Sunday, 23 December 2018

RAIS MAGUFULI AAGIZA WATUMISHI WA SHIRIKA LA NDEGE ATCL WALIOKATIWA TIKETI WAKATWE MISHAHARA

Rais John Magufuli amesema viongozi wa Serikali waliokatiwa tiketi ili wasafiri na ndege za Shirika la ATCL na kukaidi watakatwa pesa hizo katika mishahara yao.


Ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 23, 2018 wakati akipokea ndege mpya ya Airbus 220-300 ‘Dodoma’ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya abiria wamekuwa wakikosa tiketi kwa kuambiwa ndege imejaa ila wanapoingia ndani hakuna watu huku baadhi ya tiketi zikiwa za watendaji wa Serikali ambao hawasafiri.

“Mtumishi anatakiwa kusafiri kwenye ndege na amekatiwa tiketi na Serikali lakini hasafiri na kufanya ndege iende tupu, nimeshamwambia mtendaji mkuu aniletee orodha ya watendaji ambao hawakusafiri tuwakate hizo hela kwenye mishahara yao,” amesema Rais Magufuli.

“Nimeambiwa wanakadiriwa kuwa 100 kwa hiyo nina uhakika kufika wiki ijayo nitapata majina yao, mawaziri, wabunge ambao walikaa hadi saa ya mwisho ndege ikaenda tupu na hela za Serikali zikaenda,” ameongeza Rais Magufuli huku akisema tena anafikiri kesho Jumatatu yatamfikia.

Amesema watumishi hao wajiandae kurudisha fedha hizo kutoka mifukoni mwao ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wanaotumia fedha za Serikali vibaya.

“Niwaombe tu watendaji kama kuna tiketi ambayo haukuitumia leta tu hela mara moja ili mambo yaishe lakini ni matumaini yangu sasa katika suala hili la tiketi ATCL mtajipanga vizuri,” amesema Magufuli.
Share:

HII NDIYO NDEGE AIRBUS A220-300 ILIYOTUA TANZANIA...BONGE LA DUDE ..LINA NEMBO YA 'HAPA KAZI TU'

Share:

TSUNAMI YAUA WATU ZAIDI YA 160 INDONESIA


Watu 168 mpaka sasa wameripotiwa kupoteza maisha huku 750 wakijeruhiwa vibaya nchini Indonesia baada ya Tsunami kuikumba nchi hiyo siku ya jana usiku.

Mamlaka nchini humo zinasema Tsunami hiyo imetokea katika fukwe za visiwa vya Java na imesababishwa na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mlipuko wa volkano.


Msemaji wa Taasisi inayoshughulika na kuzuia majanga nchini humo, Sutopo Purwo Nugroho amesema mpaka sasa watu 30 hawajulikani walipo, huku nyumba 558, migahawa 60 ikibomolewa na Tsunami.

Nugroho amesema tukio hilo ni la kushtukiza, kwani hakukuwa na taarifa wala tahadhari yoyote ile iliyotolewa kwa wananchi.

Usiku wa Jumamosi siku ya tukio, Bendi ya muziki maarufu nchini humo ya Band Seventeen, ikiongozwa na msanii wa muziki, Riefian Fajarsyah nayo ilipatwa na kazia baada ya jukwaa lao kufunikwa na maji.


Kupitia ukurasa wa Instagram wa Riefian Fajarsyah amethibitisha kuwa watu wanne kutoka kwenye bendi yake wamefariki dunia.


Mwezi kama huu mwaka 2004, tsunami kama hiyo ilitokea katika bahari ya Hindi kufuatia tetemeko la ardhi, iliua zaidi ya watu 226,000 katika nchi 13 ikiwa 120,000 walikufa nchini Indonesia.
Share:

MAGUFULI : NAMSHANGAA SANA MUNGU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekiri kushangazwa na mambo Mungu anayoitendea Tanzania katiika kipindi hiki.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akihutubia katika mapokezi ya ndege aina ya 'Air Bus' A220-300 leo, Disemba 23 jijini Dar es salaam.

Amesema kwamba kwa baraka ambazo Mungu amekuwa akiipatia Tanzania ni wazi haitashikika na kwamba mambo yataendelea kunyooka sana.

"Nataka niwahakikishie kadiri tunavyoendelea Tanzania haitashikika tutakuwa juu mno. Tanzania tunaweza na tutaweza. Mambo yananyooka mno mpaka mimi namshangaa Mungu. Mungu anatupenda na yupo pamoja na sisi", - amesema.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema kwamba 'Air Bus' ni ndege ya kwanza katika nchi za Afrika kutua Tanzania. "ndege hii ni ya kwanza Afrika hakuna nchi yoyote kuanzia North au South ambayo ina ndege kama hii na sisi tumepiga mbili kwa mpigo".

Mbali na hayo Rais amemuagiza mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL kumpelekea majina ya watendaji wa Serikali 100 ambao wanakatiwa tiketi na Serikali lakini hawasafiri.

"Nimeambiwa kuwa baadhi ya tiketi huwa zinakatwa na watendaji wa serikali halafu hawasafiri kwahiyo nafasi ile inaenda tupu. Nimemwambia Mtendaji mkuu aniletee orodha ili tuwakate fedha hizo kwenye mishahara", -Rais Magufuli.
Share:

RAIS MAGUFULI AMMWAGIA NOTI ALIYETOROSHA NDEGE YA TANZANIA...AAGIZA ASAFIRI BURE SAFARI ZAKE ZOTE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemkabidhi kiasi cha shilingi milioni 10, Mtanzania ambaye alisababisha Shirika la Ndege la Tanzania kuwa na ndege ya kwanza ambaye anafahamika kwa jina la Mapunda.

Rais Magufuli ametoa zawadi hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa mapokezi ya ndege ya kwanza Afrika aina ya Air Bus A220-300 ambapo alimpongeza Mzee Mapunda kwa kuhatarisha maisha yake pindi alipokuwa angani akirejea Tanzania baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika ambao ndio walikuwa wamiliki wa ndege hizo.

Aidha katika mkutano huo Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Uchukuzi, Isaac Kamwelwe kuhakikisha Mapunda na mkewe wanasafiri bure kwenye ndege za ATCL katika safari zake zote.

"Kikubwa ninawaomba watanzania tuwe wazalendo, Mapunda asingekuwa mzalendo leo tusingekuwa na ndege, ninawaomba ATCL mumsafirishe bure mzee Mapunda kwa kazi kubwa aliyoifanya." amesema Rais Magufuli.

Ndege ya aina ya Air Bus A220-300 ni ndege ya kwanza kuwasili barani Afrika, hususani kwenye nchi ya Tanzania.
Share:

SIMBA YAVUNJA MWIKO WA MIAKA 15..YAIRARUA NKANA RED DEVILS BILA HURUMA


Wachezaji wa Simba na Nkana wakati wa mchezo.

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kufika hatua hiyo tangu walipofanya hivyo Simba mwaka 2003.

Simba imetinga hatua hiyo baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia kwenye mchezo wa marudiano uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaa.

Mabao ya Simba yamefungwa na Jonas Mkude akisawazisha bao la Bwalya kabla ya Meddie Kagere kufunga bao la pili sekunde chache kabla ya mchezo kwenda mapumziko.

Simba sasa inaingia hatua ya makundi ikiwa na kumbukumbu ya kupangwa Kundi A miaka 15 iliyopita. Kundi hilo lilikuwa na timu za Enyimba ya Nigeria, Ismailia ya Misri na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Kwa upande wa wachezaji wa Simba sasa Clatous Chama, amefikisha mabao 4 kwenye mechi 4 za hatua ya huku pia akiwa ametengeneza mabao takribani 4 kati ya 12 waliyofunga katika mechi 4.
Share:

KAA MBALI NA SIMBA WEWE,HUYO CHAMA SIO WA AFRIKA HII,WAIFUMUA BILA HURUMA NKANA.

 NA KAROLI VINSENT AMA kweli Simba ndio wa kimataifa ,ndivyo walichokionesha leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuichabanga  bila huruma timu ya Nkana kutoka Zambia kwa  Mabao 3-1    kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na kutinga hatua ya Makundi. Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha mwenye “Fomisheni” ya hatari Mbelgiji ,Patrick Aussems,ambapo Dakika 5 za mwanzo  walianza vizuri ila ndani ya dakika 15 walipoteana na kuruhusu bao la dakika ya 16 lililofungwa na Walter Bwalya baada ya kushambulia lango la Simba kwa muda mrefu. Katika Mchezo huo…

Source

Share:

WANACHUO KORTINI KWA KUPOST PICHA ZA NGONO ZA MWANACHUO WALIYEMLAWITI GESTI DAR



Na Francisca Emmanuel - Habarileo

MWANACHUO wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) na mpenzi wake, Samson Kisuguta (28), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kulawiti na kuchapisha picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Mwaisomo ambaye makazi yake ni kwenye Hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) huku Kisuguta akiishi mkazi wa Msasani na mfanyabiashara, walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Salim Ally. 

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Janeth Magohe alidai washitakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na mwaka huu maeneo ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Magohe alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa, washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe na mahali kusikofahamika mwaka jana, ndani ya jiji hilo, walikula njama kutenda kosa la kulawiti, kuchapisha picha za ngono na kulazimisha kupata fedha ili kutochapisha picha hizo.

 Alidai katika mashitaka ya pili kuwa, Desemba 10, mwaka jana maeneo ya nyumba ya kulala wageni ya Morgan maeneo ya Msasani wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Kisuguta alimlawiti kinyume cha maumbile mwanafunzi anaesoma katika moja ya vyuo hapa nchini.

Katika mashitaka ya tatu, inadaiwa Oktoba 7, mwaka huu ndani ya jiji hilo, Mwaisomo pamoja na Kisuguta walichapisha picha za ngono kupitia ukurasa wa WhatsApp kinyume cha sheria. 

Pia alidai Novemba 13, mwaka huu, ndani ya jiji hilo, washitakiwa hao walimlazimisha mlalamikaji huyo kutoa fedha taslimu Sh 250,000 ili wasichapishe picha hizo.

 Washitakiwa hao walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo waliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Ally alitaja masharti ya dhamana kuwa kila mshitakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoa serikali za mitaa watakaosaini bondi ya Sh 500,000 kila mmoja. 

Hata hivyo, washitakiwa hao walikosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa rumande hadi Januari 3, mwaka huu kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Inadaiwa kuwa Mwaisumo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mlalamikaji huyo wakati wakisoma sekondari ya juu na baada ya kuchaguliwa kujiunga na vyuo tofauti hawakuwa na mahusiano mazuri.

Inadaiwa baadaye mwanamke huyo (Mwaisumo) alimtafuta mlalamikaji na kutaka waonane ndipo walikutania kwenye nyumba ya kulala wageni, lakini baadaye wakati wakiwa huko, mwanamke huyo alitoka na kuingia tena na mwanamume mwingine ambaye ni Kisuguta.

 Hata hivyo, baada ya Kisuguta kuingia chumbani, alimlawiti kinyume cha maumbile mlalamikaji huku wakichukua video na baadaye walitumia picha hizo kulazimisha kupewa fedha na mlalamikaji ili wasizichapishe kwenye mitandao ya kijamii.


Share:

MANARA AWATISHIA NYAU NKANA RED DEVILS....ASEMA UJINGA NI WAKATI WA KWENDA TU


Afisa Habari wa Mabingwa watetezi nchini, Haji Manara, ameweka wazi kwamba ni lazima ushindi upatikane siku ya leo kwa klabu ya Simba dhidi ya Nkana FC ya Zambia kwenye mashindano ya Klabu bingwa Afrika.

Manara amesema hayo ikiwa yamebaki masaa machache ili timu hizo kuweza kukutana katika uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa marudiano.

"Ujinga wakati wa kwenda tu,wakati wa kurudi hata wajishike Ugoko lililoandikwa litakuwa tu Insha'Allah. Kufa au kupona", Manara.

Ujumbe huo wa Manara umekuja kufuatia wachezaji wa Nkana Red Devils kuingia uwanjani wakiwa wamejishika kichwani kila mmoja ishara ya kujikuna hivyo Manara amesema kwa hapa hata wakishika ugoko watawafunga tu.

Mchezo wa kwanza wa Simba na Nkana uliochezwa Kitwe, Zambia ulimalizika kwa wekundu wa msimbazi kukubali kupokea kipigo cha mabao 2-1.
Share:

MWIGULU NCHEMBA AACHANA NA YANGA...AJIUNGA SIMBA KUISHUGHULIKIA NKANA RED DEVILS

Share:

MAPYA YAIBUKA MSOMI KUJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI...MSIBA PIA HAUJULIKANI ULIPO


Musa Ally (25), aliyejirusha juzi kutoka ghorofa ya tatu katika jengo la Rocky City Mall jijini Mwanza na kufa papo hapo si mkazi wa Kiloleni kama ilivyoelezwa awali.

Akizungumza na Mwananchi jana, Diwani wa Ibungilo, Yusuf Msoke alisema wananchi wa sehemu hiyo wanafahamika na iwapo kama kijana huyo angekuwa mkazi wa Kiloleni kama walivyoeleza polisi, wangekuwa wanamfahamu.

Juzi, Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Advera Bulimba alisema kijana huyo alionekana akiwa amelewa kupita kiasi na tangu Desemba 16 alikamatwa na kuwekwa Kituo cha Polisi Kirumba, lakini kilevi kilipopungua aliachiwa.

Bulimba alisema baada ya polisi kumwachia alikwenda kunywa tena pombe na baadaye kujirusha kutoka ghorofa ya tatu ya jengo hilo ambapo alikutwa na pombe kali na ugoro

Katika ufafanuzi wake, Msoke alisema ana shaka juu ya majina yaliyotumika kumtambulisha marehemu, akisema iweje msiba usijulikane hata ulipo.

“Huyu kwa kweli siyo wa hapa. Watu wangu wote wana utaratibu wa kutambuana katika daftari maalumu la wananzengo (wakazi). Kama ni wa hapa itafahamika tu hata kama siyo leo,” alisema Msoke.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiloleli ‘A’ inakodaiwa ndiko alikokuwa akiishi Musa, Edgeni Lutahiwa alisema hajawahi kusikia jina la marehemu. “Mimi niliona tu mitandaoni kuna mtu kajirusha kutoka ghorofani na baadaye ikaelezwa kuwa ni mkazi wa hapa, pengine ndugu zake wanaogopa kujitokeza,” alisema.

Justine Madereke, mkazi wa mtaa huo alisema hakumtambua marehemu.

Alisema, “Huwa (marehemu) anazunguka hapa sokoni muda wa mchana na anakuwa ni mlevi tu. Sasa kwa kuwa sisi hatumfahamu hatukuwa na nia wala haja ya kumdadisi.”

Katika maelezo yake, Bulimba alisema wakati polisi wakimhoji kabla ya kumwachia Musa alidai ni mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu Dar es Salaam, na alilalamika kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kukosa kazi.

“Marehemu alidai kuwa ni msomi, hana kazi na pia ni yatima. Wakati Jeshi la Polisi wakichukua maiti hiyo ilikuwa na kijikaratasi kimeandikwa kwamba asilaumiwe mtu,” alisema Bulimba.

Na Jonathan Musa, Mwananchi
Share:

HUYU NDIYE ANAYEONGOZA DURU YA PILI YA UCHAGUZI WA URAIS NCHINI MADAGASCAR

Antananarivo, MADAGASCAR. Rais wa zamani wa Madagascar, Andry Rajoelina, anaelekea kurejea madarakani, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya duru ya pili ya Uchaguzi wa urais yanayoendelea kutangazwa. Tayari kura Milioni 3.5 kati ya Milioni 5 zimehesabiwa na Rajoelina anaongoza kwa asilimia 55.7 dhidi ya mpinzani wake Marc Ravalomanana, ambaye ana asilimia 44.2. “Tunasubiri matokeo rasmi lakini naamini kuwa, kwa namna mambo yanavyokwenda, ushindi ni wetu,” amesema Hajo Andrianainarivelo, msaidizi wa Rajoelina, ambapo matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo. Hata hivyo, Fanirisoa Erinaivo, aliyewania urais katika duru ya kwanza,…

Source

Share:

WAMESHALOWA MAPENA NKANA,SIMBA YATANGAZA BUNDUKI ZAKE HIZI HATARI ZA KUWAMALIZA.

Na Karoli vinsent NI Maangamizi tu leo  kwenye uwanja wa Taifa ndivyo naweza kusema , wakati timu ya Simba inapokutana na timu ya Nkana kutoka nchini Zambia kwenye michuano  ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika  , Ambapo sasa Mabingwa hao  wa ligi Kuu timu ya Simba wametangaza kikosi cha hatari ambacho ukikitazama unaweza kuhoji Nkama wanapita wapi kwa mafano?. Katika Kikochi hicho kulichotangazwa na Kocha wa Simba mwenye Fomesheni za hatari,Mbelgiji Patrick Aussems ,ambacho ni 1.Aishi Manila. 2.Nicolas Gyani 3.Mohamed Hussein 4.Erasto Nyoni. 5.Pascal Wawa. 6.James Kotei 7.Jonas Mkude. 8.Clatous…

Source

Share:

TIMU HIZI LA LIGI KUU ZAVYEKELEWA MBALI KWENYE MICHUANO YA FA

Moto wa kombe la Shirikisho umeendelea kushika kasi katika viwanja mbalimbali huku timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara zikieendelea kupukutishwa kwenye michuano hiyo mapaka sasa timu 5 zimetolewa kwenye mashindano hayo. Zilizoondolewa mapema ni Mwadui FC ilitolewa na Pan Africa kwa mabao 3-1, Ndanda SC ilitolewa na Tras Camp kwa penati 3-2 baada ya kutoka suluhu dakika 90, Mbao FC ilitolewa na Dar City kwa penati 4-2 baada ya kufungana 1-1. Tanzania Prisons walitolewa na KMC kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kutoka sare ya kutofungana na Ruvu Shooting walitolewa…

Source

Share:

WIKILEAKS:BALOZI ZA MAREKANI, ZINAFANYA KAZI ZA KIJASUSI

London, UK. Mtandao wa WikiLeaks umefichua kuwa, balozi za Marekani na vituo vingine vyake vya kidiplomasia kote duniani vimenunua kiwango kikubwa cha vifaa vya kijasusi, hali ambayo baadhi ya nchi zimekuwa na hofu na Marekani. Nchi nyingizi ambazo balozi na ofisi mbalimbali za kidiplomasia zimekuwa zikielezea hofu zao dhidi ya Marekani, kwamba badala ya taifa hilo kujihusisha na masuala ya udiplomasia pamoja na uhusiano mwema, inahusika zaidi na masuala ya ujasusi, mapinduzi ya serikali halali na njama zinginezo haribifu kote duniani. Wikileaks imefichua kuwa, kuna maombi zaidi ya 16,000 kutoka…

Source

Share:

MWAKA WA TSUNAMI INDONESIA, WENGINE WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA JANGA HILI

Jakarta, INDONESIA. Makumi ya watu wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na janga la Tsunami lililosababishwa na mlipuko wa volcano nchini Indonesia. Idara ya Jiolojia nchini humo imesema Tsunami hiyo imesababishwa na mawimbi ya chini ya bahari, ambayo yamelikumba Lango Bahari la Sunda, linalounganisha Bahari Hindi na Java, umbali wa kilomita 200 kusini magharibi mwa mji mkuu, Jakarta. Idara ya Kukabiliana na Majanga imesema watu 62 wameaga dunia huku 600 wakijeruhiwa, mbali na makumi ya wengine wakitoweka kutokana na janga hilo la kimaumbile na kwamba maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni…

Source

Share:

DKT.BASHIRU “MKUU WA MKOA ATAKAYESHINDWA KUSIMAMIA HAKI ZA BODABODA NA MACHINGA HANA KAZI”

Na Allawi Kaboyo-Bukoba. Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi  CCM Daktari Bashiru Ally Kakurwa, amewataka watendaji wa Serikali hususani wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini,  kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa haki wakati wa kuwatumikia Wananchi wao pasipo kulegalega. Kauli hiyo ameitoa desemba 22 mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchama wa chama hicho waliojitokeza kumlaki alipowasili mkoani Kagera na kumtolea mfano Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kwa Nidhamu, Uzalendo, Ujasiri na Uchapakazi wake uliotukuka aliouonyesha kwa Kipindi Kifupi toka Ameteuliwa. “Niwaombe wananchi wa mkoa wa…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger