


Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 20 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza Maisha.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, inasemekana kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya Hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea Hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.
Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.
0 comments:
Post a Comment