Friday, 28 December 2018

YANGA HII “IYENA IYENA” WABIKISHA DAKIKA HIZI 180 ZA KUWAZIBA MDOMO SIMBA

MABINGWA wa Kihistoria timu ya soka ya Yanga,wamepania kuhakikisha wamlalua kila anayekuja mbele yake baada ya kuhaidi kuzitumia dakika ngumu 180 kuthibi­tisha kwamba hawakuwa wakibahati­sha kwenye mzunguko wa kwanza. Watoto hao wa Jangwani ambao Kikosi chao hicho kinanolewa na kocha mwenye maajabu yake , Mwinyi Zahera hadi sasa kimecheza mechi 17 na kati ya hizo imeshinda 15 ikiwa imepata alama 47. Lakini kibarua kizito kinakuja kukamilisha mzunguko wa kwanza. ambapo ni ni dhidi ya Mbeya City na Azam FC. Endapo Yanga itafanikiwa kushinda mechi hizo mbili, itakuwa imefikisha alama 53…

Source

Share:

SAKATA LA VIKOKOTOO VYA WAFANYAKAZI LAGEUKA KAA LA MOTO,WAZIRI MHAGAMA AKALIA KUTI KAVU,BULAYA ATAKA AJIUZULU

Ikiwa ni masaa machache yamepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na Shirikisho la Chama cha Wafanyakazi (TUCTA) na kujadili masuala ya vikokotoo na kulitolea maamuzi, mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) amemtaka waziri Jenista Mhagama kujiuzulu pamoja na mkurugenzi wa SSRA. Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA), Ester Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amewataka waziri Mhagama kujiuzulu, baada ya Rais Magufuli kuagiza vikokotoo vya mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi…

Source

Share:

WAZIRI ATAKIWA KUJIUZULU BALAA LA KIKOKOTOO

Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA), Ester Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amewataka Waziri Jenista na Mkurugenzi wa SSRA kujiuzulu, baada ya Rais Magufuli kuufuta mswada wa mabadiliko ya sheria ya utoaji mafao kwa kwa wastaafu.

Bulaya amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter ambapo amesema kuwa Waziri Mhagama na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kufanya hivyo kwa kuwa wameshindwa kuwatetea wafanyakazi.

"Mh Jenista, na Mkurugenzi wa SSRA, mjiuzulu nimewashinda, hamkuwatetea wafanyakazi", ameandika Bulaya.

Siku kadhaa baada ya habari hizo kuenea aliibuka Waziri Kivuli (Ofisi ya Waziri Mkuu) wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Esther Bulaya, ambaye alieleza kuwa kikokotoo hicho kinawaumiza wastaafu na hakikujulikana kwa wabunge.

Wasimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii yaani Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), ilifafanua kuwa, lengo la kubaki kwa fedha hizo ni kumsaidia mstaafu kuishi vizuri kwa kuendelea kupata fedha ambazo zinasaidia maisha yake, kuliko kumpa zote ambazo huenda akazitapanya na kurudi katika umaskini.
Share:

KWA SIMBA HII CAF MLETENI YEYOTE YULE ATAKUFA TU,BOCCO APIGILIA MSUMARI HUU WA MWISHO

NA KAROLI VINSENT MLETENI yeyote yule  kwa Simba hii iliyosheheni wachezaji Nyota lazima watakaa ndivyo naweza kusema baada ya leo droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19 inatarajiwa kupangwa. Mabingwa hao wa Ligi kuu ya Tanzania Bara,Timu ya Simba ni miongoni mwa timu ambazo zimefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika,. Wakimataifa hao ambao wananolewa na kocha ambaye anasifika kwa “Fomesheni” ya hatari ,Mbelgiji Patrick Aussems ,kupitia kwa nahodha wa timu hiyo mshambuliaji , John Bocco(Adebayo) amebainishwa kuwa hawaogopi kupangwa na…

Source

Share:

MAMBO YAMFIKA SHINGONI MREMA,AAMUA KUVUNJA UKIMYA NA KUTOA KILIO HIKI

MAMBO yamemfika shingoni na kuamua kusema ndivyo naweza kusema baada ya Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema, kuibuka na kuingukia Serikali inapofanya marekebisho ya vyama vya siasa kuangalia umuhimu wa kuvipatia vyama vidogo vya siasa ruzuku, ili navyo viweze kujiendesha. Mbali na kutaka marekebisho hayo kuruhusu vyama vya siasa ambavyo havina wabunge wala madiwani kupewa ruzuku, pia ametaka sheria iruhusu kufanyika kwa mikutano ya siasa ili kuweza kujenga vyama hivyo. Kauli hiyo ya Mrema inakuja ikiwa imepita wiki baada ya kuvishambulia vyama vya upinzani vilivyokutana visiwani Zanzibar vilipokuwa vinazungumzia…

Source

Share:

RAIS MAGUFULI ATATUA TATIZO LILOASISIWA NA SERIKALI YAKE,NI LA VIKOKOTOO VYA MAFAO YA WAFANYAKAZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo ameuwa ndege wawili kwa wakati mmoja baada ya kutatua mzozo wa mda mrefu wa vikokotoo vya mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, vilivyokuwa vinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa viendelee kutumika kwa kila mfuko hadi mwaka 2023. Vikokotea hivyo vilipitishwa na Serikali yake hapo awali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) ambapo vilipigiwa kelele na wafanyakazi pamoja na wanasiasa wandamizi wakiongozwa na Zitto Kabwe huku baadhi ya Mawaziri wa Serikali yake walikuwa wakisifia ukokotoaji…

Source

Share:

Gumzo Shinyanga : MREMBO AMWENDESHA MME WAKE KWENYE TINGA TINGA WAKIFUNGA NDOA


Mrembo Lilian Peter Ndagiwe mkazi wa Shinyanga Mjini amezua gumzo wakati akifunga ndoa na Ottoh Yanga baada ya kupanda na kuendesha Tinga Tinga /Katapila ambalo hulitumia katika kazi zake katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Wanandoa hao wamepanda kwenye tingatinga hilo muda mfupi baada ya kufunga ndoa leo Disemba 28,2018 walipomaliza kufunga ndoa katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Buhangija mjini Shinyanga.

Kama ilivyozoeleka kuwa wanandoa hupanda kwenye magari lakini Wanandoa hao wameamua kupanda kwenye tinga tinga la kutengeneza barabara na kupita nalo mtaani. 

Imeelezwa kuwa bibi harusi Lilian Peter ni mtaalamu wa kuendesha tingatinga, kutokana na mahaba aliyonayo kwenye kazi yake ,ili kukamilisha furaha yake ya ndoa basi kaamua kuendesha Tinga Tinga na hakuona haja ya kupanda kwenye gari na mmewe.

Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha hapa chini

Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akijiandaa kupanda kwenye tinga tinga
Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akipanda kwenye tinga tinga
Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe  na bwana harusi Otto Yanga wakiwa kwenye tingatinga
Bibi Harusi Lilian Peter Ndagiwe akiendesha tingatinga
Wakipita mtaani na tingatinga lao

Msafara wa harusi
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

KAULI 22 ZA RAIS MAGUFULI AKIFUTA KIKOKOTOO LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza vikokotoo vya mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii, vilivyokuwa vinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa viendelee kutumika kwa kila mfuko hadi mwaka 2023

Tazama hapo chini nukuu ya maneno yote aliyoyasema leo 

1. Nimewasikiliza, kimsingi lina umuhimu, na ndio maana nimeona niwaite, na hasa kwa sababu nimekuwa nikisikiliza maelezo hata ya regulator, yanakuwa too academic. 

2.Ukishatoa maelezo ambayo ni too academic, unaelezea wastaafu, na kustaafu ni sifa na heshima, ulifanya kazi yako kwa uadilifu mkubwa, umesacrafice maisha yako kwa ajili ya kazi. 

3. Unapoona hiyo heshima inakuwa karaha, mateso, inafrustrate kwa mfanyakazi yoyote, sasa mimi siko hapa kumfrustrate mtu, kwani hata mimi nilikuwa mfanyakazi. 

4.Tuliamua kuunganisha mifuko, tulikubaliana NSSF ufanyiwe marekebisho, hatua hii ilitokana na ombi la muda mrefu la vyama vya wafanyakazi waliotaka hii mifuko iunganishwe. 

5.Mifuko ya jamii yote ilikuwa na hali mbaya, kwa sababu haikuwa coordinated, waendesha mifuko wote walikuwa wanapigana vita, wanagombania wanachama, walikuwa hawapendani. 

6.Mingine ilikuwa ikiendeshwa kiajabu, pakawa panaanzishwa miradi ya kiajabu, na miradi mingi ilikuwa ya majengo, nenda Kigamboni kaangalie yale majengo ya ndege vilaje, its a huge thing'. 

7.Tulipongia madarakani tulikuta deni trilion 1.2, serikali yenyewe haijachangia hii mifuko, waliostaafu kwa wakati ule ilikuwa ni shida, kwani hata ile michango ya serikali haitekelezwi. 

8.Tukaanza kulipa madeni, mpaka mwezi Machi mwaka huu madeni yote yalikuwa yamemalizika kulipwa. 

9.Matatizo yapo lazima tuende kwenye solution, kile kikokotoo angalau imefika 50%, lakini pia hata hawa walioko chini ilifaa ipande, hata hiyo formula inachanganya zaidi.


10.Mishahara mingi ya wafanyakzi serikalini si mizuri, anapofika mwisho unampa kidogo kidogo haingii, si unipe tu yote nikafie mbali, nilipokuwa nachangia hukuniambia, leo nachukua unaniambia nachukua kidogo, hata logic haingii. 

11.hata hawa Mawaziri, wabunge wanachukua hela yao yote, halafu uwaambie utachukua kidogo kidogo kila ukija, hawatakubali, kwenye reality, hata mimi hainingii. 


12.Tunahitaji watu wetu wapate fedha nyingi walipwe, lakini pia tunahitaji huu mfuko usife, hii formula haipo duniani, mtu anamaliza halafu kiwango chake unakizidisha mara 4, haipo.

13. Walioweka formula hii ni makatibu wakuu wa wakati ule, wa wakati wangu hawawezi, kwa sababu kwenye ile mifuko wengine ni beneficiary, ni kosa walifanya. 

14. Hifadhi za jamii zipunguze matumizi ya hovyo, kama mtu anastahili kulipwa 60% hatuwezi kumlipa kwa sababu hifadhi zinafanya matumizi ya hovyo. 

15. Kwa mfano kuna mfuko mmoja unachapisha kalenda kwa 1.3 bilion, hiyo hiyo imeajiri walinzi ambao ni very expensive, wanawalipa bilioni 2 kwa mwaka, wakati wangeajiri SUMA JKT wangewalipa chini ya bilioni 1 kwa mwaka. 

16. Uwekezaji kama ule wa Dege Heko village haufai, ukatumia fedha za wanachama bila ridhaa zao, halafu leo wastaafu uwaambie hamna hela formula imekataa. 

17. Mifuko muweke utaratibu mzuri, ni suala ambalo haliingii akilini nikasubiri mpaka nitakapofika miaka 60 ndio nipate mafao yangu, nimetoa michango yangu, kwanza hayupo atakaye nikumbuka kama nilifanya kazi, hata contructor atakuwa kashakwenda kwao. 

18. Kustaafu sio dhambi, kustaafu ni heshima, lazima awe respected, mwalimu amefundisha ameharibu na macho kutokana na chaki, halafu umpe condition. 

19.Mazungumzo yenu yote nimeyasikia, mimi nimeamua, angalau tuwe na kipindi cha mpito, kikokotoo kilichokuwa kinatumika kwa kila mfuko kabla ya mifuko kuunganishwa, tuendelee katika kipindi cha miaka ya mpito. 


20. Mtu anayestaafu anatakiwa kuheshimiwa, amelitumia taifa hili, amesacrafice, ni shujaa, kustaafu bila kufukuzwa ni heshima, hatakiwi kupata shida, nimeamua kikokotoo kiendelee katika kipindi hiki cha mpito, ambapo ni hadi mwaka 2023. 

21. Mifuko hiyo itakuwa imetengamaa, ni matumaini yangu, nitaichungulia kweli kweli hiyo mifuko, na Waziri natoa maagizo yake, wachungulie kweli, ili kusudi watu wasitumie hovyo hovyo, hii ni mifuko ya wanachama. 

22.Formula nzuri ni zile zinazo wapromote wafanyakazi, ndio ninazozitaka mimi, formula zinazowanyima haki wafanyakazi sio formula nzuri, ninashukuru katika kipindi hiki kifupi cha kuunganisha mifuko tumeanza kuona matokeo.
Share:

Breaking : RAIS MAGUFULI ATATUA UTATA WA KIKOKOTOO CHA MAFAO..AONDOA STRESS ZA WASTAAFU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuendelea kutumika kwa kikokotoo kilichokuwa kinatumika zamani.

Rais Magufuli ametoa uamuzi huo leo tarehe 28 Desemba 2018 alipokutana viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mawaziri wa wizara husika, kwa ajili ya kujadili masuala yahusuyo mafao ya wafanyakazi ikiwemo kuhusu kanuni mpya ya kukokotoa mafao ya wastaafu.

Vyama vilivyokutana na kuzungumza na Rais Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA), vyama shiriki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSD na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Kanuni mpya ya kikokotoo iliyotolewa hivi karibuni na serikali, ambayo inaelekeza wastaafu kulipwa mkupuo wa asilimia 25 ya mafao pindi watakapostaafu na asimilia 75 inayobaki watakuwa wakilipwa kama pensheni ya kila mwezi.

Baada ya kikokotoo hicho kutangazwa kwa umma, baadhi ya vyama vya wafanyakazi ikiwemo TUCTA, viliipinga kanuni hiyo kwa maelezo kwamba inakandamiza wafanyakazi.
Share:

Utafiti : NDOA NYINGI HUVUNJIKA BAADA YA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

Utafiti uliofanywa na wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Washington nchini Marekani umebaini kuwa ndoa nyingi huvunjika baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Wasomi hao ambao ni Profesa Julie Brines na Brian Serafini wanasema shinikizo la sherehe za Krismasi mara nyingi huathiri ndoa iwapo mambo yaliyopangwa na familia yakishindwa kutimizwa.

“Lakini ndoa zenye matatizo zenyewe hudhani kuwa sikukuu ni wakati mzuri wa kuimarisha uhusiano na kuanza upya. Wanafikiri kuwa na Krismasi yenye furaha pamoja na familia zao au kuwapeleka watoto safari. Watu wanakuwa na matarajio mengi licha ya changamoto walizokuwa nazo siku za nyuma,” anasema Profesa Brines.

Wanaeleza kuwa endapo matarajio hayo yasipotimia, huongeza mivutano ya kifamilia na kuvunjika moyo kwa wanandoa, jambo linalosababisha baadhi yao kutengana kabisa.

Pia, wanasema masuala ya kifedha wakati wa Krismasi huchangia hali hiyo kutokana na mazoea ya wengi kutumia fedha kiholela na baada ya sherehe kumalizika hukumbana na hali ya ukata inayosababisha migogoro ya kifamilia.

“Hii inatokana na kuwa baada ya sherehe za mwisho wa mwaka, mahitaji ya fedha huongezeka kwa sababu ni msimu wa kupeleka watoto shule, kulipa kodi za nyumba na mambo mengi yanayohitaji fedha,” anasema Profesa Serafini.

Anasema tabia ya watu wengi kuamua kusherehekea sikukuu hizo kwa gharama za kupindukia hususan katika vilevi, imetajwa kuwa kishawishi cha wengi kushiriki ngono ovyo suala ambalo ni tishio kwa ndoa na mahusiano ya wapenzi ambao bado hawajafunga ndoa.

Mtaaalamu wa saikolojia, Charles Nduku anasema kwa hapa nchini mambo hayo hutokea kutokana na watu kuwa na furaha kupindukia baada ya kusubiri kwa muda mrefu.

Anasema hali hiyo husababisha watu kutumia hata akiba ya fedha kwa ajili tu ya sherehe, jambo ambalo huwafanya kuathirika kiuchumi baada ya sherehe.

“Mara nyingine ni kukosa self-control (kujidhibiti) kwa mtu binafsi kwa sababu kuna maisha hata baada ya sikukuu. Ikifika sikukuu watu wanalewa, wanachepuka kiholela na mara nyingine ni kama kuiga kwa sababu kila mtu anafanya hivyo,” alisema Nduku.

Share:

Video:MCHEZAJI WA MANCHESTER KATULETEA VIDEO YA WIMBO WAKE 'NO LOVE'

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na sasa akiitumikia klabu ya Lyon ktoka nchini Ufaransa pia akiitumikia timu yake ya taifa ya Uholanzi Memphis Depay ameachia video ya wimbo wake.

Mchezaji huyo ambaye alishawahi kujihusisha na mambo ya muziki kwa mara kadhaa, kwa wakati huu ameamua kuwa serious kweny muziki na kuamua kuachia video ya wimbo wake wa “No Love”.

Wengi wamekizungumzia hiki kwamba huenda ni kwasababu ameachwa na mpenzi wake ambaye inasemekana anatembea na msanii kutoka nchini Marekani Trey Sonngs

Share:

MALI ZA JOKATE KUPIGWA MNADA NDANI YA SIKU 30


Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imezuia Makontena zaidi ya 1000 Bandarini, ambayo yanaonekana kuwa ni ya baadhi ya vigogo na makampuni makubwna na endapo hayatolipiwa ndani ya siku 30, yatapigwa mnada.

Baadhi ya taasisi hizo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Inspekta Jenerali wa Polisi, Klabu ya Simba ya Dar es salaam na kampuni ya Kidoti, inayomilikiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Kupitia tangazo la Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Usaje Asubisye, kwenye gazeti la serikali la Daily News la Disemba 19, limeorodhesha mali na wamiliki wake huku likitoa siku 30 kuziondoa.

“Mamlaka ya Mapato inautangazia Umma kuwa bidhaa zilizoorodheshwa zitatambuliwa kuwa zimetelekezwa endapo hazitaondolewa kwenye maeneo ya forodha ndani ya siku 30”, limesema tangazo hilo.

Kampuni ya Kidoti inayojishughulisha na urembo, iliagiza kontena namba HJCU2320135 la nywele bandia (hair weaves) ambazo zimekwama bandarini hapo.

Kukwama kwa makontena hayo bandarini kumekuja ikiwa ni miezi mitatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kukumbana na mkasa kama huo baada ya kuagiza makontena 20 yenye samani aliyodai yalikuwa kwa ajili ya shule za mkoa wake.

Makonda alitakiwa kulipa ushuru wa shilingi bilioni 1.2, jambo ambalo lilikuwa gumu kutekelezeka na baadaye TRA ililazimika kuzigawa samani hizo baada ya minada takribani mitatu kukosa wateja.
Share:

MBUNGE WA CCM AMTEMBEZEA KICHAPO MWANANCHI

Waziri wa zamani wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, ameingia matatani baada ya kudaiwa kumshambulia mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam, Kassim Abdallah (37) hadi kusababisha alazwe Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe (CCM), anadaiwa kutenda tukio hilo Jumatatu wiki hii eneo la Vingunguti, wilayani Ilala.

Abdallah ambaye ni dereva, hivi sasa amelazwa Muhimbili akipatiwa matibabu ya majeraha. Aliumia kichwani na sehemu nyingine za mwili.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Abdallah aliyelazwa wodi namba 18 ya wagonjwa binafsi kwenye jengo la Sewahaji, alisema alikumbwa na mkasa huo Jumatatu usiku alipokuwa katika harakati za kwenda kuegesha gari ofisini kwao.

Dereva huyo alikuwa akitoka safarini Rwanda na alisema ‘yard’ yao iko jirani na baa ya Titanic mahali ambako tukio lilitokea.

“Ilikuwa saa 6 usiku, nilikuwa nakwenda kuegesha gari na yeye (Simbachawene) alikuwa ameegesha gari jirani na baa, nilisimama mbali kidogo nikamuwashia taa, alifungua mlango akatoka na kuniambia nitulie.

“Nilidhani labda atasogeza gari, alikuwa amekaa ananiangalia, nilimuwashia tena taa, lakini alitoka na kuanza kucheza,” alisema Abdallah.

Alisema baada ya kuona mbunge huyo hajasogeza gari, aliamua kuwaomba vijana wa bodaboda waliokuwa jirani na eneo hilo wasogeze pikipiki zao ili aweze kupita.

“Niliporudi nyuma nilimuona kwenye kioo cha pembeni anakuja, nilikaa usawa wa geti nikapiga honi mlinzi aje afungue.

“Wakati najiandaa kuingia ndani nikaona meneja wake amenifuata akawa anasema mkuu (Simbachawene) analalamika nimepita karibu na gari lake.

“Nikamwambia sijaligusa, ghafla nikaona Simbachawene amekuja na kundi la watu akiwamo mwanawe Daudi.

“Akaniambia mimi ni jeuri, nikamuuliza kwanini, akasema kwanini nipite karibu na gari lake, atanionyesha adabu… akanizaba kibao, watu wakinizuia nisifanye chochote, nikaona busara nitulie tu,” alisema.

Kwa mujibu wa Abdallah, pia alishambuliwa na watu aliodai kuwa ni walinzi wa baa hiyo na mtoto wa mbunge huyo.

“Daudi (mtoto wa Simbachawene) alining’ata mkono wa kushoto na wengine walikuwa wananipiga bakora na marungu mikononi na kichwani,” alisema.

Abdallah alisema vijana wa bodaboda waliokuwa jirani walishirikiana na utingo wake na kumsaidia akainuka kisha kumpeleka katika Kituo cha Polisi Buguruni.

Alisema alitoa taarifa katika kituo hicho kisha kupewa fomu ya matibabu (PF3) na RB namba 11587/2018 ya shambulio la kudhuru mwili ambayo MTANZANIA imefanikiwa kuiona.

Abdallah alisema bado anasikia maumivu makali mwilini, hasa sehemu za kichwani na mikononi.

Sehemu ya kichwani alikuwa na alama ya kipigo na mkono wa kushoto pia ulikuwa umevimba ukiwa na alama za fimbo.

SIMBACHAWENE

Akizungumza na MTANZANIA jana, Simbachawene alikiri kufahamu tukio hilo na kusisitiza kuwa hakuwapo wakati kijana huyo anapigwa.

“Ni kweli kulitokea tukio hilo siku ya tarehe 23, huyo kijana alipotoka na gari lake aliingia katika mazingira ambayo alikuwa na fujo.

“Na pale ni pembamba, akaingia na gari kama anapita kwenye barabara kubwa na kila mtu alihamaki, vijana wa bodaboda, wateja na mimi nilikuwa mmojawapo katika watu waliohamaki.

“Nilikuwa ndio naanza kuondoka, kosa lililotokea ni kwamba viongozi wa pale kwenye baa hawakuwa ‘active’ kama siku zote, kwamba mtu anapoleta fujo wanawahi kuripoti polisi.

“Wakati linatokea hilo mpaka anachapwa na walinzi mimi nilikuwa nimeshaondoka, kwahiyo sikujua kilichotokea nyuma. Mpaka kijana wangu alipokuja kukamatwa ndio nilipata taarifa ya kilichotokea jana yake,” alisema.

Alisema aliitwa kwenda kutoa maelezo polisi na alitii wito huo kwani tuhuma si kitu cha ajabu.

“Nilipigiwa na polisi, nimeenda nimetoa maelezo kwa sababu ni tuhuma na si kitu cha ajabu, kwahiyo taratibu za kisheria zimefuatwa, hivyo wanaendela kupeleleza,” alisema.

Hata hivyo, Simbachawene alisema wameanza mazungumzo ya kifamilia kwa sababu anafahamiana na kijana huyo na ndugu zake.

“Tuko pamoja geti hili na lile, ananifahamu lakini hata magari yangu yanaegeshwa kwenye ‘yard’ yao, tunaweza kuingia kwenye ligi isiyokuwa na sababu,” alisema.

Share:

MKUU WA MAJESHI AOMBA VIONGOZI WA DINI KUDUMISHA AMANI..ASKOFU SANGU ANENA

Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano.

Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama na Serikali, ambapo alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo kwa Taifa lolote duniani.

“Suala la amani na utulivu ni la msingi sana katika nchi yetu, kwa vile kila mwananchi ana dini yake tunaamini kuwa viongozi wa dini zote kwa kuwa wanasikilizwa sana na waumini wakiweka msisitizo katika suala la amani, amani itatawala na kutakuwa na utulivu”

“Utulivu huu tunauhitaji sana ili tupate maendeleo, kama viongozi wetu wa kisiasa wanavyosisitiza kuwa tudumishe amani na utulivu tupate maendeleo, bila utulivu watu wakiwa wanahaingaika hakuna maendeleo kwa sababu hakuna shughuli mtu anaweza kufanya kama hana amani na utulivu, hivyo hataweza pia kuleta maendeleo yake, familia, jamii na Taifa kwa ujumla” alisema Jenerali Mabeyo

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro amesema vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na uhalifu ikiwemo ukataji wa mapanga na mauaji ya vikongwe na yanachangiwa na watu kukosa hofu ya Mungu; hivyo nyumba za ibada(makanisa na misikiti) zinapojengwa kwa wingi zitakuwa msaada mkubwa sana kwa watu kuwa na hofu ya Mungu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema jamii inayoamini uwepo wa Mungu haiwezi kuwa na vitendo vya kisasi, kukatana mapanga na mauaji ya vikongwe huku akiwaasa Watanzania kukaa kwa amani na upendo bila kufanya mambo yanayoweza kuhatarisha amani.

Akibariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega, Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Muhashamu Liberatus Sangu amewataka Watanzania kupendana na kuacha roho ya ubinafsi na visasi.

Aidha, Askofu Sangu ametoa wito kwa viongozi na waumini kufanya nyumba za ibada zibaki nyumba za sala kama yanenavyo maandiko matakatifu na kamwe zisitumike kama majukwaa la wanasiasa.

” Palipo na msamaha pana umoja, uelewano na usawa lakini palipo na kisasi hapana maendeleo; nyumba ya ibada isitumike kama jukwaa la Wanasiasa alisisitiza Muhashamu Askofu Sangu.
Share:

MUME AUA MKE KWA WIVU WA MAPENZI BAA

Jeshi la Polisi mkoani Kagera, linamshikilia Kamugisha Kadodi (32), kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Kemilembe Paulo (30) na kusababisha kifo chake, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.

Mwanamke huyo alipigwa na mumewe wakiwa katika baa walipokwenda kunywa pombe ambapo mtuhumiwa alianza kumtuhumu mkewe kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamme mwingine.


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, alisema tukio hilo la mauaji lilitokea Desemba 25, mwaka huu saa 11 jioni katika Kijiji cha Kigorogoro kilichoko mpakani mwa Tanzania na Uganda Wilaya ya Kyerwa.


Kamanda Malimi alisema siku ya tukio wanandoa hao waliondoka pamoja kwenda kunywa pombe baa kama sehemu ya kusherehekea sikukuu ya krismasi na wakiwa kule, ghafla ulizuka ugomvi uliosababisha mwanamke huyo kupigwa hadi kupoteza maisha pale pale.


Alisema mtuhumiwa huyo wa mauaji amekuwa akimtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamme ambaye hajafahamika ambaye Jeshi la Polisi bado linamfuatilia.


‘Mtuhumiwa tumemkamata kwa mahojiano zaidi, baada ya uchunguzi tutamfikisha mahakamani ili akakabiliane na mashtaka yatakayofunguliwa dhidi yake,” alisema.


Katika tukio la pili, Kamanda huyo alisema Justus Clemence (42), mkazi wa kitongoji cha Itokozi wilayani Biharamulo, alipoteza maisha baada ya kupigwa na watu waliomtuhumu kuiba kondoo wa mwanakijiji mwenzao.


Kamanda alisema uchunguzi unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata waliohusika na mauaji hayo.


Katika tukio lingine, Kamanda Malimi alisema mtoto mmoja wa kiume aliokolewa juzi usiku kutoka katika shimo la choo, alikotupwa na mama yake mzazi muda mfupi baada ya kujifungua.


Kamanda Malimi alisema tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Mramba Kata Kihanga wilayani Karagwe na kwamba mtuhumiwa, Alisia Philemon (17), ameshakamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi.


Kamanda alisema kwa mujibu wa utetezi wa mtuhumiwa huyo, alifikia uamuzi huo baada ya kupewa ujauzito na mtu ambaye alimtelekeza.


“Tumeanza kumfuatilia mtu huyo anayedaiwa kuhusika na kumpa ujauzito huyu msichana ili atakapokamatwa afikishwe katika vyombo vya sheria,” alisema.
Share:

Thursday, 27 December 2018

JENERALI MABEYO ATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI KUHUBIRI AMANI.

  Na Stella Kalinga, Simiyu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa Viongozi wa Dini nchini kuendelea kuhubiri amani ili kujenga jamii iliyo bora yenye kudumisha upendo na mshikamano.   Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa ibada ya kubariki na kutabaruku Kanisa la Mtakatifu Petro, Kigango cha Kiloleli Parokia ya Ilumya wilayani Busega ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dkt. Benard Kibese na viongozi wengine wa Chama…

Source

Share:

MOTO WATEKETEZA VYUMBA VINNE WILAYANI NJOMBE

Na Amiri kilagalila Moto mkubwa umewaka ghafla kwa nyakati tofauti na kuteketeza vyumba vinne katika nyumba ya mkazi mmoja wilayani Njombe aliyefahamika kwa jina la Fedrick kitalula na kusababisha hasara kubwa ya samani zilizokuwemo katika vyumba hivyo. Akizungumza na mtandao huu mmiliki wa nyumba hiyo ndugu Fedrick kitalula ambaye ni mtumishi (katekista) wa kanisa la Roman kathoriki lililopo kijiji cha kichiwa huku yeye akiishi kijiji cha Ilunda kilichopo kata ya mtwango wilayani Njombe,amesema kuwa moto huo awali ulianza kuwaka katika chumba anacholala mtoto wake wa kiume na kufika katika vyumba…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger