Thursday, 6 June 2019

JAMAA ALIYEJITANGAZA LIVE KUWA NI 'SHOGA' ATEULIWA KUWA WAZIRI WA SHERIA

...
Mwanaume wa kwanza kutangaza wazi kuwa anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja ameteuliwa kuwa waziri na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Amir Ohana,kutoka chama cha Natanyahu cha Likud , amemteua kama kaimu waziri wa sheria kufuatia kufutwa kazi kwa mtangulizi wake.

Bwana Ohana, mwenye umri wa miaka 43, ni mfuasi sugu wa Netanyahu , ambaye aliunga mkono hatua za kumlinda waziri mkuu dhidi ya kushtakiwa.

Uteuzi wake unakuja siku kadhaa baada ya bunge kuvunjwa kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mpya.Bwana Ohana ni mfuasi sugu wa Netanyahu, na ametumia juhudi zake zote kuunga mkono muswada tata uliomuwezesha waziri mkuu aliyeko madarakani kuwa na kinga ya kutoshtakiwa

Bwana Netanyahu alimfuta kazi waziri wa sheria aliyekuwepo madarakani , Ayelet Shaked, miezi mitatu iliyopita.

Chama cha Shake ,ambacho kilikuwa sehemu ya serikali ya muungano wa Netanyahu, hakikupata viti vya kutosha kukiwezesha kurejea bungeni katiika uchaguzi wa mwezi Mei.

Waisrael watafanya tena uchguzi mwezi wa Septemba baada ya Bwana Netanyahu kushindwa kupata uungaji mkono wa kutosha kutoka kwa vyama kumuwezesha kuunda serikali ya mpito.

Ikitangaza utuzi wake, ofisi ya waziri mkuu ilisema kuwa Bwana Ohana ambaye ana taaluma ya sheria ni mwenye uelewa mkubwa sana mfumo wa sheria''

Bwana Ohana ni mfuasi sugu wa Netanyahu, na ametumia juhudi zake zote kuunga mkono muswada tata uliomuwezesha waziri mkuu aliyeko madarakani kuwa na kinga ya kutoshtakiwa.

Bwana Netanyahu anachunguzwa kwa madai rushwa na ufisadi na anaweza kushtakiwa miezi michache ijayo .Anakanusha vikali shutuma dhidi yake.
Bwana Ohanani mwanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja , ambaye anatetea ndoa za jinsia moja, jambo ambalo halitambuliki nchini Israeli isipokuwa kwa wale watakaoamua kufunga ndoa yao nje ya nchi . Mwaka jana apinga muswada wa sheria uliopiga marufuku ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja kwa kuzingatia utambulisho.

Ingawa haki za wapenzi wa jinsia moja zinapingwa na jamii ya Wayahudi nchini Israeli, kwa ujumla taifa hilo limekuwa na mafanikio katika kucommunity zenye sheria inayowalinda wapenzi wa jinsia moja.

Bwana Ohana ni mmoja wa wabunge kadhaa waliotangaza wazi kuwa wanashiriki mapenzi ya jinsia moja na mwaka jana mji wa Israel uliopo karibu na Tel Aviv ulikuwa wa kwanza kuwa na Meya mpenzi wa jinsia moja anayetangaza wazi kuwa anashiriki mapenzi hayo.
Chanzo - BBC
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger