Monday, 4 February 2019

SERIKALI KUFUMUA SHERIA YA UVUVI

Na.Amiri kilagalila Serikali imeamua kuifumua Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 ili kuondoa vikwazo vya kibiashara na uwekezaji katika sekta ya uvuvi. Pia kwenda na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya awamu ya tano inayolenga kujenga Tanzania ya viwanda, kuwatetea na kuwalinda wanyonge. Akizungumza katika uzinduzi wa ukusanyaji maoni ya wadau kuhusu rasimu ya Sheria ya Uvuvi na Sheria ya Ukuzaji viumbe kwenye maji jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, alitaja sababu nyingine zilizosababisha kuwapo mabadiliko hayo.…

Source

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 4,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 4, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Sunday, 3 February 2019

CCM TABATA YAOMBA WANACHAMA WASICHAFUANE

Na Heri Shaban Chama cha Mapinduzi CCM Mtaa wa Kimanga darajani imewataka wana CCM wasichafune katika kipindi hiki cha kuelekea chaguzi za Serikali za Mitaa badala yake wanachama wa chama hicho wametakiwa wajenge chama na Jumuiya zake. Hayo yalisemwa na Katibu Mwenezi wa CCM Kimanga Deogratius Mkude wakati wa hafla ya mkutano mkuu wa CCM Kimanga darajani. Mkude alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa sasa sio mda wa kuchafuana ni mda wa kujenga chama pamoja na jumuiya za Vijana, Wazazi na jumuiya ya Wanawake UWT…

Source

Share:

JIKO LAUA WATOTO WAWILI TARIME

Jiko la mkaa lililokuwa ndani limesababnisha vifo vya watoto wawili baada ya kukosa hewa wakati wakiwa wamelala usiku.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Februari 3, 2019, katika mtaa wa Kebaga, wilayani Tarime mkoani Mara kwa watoto hao Witness Machugu (1) na Christina Marwa mwenye umri kati ya miaka 12-13 wakiwa wamelala chumba kilichokuwa na jiko la mkaa huku madirisha yakiwa yamefungwa.

Babu wa marehemu hao, Hobo Kihugi alisema mkwe wake aliweka jiko hilo kwenye chumba cha watoto jana usiku kwa lengo la kuandaa uji wa watoto.

Kamanda wa Polisi, Tarime-Rorya hajazungumzia tukio hili licha ya gari la polisi na askari kufika nyumbani kwa marehemu kuuchukua mwili wa Witness na kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mji wa Tarime.

Mwili wa Christina ulibaki nyumbani kwa ndugu zake wakidai wanataka kuuzika kwani taratibu zote zilikuwa zimekamilika ikiwamo kuchimba kaburi. Hata hivyo, polisi wamedai haiwezekani kwani lazima uchunguzi ufanyike.

Na Waitara Meng'anyi, Mwananchi
Share:

BALOZI WA TANZANIA UJERUMANI AMVAA TUNDU LISSU


Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi ametoa tamko akijibu madai ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyoyatoa hivi karibuni nchini humo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha News Africa cha kituo cha televisheni cha Deutsche Welle (DW).

Lissu ambaye kwa sasa yuko nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu kufuatia shambulio la risasi la Septemba 7, 2017 jijini Dodoma amekuwa akiituhumu Serikali kuhusika huku akihoji sababu ya kutokamatwa kwa mshukiwa yeyote, mbali pia na madai ya ukandamizwaji wa demokrasia nchini.

Akijibu madai ya Lissu katika tamko lake la Januari 29, 2019, Dk Possi amesema Serikali imekuwa ikilifuatilia suala hilo ikiwa ni pamoja na kuanza uchunguzi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa taarifa ya kulaani tukio hilo na kuagiza uchunguzi wa kina wa haraka. Kwa nyakati tofauti Rais amemtuma Makamu wake, Rais mstaafu na viongozi wengine wa Serikali kumtembelea Lissu akiwa hospitali akiwa Dodoma, Nairobi na Brussels (Ubelgiji).”

“Ni vema sasa mbunge angepima ishara hizo njema za Rais kwenye madai anayotoa yasiyo na msingi,” amesema Dk Possi katika tamko lake.

Kuhusu madai ya kutochunguzwa kwa tukio hilo, Dk Possi amesema mamlaka za Serikali zingetaka kumpata Lissu ili atoe ushirikiano wa taarifa kuhusu tukio hilo.

Ameongeza uchunguzi ulishaanza mara tu baada ya tukio hilo lakini umeshindwa kuendelea kwa sababu ya kutopata ushirikiano kutoka kwa mbunge huyo.

Na Elias Msuya, Mwananchi
Share:

MANARA AWAPA POLE WANA SIMBA KICHAPO CHA 5G


Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameibuka kwa mara ya kwanza kufuatia kichapo cha pili mfululizo cha mabao 5-0 dhidi ya Al Ahly ya nchini Misri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagrma, Haji Manara amewapa pole mashabiki wa klabu hiyo na kuwapa ahadi kuwa Simba lazima ipate pointi 6 za nyumbani na itafuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo.

"Poleni sana Wanasimba wote, Najua mnavyojisikia now ila niwaambie hesabu zipo kwetu,kama ninavyowaambia always,lazima tupate points tisa za nyumbani!! Yes tukifanikiwa kushinda mechi mbili zilizobaki za home,wanaowacharura leo watawapa hongera!! Yes We Can".

Simba imepoteza mchezo wa pili mfululizo wa ugenini, kwa idadi sawa ya mabao 5-0. Mchezo wa kwanza ukiwa dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo.

Wekundu hao wa Msimbazi bado wako katika nafasi ya tatu kwa pointi tatu, wanayo nafasi ya kusonga mbele endapo watafanikiwa kushinda michezo yao yote iliyobakia, miwili wakicheza uwanja wao wa nyumbani na mchezo mmoja wakicheza ugenini dhidi ya JS Saoura.
Share:

RAIS WA TFF AOMBA RADHI

Rais wa TFF, Wallace Karia amesema alimfananisha Mbunge Tundu Lisu na Richard Wambura kutokana na mambo wanayoyafanya. Wambura akisoma hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa TFF jana Jumamosi jijini Arusha alisema watu wanaojifanya kina Tundu Lisu kwenye mpira hawatapewa nafasi. “Nilisema hivyo nikimfananisha Wambura na Tundu Lisu kutokana na namna watu hao wanavyozungumza kila siku. Kama kuna baadhi ya watu nimewakwaza katika hilo basi wanisamehe,” alisema Karia. Aidha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema awali kilimtaka Rais wa TFF Wallace Karia kumuomba radhi Mbunge wake na Mwanasheria Mkuu wa chama…

Source

Share:

MBUNGE BOBALI ATISHIA KUJIUZULU

Sakata la ununuzi wa korosho limeendelea kuwasha moto bungeni baada ya Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali kusema yupo tayari kujiuzulu ubunge iwapo itathibitika kwamba wakulima hawalipwi Sh2,640 kwa kilo badala ya Sh3,300 iliyotangazwa na Rais John Magufuli. Akichangia taarifa za kamati za Bunge za Bajeti na ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) jana, Bobali alisema kwa taarifa zilizotolewa na Serikali ni wazi kuwa kilo moja ya korosho imeuzwa kwa Sh4,180 na kuitaka kueleza kama itaendelea kuwalipa wakulima korosho daraja la kwanza kwa Sh3,500. “Tunataka kauli kama mmeuza kwa…

Source

Share:

AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA AKITETEA MIFUGO ISILE MAZAO YAKE

Mkazi wa Kijiji cha Makole aliyetambulika kwa jina moja la Ally ameuawa kwa kukatwa mapanga.


Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Edward Bukombe amethibitisha kutokea mauaji hayo yaliyofanyika kijiji cha Makole, Kata ya Kwalukonge wilayani Korogwe.

Kamanda Bukombe alisema mauaji hayo yalitokea baada ya mfugaji, Paulo Marko (24) kuingiza mifugo yake katika shamba la Ally, na katika mabishano, ndipo Marko aliamua kumkata mapanga hadi kufikwa na umauti.

“Ni kweli kumetokea mauaji katika Kijiji cha Makole, Kata ya Kwalukonge wilayani Korogwe ambapo mfugaji Paulo Marko amemuua bwana Ally wakati akitetea mazao yake,” alisema.

Aliongeza, “mfugaji aliingiza ng’ombe wake kwenye shamba la mkulima akaanza kula mazao na mkulima huyo alipomwambia aondoe ng’ombe wake, katika mabishano ya muda mrefu ndipo ikafikia hali hiyo ya mauaji.”

Via Habarileo
Share:

BASI LA FRESTER LAPATA AJALI BUKOBA

Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea jijini Dar es salaam wamenusurika kifo huku watu wanane wakijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao baada ya basi la Frester kupata ajali katika Kata ya Katahoka wilayani Biharamulo mkoani humo.

Gari hilo limetambulika kwa namba za usajili T375 DND ambapo mkuu wa polisi wilaya ya Biharamulo, Rashid Mududhwari amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Aidha, mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo ambaye ni diwani wa Kata ya Katahoka wilayani Biharamulo, Tulieni Abedinego Mathayo amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa jana saa 3:10 asubuhi katika kona ya kijiji cha Kasuno na kwamba kati ya majeruhi hao mwanamke mmoja amevunjika mkono.

Amesema kuwa viongozi wa wilaya wakiongozana na askari wa JWTZ Biharamulo na polisi waliwahi kuokoa abiria na kuwapelekwa Biharamulo Mjini kuwatafutia usafiri walionusurika na majeruhuhi kuwahishwa hospitali.
Share:

MAITI YAKUTWA IMESHIKILIA SAHANI YA WALI MKONONI


Kumetokea kisa cha ajabu mjini Matuu Kaunti ya Machakos nchini Kenya baada ya mfanyabiashara maarufu eneo hilo kukutwa katika gari lake akiwa amefariki huku ameshikilia sahani ya wali na pembeni kukiwa na chupa ya chai moto.
Wengi walioshuhudia walipatwa na mshtuko mkubwa na haijabainika iwapo aliuawa ama aliaga dunia kwa njia ya kawaida.

 Mkuu wa polisi eneo la Yatta Eric Ng'etich amethibitisha tukio hilo na kusema, marehemu alikuwa amekamata sahani ya wali na pembeni kulikuwa na chupa ya chai moto.

 Polisi walisema kwa sasa hawawezi kuthibitisha kilichomuua mfanyabiashara huyo lakini uchunguzi wao umeanzishwa.

 "Ni masikitiko kwa visa vya aina hii. Marehemu ni Joe, mfanyabiashara maarufu hapa. Alipatikana akiwa maiti ndani ya gari lake. Hatuwezi kufahamu ikiwa ni kweli alikuwa akila wali ama sahani na chupa ya chai alilazimishiwa," Ng'etich alisema. 

"Uchunguzi umeanzishwa. Tutachunguza hadi tutakapopata ukweli kuhusu kifo chake," mkuu huyo wa polisi alisema. 

Alisema kuwa, walivunja mlango wa duka la marehemu lililokuwa karibu na kukuta pingu zilizokuwa juu ya kaunta.

 Wakazi wa eneo hilo ambao sasa wana hofu kufuatia mauaji hayo, wanahusisha mauaji hayo na kisa cha 2018 ambapo mfanyabiashara mwingine aliuawa katika eneo hilo.

 Jumatano, Novemba 14, Peter Mwangangi mfanyabiashara maarufu wa eneo la Kanyonyoo, Machakos alipataikana amekufa katika gari lake aina ya Toyota Harrier na polisi kushuku aliuawa kwa kudungwa sindano zenye sumu.

Share:

RAIS WA TFF AITIBUA CHADEMA KAULI YA "TABIA ZA U - TUNDU LISSU', WAMTAKA AOMBE RADHI

 Kauli ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kumfananisha mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Michael Wambura kwa kupinga hoja, kumeiibua Chadema na kumtaka rais huyo kuomba radhi hadharani.

Chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimetaja mambo manne kinachoazimia kuyatekeleza iwapo Karia hatoomba radhi.

Jumamosi Februari 2, 2019 jijini Arusha katika mkutano mkuu wa TFF Karia alikemea watu wenye tabia za ‘u Tundu Lissu’ katika soka, kwamba kamwe hawezi kukubali kuona wakiendelea kukosoa uongozi wa TFF.

Baada ya mkutano huo Karia alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo amesema, “Nimesema kama kuna ‘ma Tundu Lissu’ kwenye mpira, nadhani mnaelewa Lissu anahangaika kwenye vyombo vya habari kuikashifu Serikali, na Wambura anazungumza kwenye vyombo vya habari kuikashifu TFF na uongozi wa TFF.”

“Hivyo nikamlinganisha Wambura na Lissu, ila kama hii kauli imewakera wengine naomba samahani.”

Kufuatia kauli hiyo,jana jioni mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alitoa tamko la chama hicho, akimtaka Karia kuomba radhi.

“Tumepokea kauli yenye ukakasi mkubwa (ya Karia) kuwa atawashughulikia wale wote ambao wataleta ‘ U-Tundu Lissu’ kwenye mpira. Kauli hii imebeba ujumbe mahsusi kuwa watu aina ya Tundu Lissu wanastahili kushughulikiwa kwenye sekta zote,“ amesema Mrema.

Amebainisha kuwa chama hicho kinaamini kuwa watu aina ya Lissu ni wale wote wenye mtazamo na uwezo wa kuhoji, wanaotaka utawala wa sheria ufuatwe na wanaotaka sheria na Katiba ziheshimiwe.

“Sasa kauli ya Karia inatufanya tujiulize maswali inawezekana anawajua waliomshughulikia Lissu na ndio maana anataka kuwatumia kushughulikia 'Tundu Lissu' walioko kwenye mpira,” alisema Mrema.

Katika maelezo ya leo ya Chadema, chama hicho kimesema kufuatia kauli hiyo ya Karia kinatafakari kufanya mambo manne ambayo ni; kuhamasisha wanachama wake kutoshiriki matukio ya TFF, kususia bidhaa zote zenye nembo na au zinazotolewa na TFF zikiwemo jezi za timu za Taifa, kuchukua hatua dhidi ya kampuni zitakazoendelea kushirikiana na TFF na kushawishi wadau wa mpira kutoshirikiana na TFF.

Via Mwananchi
Share:

Saturday, 2 February 2019

WAARABU AL AHLY WAICHAPA SIMBA 5 - 0...KIPIGO CHA MBWA KOKO


Dakika 90 za Mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya Makundi kati ya Simba SC na Al Ahly zimemalizika kwa Simba SC kuambulia kichapo cha Bao 5 - 0.

Share:

Picha : UVCCM MKOA WA SHINYANGA WASHEHEREKEA MIAKA 42 YA CCM KWA BONANZA KUBWA


Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Shinyanga umefanya Bonanza lililohusisha michezo mbalimbali kwa lengo la kusherehekea miaka 42 ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Bonanza hilo limefanyika leo Februari 2,2019 katika uwanja wa mpira wa CCM Kambarage uliopo mjini Shinyanga 


Akizindua bonanza hilo mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kwa awamu nne zilizopita mpaka sasa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kupiga hatua za kimaendeleo. 

“Vitu vingi vikubwa vimefanyika kupitia CCM na serikali yake na jumuiya zake kwa ujumla, nchi yetu imeendelea kuwa salama miundombinu imeboreshwa barabara ndio usiseme Shinyanga haikuwa hivi, sekta ya afya , elimu vimeboreshwa na tulikuwa na ndege moja leo tunazo saba vyote hivi vipo ndani ya ilani ya chama”alisema Malola 


“Na mimi niombe tuendelee kuyaenzi maendeleo haya yaliyoletwa na CCM kwa vitendo”,aliongeza Mlolwa. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amewakumbusha vijana kuendelea kudumisha ushirikiano katika mambo yote yanayofanywa na chama pamoja na serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi wanaowatumikia. 

“Nawashukuru sana ndugu zangu wote na viongozi wote wa serikali na chama mlioshiriki katika Bonanza hili tudumishe umoja na mshikamano kati yetu hivi ndivyo serikali yetu inataka” ,alisema Shemahonge. 

Bonanza hilo limeshirikisha michezo mbalimbali ukiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete , mchezo wa kuvuta kamba , kukimbia kwenye magunia na kuwashirikisha viongozi wa serikali na chama cha CCM. 
Kauli mbiu kwa mwaka huu inasema “Kazi ni kipimo cha utu ,chapa kazi tulinde uhuru na utaifa wetu”.

Mgeni rasmi katika Bonanza la UVCCM Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na wadau waliohudhuria katika bonanza la michezo ambapo amepongeza jitihada zilizofanywa na serikali ya CCM kwa awamu nne zilizopita mpaka sasa awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa kiwango kikubwa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kupiga hatua za kimaendeleo. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack katika bonanza hilo ambapo aliwataka vijana kushirikiana katika kuijenga Shinyanga wakishirikiana pamoja na serikali yao.
Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) akimpatia zawadi ya jezi mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa katika ufunguzi wa bonanza hilo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Husein Egabano akiongoza msafara wa vijana kuingia katika uwanja wa CCM Kambarage lilipofanyika bonanza hilo
Mgeni rasmi katika bonanza hilo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua michezo katika bonanza hilo kwa kupiga penati.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika bonanza hilo wakifuatilia kwa umakini matukio yote yanayoendelea uwanjani.
Timu ya wanawake ambao ni wanachama wa CCM (wenye jezi za kijani) wakichuana vikali na timu ya watumishi wa serikali (wenye jezi za rangi nyekundu) katika mchezo wa pete, ambapo timu ya watumishi ilishinda kwa goli 14 dhidi ya wanachama 9.
Mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa( katikati) akiwa pamoja mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba(kulia) pamoja na mwenyekiti UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (kushoto) wakifuatilia michezo katika uwanja wa CCM Kambarage.
Mpira wa miguu ukiendelea katika uwanja wa Kambarage hapa ni mchezo kati ya timu ya walimu kutoka chuo cha Shy com (wenye jezi ya kijani) na Timu ya Stand United chini ya miaka 20(jezi rangi ya chungwa)
Mgeni rasmi akikabidhi zawadi ya kikombe kwa timu ya watumishi wa serikali walioshinda michezo mingi katika bonanza.
Mchezo wa kukimbia na magunia ukiendelea 
Vijana wa kikundi cha dance kijulikanacho kama The Fighter cha mjini Shinyanga wakionesha moja ya mchezo ambapo waliigiza mtu akicheza kama amechomwa kisu shingoni .
Share:

DAKIKA 45 ZA MWANZO : AL AHALY 5,SIMBA 0

No photo description available.
Share:

TIMU YA NJOMBE MJI YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA NAMUNGO FC UWANJA WA NYUMBANI

Na.Amiri kilagalila Timu za NJOMBE MJI FC na NAMUNGO FC zimegawana pointi moja, baada ya kumaliza dakika tisini za mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Njombe mkoani mkoani humo, matokeo ambayo yamewafanya mashabiki wa soka wa Njombe mji kutoa lawama za wazi kwa waamuzi wanaochezesha michuano hiyo. Penati iliyochezwa dakika tatu kabla mpira haujamalizika ndiyo iliyopoteza matumaini ya timu ya Njombe Mji Fc kutoka uwanjani na alama tatu kufuatia mchezaji wa timu hiyo kumwangusha mchezaji wa Namungo Fc katika eneo la hatari,…

Source

Share:

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI CHARLES KITWANGA ALIYELAZWA HOSPITALI MUHIMBILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemjulia Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

January 31 mwaka huu alisafirishwa kutoka Dodoma kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger