisha uteuzi huo kupitia upigaji wa kura.

Baada ya kuteuliwa Bw. Mishustin alitoa hotuba kwenye baraza la chini la bunge, na kuwashukuru rais Putin na baraza hilo kwa uungaji mkono wao, pia amesema ataripoti sera za serikali mpya kwa baraza la chini mnamo mwezi Aprili mwaka huu.

Vilevile amewaambia waandishi wa habari kuwa atakabidhi orodha ya mawaziri kwa rais Putin hivi karibuni.

Waziri mkuu wa zamani wa Russia Dmitry Medvedev ameteuliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Baraza la usalama la Urusi.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger