Monday 27 January 2020

Waziri mkuu wa Lesotho pamoja na Mkewe wakabiliwa na tuhuma za mauaji

...
Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane pamoja na mkewe, Maesaiah Thabane wanatakiwa kuhojiwa kuhusiana na mauaji yaliyotokea mwaka 2017 ya Mke wa kwanza wa Thabane, Lipolelo Thabane (58)
 
Lipolelo alikuwa ametengana na mume wake na alikuwa akiishi peke yake tangu mwaka 2012 ambapo aliuawa siku 2 kabla ya Thabane kuapishwa kuwa Waziri Mkuu kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake

Ushahidi wa hivi karibuni uliowasilishwa Mahakamani na Kamishena wa Polisi umebaini kwamba kulikuwa na mawasiliano ya simu katika eneo la tukio kwa kutumia namba ya simu inayodhaniwa kuwa ni ya Thabane

Waranti ya kukamatwa kwa Maesaiah Thabane ilishatolewa lakini hajaonekana hadharani kwa wiki 2 sasa, hakuna anayejua alipo na Thabane amekataa kusema alipo mke wake


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger