Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo imepanga kufanya mkutano wa kusikiliza Maoni ya wadau [Public Hearing ]kuhusu Muswada wa sheria wa usuluhishi ya Mwaka 2020[The Arbitration Bill 2020] kwa mujibu ya kanuni ya 84[2] ya kanuni za kudumu za Bunge,Toleo la Januari ,2016,ambapo Muswaada huo umesomwa kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 28,Januari,2020.
Katika taarifa iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kimataifa ofisi ya Bunge Januari 28,2020 jijini Dodoma imefafanua kuwa mkutano huo wa kusikiliza maoni ya wadau[Public Hearing ]utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 31,Januari,2020 saa saba mchana katika ukumbi Na. 229 jengo la Utawala Bungeni jijini Dodoma.
Aidha,katika taarifa ya kitengo hicho cha Mawasiliano na Uhusiano wa kimataifa Ofisi ya Bunge imeendelea kufafanua kuwa ,kwa kuzingatia umuhimu wa muswada huo ,kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni ya wadau ambapo pia Maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa barua pepe cna@bunge.go.tz na muswada unaweza kupakuliwa kupitia www.parliament.go.tz.
0 comments:
Post a Comment