Monday, 13 January 2020

Al Shabaab Waivamia Tena Kenya....Walimu Watatu Wauawa

...
Watu watatu wameuawa baada ya wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab kuvamia mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa huku kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.

Maafisa wa polisi wanafuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama zikionyoesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo.

Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.

Hili ni shambulizi ya 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi 4 yakitekelezwa Garissa, 3 Wajir, 2 Mandera na 2 Lamu.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger