Saturday, 21 May 2016

HIZI NDIZO FAIDA KUBWA ZA KWENDA JKT KWAKO WEWE MWANAFUNZI KIDATO CHA 6 ULIEPANGIWA JKT KWA MUJIBU

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
upload_2016-5-21_8-34-17.jpeg
Habari zenu ndugu zangu ;
Leo napenda kuzungumzia suala la kidato cha sita na walimu kwenda jkt kama ilivyopitishwa na serikali kuwa ni suala la lazima kwenda jeshi kabla ya kupata ajira. Mimi ni miongozi mwa vijana waliobahatika kupata mafunzo hayo baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2013 mwezi wa pili amapo nilipangiwa kambi ya rwamkoma musoma 822kj.

Kusema ukweli nilishtuka sana kwani nilikuwa najiapanga kwenda chuo kikuu baada ya kumaliza msoto wa kidato cha sita kama ilivyo kawaida kuwa elimu yetu ya tanzania ni ngumu sana.

Siku zikasogea nikaenda  jeshini kiukweli maisha ya kweli mwanzoni yalikuwa mapya sana kwani nilichoshangaa zaidi ni kwamba salamu ya kule sio mambo tena bali NI JAMBO AFANDE.



Nikakutana na jamaa jeshi limeshawakolea nilichukua siku nyingi mpaka kuwazoea ,kiukweli tulikuwa wengi sana kwani nakumbuka kuwa  nilipiga kwata na mtoto wa mh.mwinyi .

Ndugu zangu walimu maisha ya jeshi ni mazuri sana kwani nimepata faida nyingi sana ambazo ni;

UZALENDO WA NCHI YANGU;Kwani hadi mda huu nimetokea kuipenda nchi yangu kwa kiasi kikubwa kana kwamba nikikuta mtu anaikashfu serikali hii natamani nimpige lakini kwa kuwa si ruhus kufanya hivyo inabidi nimpe elimu juu ya serikali ya nchi hii.

NIMEFUNDISHWA SILAHA ZOTE,KUZITUMIA NA KUZISAFISHA,je ningebaki nyumbani ningejua?nawaombeni muende.

NIMEPATA MARAFIKI WENGI SANA ,ambao wamenifanya kutembea mahala popote tanzania na kuwa na uhakika na sehemu ya kuishi.

NIMEJIFUNZA USHIRIKIANO,kwani kila kazi tulikuwa tukifanya kwa ushirikiano wa hali ya juu.

NIMEJIFUNZA KWATA,nilifurahi sana kwani nakumbuka nikiwa jeshini kombania yetu ya e coy ilishinda kwata chini ya uongozi wa sir meja macha.
NITAENDELEA,ku........contact me kwa maoni,swali ushauri nk. zaidi(+255768260834)

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger