Thursday 30 January 2020

AFISA USALAMA WA TAIFA FEKI AKAMATWA AKITAPELI WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA

...
                                      Sheliku Sweya
                      Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga Dk. Rose Malisa amenusurika kutapeliwa na mwanaume aitwaye Sheliku Sweya (45)ambaye alijifanya kuwa ni ofisa usalama wa taifa akimtaka ampe rushwa ya ngono ili amsaidie kutatua changamoto zilizopo hospitalini huku Dk. Geofrey Mboye akitapeliwa Sh 300,000 ili asaidiwe kupata uhamisho wa kwenda mkoani Dodoma.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juzi,Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba alisema baada ya kupata taarifa hizo waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Januari 23,2020, ambapo katika uchunguzi wa awali wamebaini mtuhumiwa siyo ofisa usalama wa taifa bali amekuwa akitumia cheo hicho kujipatia kipato au rushwa ya ngono ili kufanikisha malengo yake.

Alisema madaktari wote ni watumishi katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo Dk .Malisa ambapo alielezwa kuwa iwapo atatoa rushwa ya ngono atapatiwa vifaa tiba na kuongezewa watumishi wa afya ikiwa ni pamoja na kumuahidi kumfutia deni kiasi cha Shilingi milioni 40  anazodaiwa na taasisi ya afya alikopatia masomo yake ya udaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.

"Kutokana na ushirikiano mkubwa uliofanyika na Dk.Malisa tuliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa kabla hajafanikiwa kupata rushwa ya ngono,anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika",alisema kamanda Magiligimba.

Katika maelezo yake polisi Dk. Rose Malisa alieleza kuwa alimtilia mashaka mtuhumiwa na kutoa taarifa polisi ambao walishirikiana ikiwa ni pamoja na kuweka mtego ambao ulisaidia kufanikiwa kumkamata mtu huyo aliyejifanya ofisa usalama wa taifa ili kufanikisha malengo yake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger