Tuesday 28 January 2020

Polepole Amvaa Zitto Kabwe...."CCM Itashinda Hata Wakizuia Mkopo Wao"

...
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole  amemtolea uvivu Zitto Kabwe kwa kitendo cha kuzuia fedha za elimu huku akisema watashinda Uchaguzi Mkuu hata akizuia fedha hizo.

Zitto ambaye  ni kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo aliandika barua za kutaka Benki ya Dunia kusitisha mkopo wa elimu baada ya kudai serikali inakiuka taratibu kwa kuwazuia wanafunzi waliopata ujauzito wasiendelee na masomo.

Pia zitto alisema mkopo huo sio kweli ulilenga kuwanufaisha wanafunzi na kwamba ni kwa ajili ya kampeni za kisiasa 2020.

Polepole baada ya kuona taarifa hiyo alimjibu kuwa; Kumbe tatizo ni Uchaguzi 2020. Kabwe anaomba tunyimwe mkopo wa kuongeza umadhubuti wa elimu ya watoto wetu kwasababu anajua ni jukumu letu kujenga shule na sifa zitakuja CCM, inayokwama si CCM, ni watoto wa Kigoma Ujiji. Kushinda tutashinda tu! Najiuliza watoto wake wanasomawapi?


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger