Thursday, 27 December 2018

KRISMASI YAONDOKA NA WANNE KAGERA..YUMO ALIYEUAWA KWA MAPENZI,PIA MWIZI WA KONDOO

Watu wanne wamefariki dunia mkoani Kagera katika kusherehekea sikukuu za Krismasi na siku ya Boxing Day , kufuatia matukio manne yaliyotokea kwa nyakati tofauti mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi, lipo tukio la Desemba 25 katika kijiji cha Kigorogoro wilaya ya Kyerwa, mwanamke alipigwa na mpenzi wake wakati wakisherehekea sikukuu hiyo kwenye moja ya majumba ya starehe, ambapo mwanaume huyo alimtuhumu mpenzi wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Katika tukio la pili Kamanda huyo amesema kuwa Justus Clemence mwenye umri wa miaka 42 mkazi wa kitongoji cha Itokozi wilayani Biharamulo anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili, alipoteza maisha baada ya kupigwa na watu waliomtuhumu kuiba kondoo wa mwanakijiji mwenzao.

Aidha kamanda huyo amesema kuwa bibi aliyetambuliwa kwa jina la Magdalena Martine mwenye umri wa miaka 75 amefariki Desemba 25 mwaka huu saa tisa mchana katika kijiji cha Migara Bukoba vijjini, baada ya kulipukiwa na moto wakati akipika katika jiko lake lililoezekwa kwa nyasi na kuwa alifariki kutokana na moto kumzidi nguvu.

Pia kamanda Malimi amezungumzia tukio jingine la Ronald Hitiman raia wa Rwanda ambaye amepoteza maisha Desemba 26 baada ya kujinyonga katika chumba chake alimokuwa akiishi katika mtaa wa Kamizilente kata Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba.

Chanzo - EATV
Share:

WATUMISHI WAMKERA WAZIRI MKUU...KESHO KUKUTANA NA MAWAZIRI NA MAKATIBU WOTE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali lililoko Ihumwa na kubaini kuwa baadhi ya wakandarasi hawaendi na kasi inayotarajiwa na Serikali.

Waziri Mkuu ameamua kuitisha kikao cha Mawaziri wote na makatibu wakuu wote kesho (Ijumaa) saa 5 asubuhi ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini.

Ametoa agizo kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 27, 2018) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Mtumba lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

“Nimekagua maeneo yote na kukuta baadhi ya wakandarasi wanatakiwa kujenga majengo ya wizara nne hadi tano. Sijaridhika na baadhi ya kazi, nimeitisha kikao cha Mawaziri wote kesho ili tuangalie ni mkandarasi yupi anaweza kumudu hii kazi.”

“Nimebaini kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kama kokoto, nondo, matofali na kikao cha kesho kitahusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, viongozi wa Mkoa na Jiji la Dodoma, wakandarasi wote ili tukubaliane kazi hii inaisha lini,” amesema.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu amesema wajasiriamali wanaotengeza matofali Dodoma wako wengi lakini matofali tyao yako chini ya kiwango, kwa hiyo wanatakiwa watu wa kutengeneza matofali mengi yenye uimara. “Tuna ujenzi wa wizara 24, tunataka matofali imara siyo yale ambayo ukilishika tu, mchanga unamomonyoka,” amesisitiza.

Akisisitiza uharaka wa kazi hiyo, Waziri Mkuu amesema kazi hiyo ina malengo maalum na inatakiwa ikamilike haraka sana. “Tarehe ya mwisho ya kukamilisha ujenzi iliyotolewa na Mheshimiwa Rais ilikuwa Desemba 31, mwaka huu lakini kuna sababu zimetajwa kukwamisha ujenzi huo zikiwemo mvua na uhaba wa kokoto,” amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesifia kazi nzuri iliyofanywa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Utumishi, Ujenzi, Katiba na Sheria, Maji na Elimu. Kazi hizo zimefanywa na wakandarasi ambao ni Magereza, SUMA JKT, Wakala wa Majengo (TBA) na Vikosi vya Ujenzi vya Mwanza na Dar es Salaam vilivyoko chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Wakandarasi walioboronga ni JWTZ – Mzinga, National Housing na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Waziri Mkuu amemwagiza Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe ahakakishe anapokea taarifa kutoka kila taasisi inayohusika na ujenzi huko Ihumwa na akishaijumuisha, aiwasilishe kwake ifikapo leo jioni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi ashirikiane na Mkurugenzi wenzake wa Chamwiono kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa za ajira kwenye mradi huo.

“Mkurugenzi wa Jiji wasiliana na Mkurugenzi mwenzako wa Chamwino mhakikishe vijana na akina mama wanakuja kufanya kazi hapa. Pia itisha kikao cha^ waandishi wa habari uwaeleze wananchi wako fursa zilizopo, kuanzia ufyatuaji wa matofali, uuzaji wa nondo, kokoto na utengenezaji wa pavement blocks, hizi zote ni fursa, tuna wizara 24 na mahitaji ni makubwa,” alisisitiza.

Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Anthony Mavunde alisema zoezi la kusafisha eneo la ujenzi wa mji wa Serikali lilianza Novemba 28, mwaka huu.

Alisema wizara zote zimepata viwanja na zimeanza ujenzi isipokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) ambao bado wanasubiri kupatiwa fedha.

Alisema kazi ya ujenzi wa Mji wa Serikali inasimamiwa na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Share:

WAZIRI MHAGAMA AANIKA MIKOA 11 YENYE MABARAZA YA BIASHARA

Na. OWM, Kigoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameitaja mikoa 11 ambayo ilianzisha mabaraza ya Biashara na hadi sasa yako hai na kubainisha kuwa mikoa mingine ilitekeleza agizo la kuanzisha mabaraza hayo tu lakini utendaji wa Mabaraza hayo umekuwa siyo endelevu.

Waziri Mhagama ameitaja Mikoa hiyo 11 ambayo Mabaraza yake yako hai hadi sasa kuwa ni Dodoma, Kigoma, Tanga, Geita, Morogoro, shinyanga, Dar es Salaam, Pwani, Iringa, Songwe na Mbeya. Aidha, Mhagama amebainisha kuwa Mikoa mingine ambayo mabaraza yake hayafanyi vikao inakiuka Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 unaosisitiza kuanzishwa kwa mabaraza hayo na utendaji wake kuwa endelevu.

Akiongea wakati wa kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Baraza la Taifa la Biashara mkoani Kigoma, Waziri Mhagama alifafanua kuwa Dhumuni kuu la kuanzisha mabaraza ya biashara hususani katika ngazi ya wilaya na mikoa ni kuweka mfumo rasmi wa kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali na Sekta Binafsi katika kila ngazi ya utawala, kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa ajili ya kukuza sekta binafsi ambayo ndio muhimili muhimu wa kukuza uchumi wa nchi.

“Hatuwezi kuwa tunamshuhudia Mhe. Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli anaitisha vikao vya Baraza la Taifa la Biashara katika ngazi ya Taifa lakini katika ngazi ya mkoa na wilaya hamtekelezi maagizo hayo, lazima mabaraza yakutane ili kutatua kero za wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi ya mkoa na wilaya, lakini pia itasaidia kuibua fursa za uwekezaji na kuzinadi fursa hizo, na sisi tumeamua kukagua mkoa mmoja baada ya mwingine ili kupunguza kero za wafanya biashara na wawekezaji” Amesema Mhagama

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati Waziri Mhagama alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Mkoa la Biashara, Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga , Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Samson Anga na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Rashid Mchata, walieleza kuwa kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC), wameweza kuimarisha mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi kupitia Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya.

Naye Mratibu wa Mradi huo, Andrew Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa unaboresha mazingira ya Biashara na uwekezaji nchini tayari kwa kushirikiana Baraza la Taifa la Biashara wameandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na yenye ufanisi.

Baraza la Taifa la Biashara lilianzishwa kwa Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2001 na kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 39 la tarehe 28 Septemba 2001. Baraza hilo ni jukwaa la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, na lengo kuu la Baraza ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa njia ya majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share:

YANGA HII NI “IYENA IYENA TU” MBEYA CITY ISUBILI KUUMIA

MABINGWA wa Kihistoria timu ya soka ya Yanga,wamepania kuhakikisha wamlalua kila anayekuja mbele yake baada ya kuhaidi kuzitumia dakika ngumu 180 kuthibi­tisha kwamba hawakuwa wakibahati­sha kwenye mzunguko wa kwanza. Watoto hao wa Jangwani ambao Kikosi chao hicho kinanolewa na cha mwenye maajabu yake , Mwinyi Zahera hadi sasa kimecheza mechi 17 na kati ya hizo imeshinda 15 ikiwa imepata alama 47. Lakini kibarua kizito kinakuja kukamilisha mzunguko wa kwanza. ambapo ni ni dhidi ya Mbeya City na Azam FC. Endapo Yanga itafanikiwa kushinda mechi hizo mbili, itakuwa imefikisha alama 53…

Source

Share:

BENARD MEMBE AGEUKA KUWA TISHIO KWENYE URAIS 2020,UVCCM WAIBUKA NA KUMKINGIA KIFUA JPM

NA KAROLI VINSENT NI wazi Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Benard Membe ni kama amekitikisa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu mikakati yake ya kuwania Urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 ndivyo naweza kusema,baada ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuibuka na kutaka Rais John Magufuli apewa nafasi tena ya Urais 2020. Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi waUmoja huo Hassan Bomboko, amesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais…

Source

Share:

SHABIKI AFARIKI UWANJANI KUTOKANA NA VURUGU


Shabiki wa Inter Milan amepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa katika mchezo dhidi ya FC Napol uliopigwa kwenye uwanja wa San Siro baada ya kuibuka vurugu kubwa kwa mashabiki wa pande zote mbili kabla ya mechi.

Taarifa kutoka nchini Italia zinasema kuwa mshabiki huyo alipoteza maisha kwa kugongwa na gari nje ya uwanja kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliocheza jana na kushuhudia Inter Milan kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Napol.

Katika mchezo huo ambao uligubikwa na vurugu nyingi ndani na nje ya uwanja kiasi cha kupelekea beki wa kati wa klabu ya Napol anaye windwa na Manchester United, Kalidou Koulibaly kutolewa nje ya uwanja baada ya kuoneshewa kadi mbili za njano.

Licha ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezaji huyo, mashabiki wa wa Inter Milan walionekana kufanya vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa beki huyo baaada ya kutoa milio kama nyani wakati mchezaji huyo anaposhika mpira uwanjani kiasi kilichompelekea kuandika ujumbe mzito katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Vitendo hivyo ambavyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuvipinga vikali lakini bado vinaonekana kushamili kwa wachezaji wenye ngozi nyeusi wanaocheza soka la kulipwa barani Afrika.
Share:

MWANAJESHI ANAYEDAIWA KUMUUA MWANAJESHI MWENZAKE ATAKA UPELELEZI UKAMILIKE MAPEMA


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Ramadhan Mkalu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukamilisha upelelezi wa kesi inayomkabili.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 27, 2018 katika mahakama hiyo baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Mshtakiwa huyo alinyoosha mkono mahakamani hapo na kuomba upelelezi kukamilika mapema.

Wakili wa Serikali, Neema Mbwana amedai mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Janeth Mtega kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine.

"Naomba uelewe kuwa upelelezi unafanywa na polisi hivyo sisi tunasubiri amalize ili tuweze kutenda haki," amedai wakili huyo.

Kufuatia maelezo hayo hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 8, 2019 itakapotajwa tena.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mlaku anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 30, 2017 eneo la Upanga, Makao Makuu ya JWTZ.

Mlaku ambaye ni mwanajeshi wa jeshi hilo katika kambi iliyopo Makongo anadaiwa kumuua mwanajeshi wenzake namba MT 79512, Sajenti Saimon Munyama.
Share:

UVCCM YAMUANIKA MGOMBEA URAISI 2020

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, kupitia kwa Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Hassan Bomboko, imesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais John Pombe Magufuli, anapewa nafasi ya kuwania tena Urais.
Kwa mujibu wa Bomboko kwenye kikao kitakachofanyka Dodoma Umoja huo hautakuwa na lengo jingine zaidi ya kumpitisha Rais Magufuli kuwania tena nafasi hiyo ya kukiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa awamu ya pili.

"Kama msemaji rasmi wa UVCCM, msimamo wa taasisi yetu ni kwamba hatuna na hatutakuwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais 2020 mwingine zaidi ya Magufuli ambaye ndiyo Mwenyekiti wa CCM" amesema Hassan Bomboko, UVCCM.

Aidha Bomboko amesema kuwa "mwaka 2020 tutakwenda Dodoma kwenye mchakato wa kidemokrasia Kukamilisha desturi yetu ya CCM ya kumbariki mgombea wetu kwa muhula wa pili, uchaguzi wa mgombea wa CCM tulishamaliza mwaka 2015"

"Kwa wenye nia ya kugombea Urais 2020 kupitia CCM watafute biashara nyingine ya kufanya kwani CCM hakuna Urais wa kupeana kiushemeji" ameongeza Hassan Bomboko.

Share:

MANARA ATUMA SALAMU KWA MWANA FA ,AMWAMBIA FERRARI NDIO HADHI YA MSEMAJI MKUBWA


Ikiwa imepita siku moja tu ,tangu klabu ya Simba kupata matokeo mabaya ya kufungwa jumla ya mabao 3 – 2 dhidi ya Mashujaa FC na kuyaaga mashindo ya Azam Sports Federation Cup (FA), mapema hii leo Afisa habari wake, Haji Manara ameonyesha gari jipya aina ya Ferrari huku akielezea kuwa msemaji mkubwa ndiye mwenye hadhi ya kutumia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameweka picha ya gari jipya aina ya Ferrari huku akiandika gari hilo ndio hadhi ya msemaji mkubwa mwenye ustaa wake.

”Engineer @mwanafa soma hyo!!, Yajayo ndio hayo madhee!!, Ferrari ndio hadhi ya msemaji mkubwa mwenye wastawa wakemjini!!, No Nzi wala lift,Dadadeki,” ameandika Manara kwenye mtando wake wa Instagram

Mkuu huyo wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Haji Manara ameonekana kwenye gari hiyo ya Ferrari ya rangi nyekundu.
Share:

RUSSIA:HATUKOSI USINGIZI HATA KIDOGO KWA VITISHO VYA MAREKANI

Moscow, RUSSIA. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Ryabkov, ametangaza kuwa nchi yake haishughulishwi na matamko na amri iliyotangazwa na Marekani kutekeleza vitisho vyake kuhusu kujitoa katika Mkataba wa Silaha za Masafa ya Wastani za Nyuklia (ANF). Waziri Ryabkov amenukuliwa na shirika la habari la RIA Novosti akisema hayo na kuongeza kuwa mkataba wa ANF uko wazi na umekuwa ukitangazwa waziwazi hadharani, hivyo, vitisho na amri zinazotolewa na Marekani kuhusu mkataba huo hazikubaliki kabisa. Marekani inaituhumu Russia kuwa inakanyaga vipengele vya mkataba wa ANF, hivyo Marekani imeamua…

Source

Share:

CHUPA ZA DAMU 601 ZINAHITAJIKA MKOANI NJOMBE ILI KUKIDHI MAHITAJI

Na Amiri kilagalila Zaidi ya chupa za damu 550 zinahitajika mkoani Njombe ili kukidhi mahitaji yote kwa mwezi ambapo jumla ya chupa 470 tu kati 601 ndio zinazo kusanywa huku kukiwa na upungufu wa chupa 131 hali inayowalazimu waratibu wa damu salama kuiomba jamii kujitokeza katika zoezi la uchangiaji ili kuwasaidia wenye mahitaji hayo. Akizungumza na mtandao huu wakati jeshi la polisi pamoja na waandishi wa habari wakichangia damu,Mratibu wa Damu Salama Mkoa wa Njombe Bi.Prisca Ndiasi amesema Wanalazimika Kuendesha Zoezi hilo Muhimu Kutokana na Upungufu Mkubwa wa Damu. “Mpaka…

Source

Share:

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA YAKANUSHA TUHUMA ZA FASTJET KUZUIWA KUINGIZA NDEGE TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Hamza S. Johari leo Disemba 27, 2018 amezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kampuni ya Fastjet kuzuiwa kuingiza ndege hapa nchini pamoja na tuhuma kibao walizozitoa wakidai AirTanzania inapendelewa.

==>>Hapo chini kuna nukuu ya mambo machache aliyoyasema. 

1.FastJet hawakuwa na ndege hata moja hivyo kama mamlaka ya TCAA hatuna budi kuwazuia, wanamadeni ya 6 billion japo wamelipa kidogo, lakini sheria inawataka walipe yote, hivyo kama wao wanahitaji kufanya biashara wafuate masharti na walipe madeni. 

2.Tulipata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba tarehe 22 Disemba 2018 wangeleta hizo ndege zao, lakini mamlaka haikuwa na taarifa hizo na wao utaratibu wa kuingiza ndege nchini wanaujua.


3.Ilipofika Tarehe 24 Disemba 2018 saa 6 mchana ndo wakatuma email ya maombi ya kuleta ndege hizo zenye usajili wa Afrika Kusin. 

4.Ikumbukwe kwamba, tarehe 25 ilikuwa ni sikukuu na tarehe 26 ilikuwa ni Boxing Day hivyo sote hatukuwa ofisini. Wanaposema et tumewazuia kuzileta ni waongo. 

5.Katika notisi ya siku 28 tuliyowapa, tuliwataka Fastjet walete andiko la kudhibitisha uwezo wa kufedha ili kuona kama wanajiweza na pia walete Meneja Mwajibikaji mwenye utaalamu na mambo ya ndege. Fastjet hawakuletea hivyo vitu


6.Badala yake Tar 24.12.2018 ndo sasa wakaleta maombi na barua ya mkurugenzi mtendaji wa Fastjet Lawrence Masha wakitujulisha kuwaLawarence Masha amejiteua mwenyewe kuwa accountable manager. 

7.Fastjet waache mzaha. FastJet itakufa kwasababu zao wenyewe maana wanamatatizo mengi, TCAA tunasimamia sheria ili kulinda usalama wa abiria, kulinda maslahi ya watoa huduma (supplies). Habari zote zilizoelezwa si za kweli ni upotoshaji mtupu.
Share:

BAADA TRUMP KUTUA KINYEMELA IRAQ, UBALOZI WA MAREKANI WASHAMBULIWA

Baghdad, IRAQ. Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad nchini Iraq umeshambuliwa kwa maroketi mapema leo Alhamisi masaa machache baada ya Rais Donald Trump kufanya safari ya kinyemela nchini Iraq akiandamana na mkewe. Vyombo vya habari na wafanyakazi katika eneo la al Khadhraa lenye ulinzi mkali katikati mwa Baghdad wanasema kuwa ubalozi wa Marekani mjini humo umeshambuliwa kwa maroketi mawili alfajiri ya leo. Duru hizo zinasema alfajiri ya leo kulisikika ving’ora vya tahadhari kutoka kwenye jengo la ubalozi wa Marekani baada ya shambulizi hilo ambalo bado hasara zake hazijajulikana. Shambulizi dhidi ya…

Source

Share:

DUH!! TUME YA UCHAGUZI DRC YAAHIRISHA TENA UCHAGUZI

Kinshasa, DRC. Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI) hapo jana iliahirisha uchaguzi katika miji mitatu nchini humo, uchaguzi wa rais na wa bunge uliopangwa kufanyika Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu hadi mwezi ujao wa Machi. Hatua hii inamaanisha kuwa kura za miji hiyo mitatu hazitajumuishwa katika mchuano wa kiti cha urais. Miji hiyo mitatu huko Congo ambayo uchaguzi umeahirishwa ni Beni na Butembo inayopatikana mashariki mwa nchi hiyo ambayo imekuwa ikisumbuliwa na homa ya Ebola tangu mwezi Agosti. Aidha, mji wa Yumbi magharibi…

Source

Share:

MAGAIDI NCHINI MALI KUKIONA, QATAR YAONGEZA NGUVU KUPAMBANA NAO

Bamako, MALI. Serikali ya Qatar imesema kuwa imetuma nchini Mali magari ishirini na nne (24) ya kijeshi kwa lengo la kile ilichokitaja kuwa kuzisaidia nchi za Afrika za eneo la Sahel kuendesha vita dhidi ya ugaidi. Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo na kuongeza kuwa, magari hayo ya kijeshi yatasaidia vita dhidi ya ugaidi na kudhamini hali ya usalama si nchini Mali pekee bali katika nchi zote za eneo la Sahel zinazojulikana kwa jina la G5. Nchi hizo za G5 ambazo ni Mali, Burkinafaso, Niger,…

Source

Share:

VIGOGO MABASI YA MWENDOKASI WAACHIWA KWA DHAMANA , BAADA YA KUKAA MAHABUSU KWA SIKU 60

Wafanyakazi saba wa Kampuni ya Uda-Rapid Transit (UDART), akiwamo kigogo wa idara ya fedha, wanaodaiwa kuhusika katika mtandao wa uhujumu wa mapato ya mabasi ya mwendokasi kwa kuchapisha tiketi feki kwa abiria wameachiwa kwa dhamana.

Hatua hiyo imekuja baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 60 na Jeshi la Polisi huku wakiendelea kusubiri uamuzi wa jalada lao ambalo lipo kwa mwanasheria mkuu wa Serikali, likisubiri hatima yao kama kufikishwa mahakama ama laa.

Pamoja na kuachiwa, wafanyakazi hao ambao awali walikuwa wanane wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi mara kwa mara huku upelelezi wa kesi yao ukiendelea.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa jana alisema tuhuma zinazowakabili wafanyakazi hao ni za kughushi na kuhujumu mapato ya mradi wa mabasi ya mwendokasi, hivyo upelelezi wake unachukua muda mrefu ili kuhakikisha wanapata mtandao mzima.

Alisema awali Jeshi la Polisi lilikuwa linawashikilia wafanyakazi wanane, lakini upelelezi ulipokuwa unaendelea, walilazimika kuwaongeza wafanyakazi wengine watatu.


“Tumelazimika kuwaachia kwa dhamana kwa sababu upelelezi wa kesi yao bado unaendelea, awali walikuwa wafanyakazi wanne, lakini tumelazimika kuongeza wengine watatu na kufikia saba,” alisema.

Mambosasa alisema jalada la watuhumiwa hao lipo mikononi mwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili aweze kulikagua na kuangalia taratibu za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa ili kufikishwa mahakamani.

Alisema upelelezi umechukua muda mrefu kutokana na tuhuma za kughushi zinazowakabili ambazo zimehusisha mtandao wa kihalifu.

Mambosasa alisema Jeshi la Polisi litaendelea kuwakamata na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria wale wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya kihalifu pamoja na kwenda kinyume na sheria za nchi.

Wafanyakazi wanane wa Udart walikaa mahabusu zaidi ya miezi miwili baada ya kukamatwa wakidaiwa wanajihusisha na mtandao wa tiketi za kughushi huku wengine 18 wakiachiwa kwa dhamana.

Awali, Kamanda Mambosasa alidai kuwa watuhumiwa hao wamefanya kosa la kuhujumu mradi wa Serikali ambao ni wa kitaifa na kimataifa kwa kutaka kufifisha jitihada za Serikali.
Share:

RAIS AL BASHIR ATISHIA KUWAKATA MIKONO WAANDAMANAJI

Khartoum, SUDAN. Rais Hassan al Bashir wa Sudan amekemea vikali maandamano ya mkate yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini humo dhidi ya serikali yake na kusema kuwa atakata mikono ya waandamanaji hao. Rais Al Bashir amesema kuwa atakandamiza vikali maandamano hayo na kwamba jeshi la Sudan litaharibu maisha ya waandamanaji na kukata mikono yao. Aidha, kiongozi huyo amesisitiza waziwazi kwamba, hatasalimu amri mbele ya matakwa ya taifa la Sudan au matakwa ya wasaliti. Vilevile amewatahadharisha Wasudani kuhusu kile alichokiita uvumi na kusema kuwa, mwenendo wa marekebisho umeshika njia…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger