Monday, 13 June 2016

New AUDIO | YAMOTO BAND Ft. RUBY - SU.. | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD
https://mkito.com/song/11978?referrer=b9c7f677fae97ab3e1ffe848121a99aad16ee2ce
Share:

Magazeti ya Leo Jumatatu 13 June 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

MPYA:SERIKALI KUTANGAZA AJIRA ZA WALIMU 2015/2016 JULAI MWAKA HUU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY\
 
Serikali inatarajia kutangaza nafasi mpya za ajira za walimu mara baada ya bajeti kuu ya serikali kupitishwa na Bunge.
Katibu mkuu wa wizara ya Tamisemi Mhandisi Musa Iyombe aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzushi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali imesitisha ajira za walimu wa masomo ya sanaa na biashara.
Alisema taarifa hizo si za kweli na kwamba kinachosubiriwa ili kutangazwa kwa ajira hizo ni Bajeti kuu kupitishwa na Bunge. Bajeti kuu ya serikali itapitishwa na kuanza kutumika rasmi Julai 1. 
"Tumesikitishwa na taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kuwa tamisemi imesitisha ajira za walimu. Tamisemi inapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hiyo ni batili na inalenga kuchonganisha wananchi na serikali yao ya awamu hii" Alisema.
Alisema pia taarifa hiyo imelenga kuwapa hofu na chuki walimu waliohitimu masomo ya sanaa na biashara.
Iyombe alisema utaratibu utakaotumika kutangaza nafasi za ajira kwa walimu haujabadirika na kwamba utatumika uliozoeeleka miaka yote.
Sambamba na hilo, alitaka wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika kusambaza taarifa hizo za uongo.
"Tamisemi inaitaka Mamlaka yenye dhamana ya kusimamia mitandao ya kijamii ichunguze na kubain aliyesambaza taarifa hizi za uongo na achukuliwe hatua stahiki" alisema
Kwa upande wake katibu mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Profesa faustini Kamuzora, alisema kuna sheria ya mtandao ambayo itatumika ili kuhakikisha watu hao wanakamatwa na kuchukuliwa hatua.
Taarifa hiyo iliyokuwa imesambazwa mitandaoni ilieleza kuwa serikali inatarajia kuajiri masomo ya Hisabati na Sayansi pekee na kwamba walimu wa masomo ya Sanaa na Biashara hawataajiriwa.
Share:

Pemba Walalamikia Kupigwa Mabomu ya Machozi Zaidi ya 100.........Ni katika vijiji Ambavyo watu Wasiofahamika waliharibu na kufyeka mazao

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Wakazi wa Pemba wamelalamikia Jeshi la Polisi kuvamia maeneo yao na kupiga mabomu ya machozi na kufanya doria usiku wa kuamikia juzi katika mitaa na vijiji mbalimbali kisiwani humo na kuzua hofu miongoni mwao.

Maeneo yaliyokabiliwa na hali hiyo ni pamoja na Mahuduthi, Kengeja, Mgagadu na Kiwani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ambako polisi wanadaiwa kupiga mabomu ya machozi zaidi ya 100 na kutumia risasi za mpira kuwatawanya watu.

“Ilikuwa saa 1.30 usiku (wa kuamkia Jumamosi), gari za polisi zilifika kiamboni (kijijini) kwetu zikipiga misere kwa kasi, sote tukawa na hofu, watu walikimbia na kwenda kujificha, wengine waliumia na baadaye wakapiga mabomu mfululizo, sijui waliondoka saa ngapi maana tulijifungia ndani,” alisimulia Zuberi Said (34), mkazi wa Kiwani.

Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo walidai huenda hatua hiyo ya polisi ilitokana na matukio ya kuhujumu mali za viongozi wa Shehia yanayoendelea.

Inadaiwa kuwa watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Ijumaa waliteketeza miti na mashamba yanayomilikiwa na Sabiha Mohamed Ali na Abdalla Makame Hamad, ambao ni mashekha wa Shehia za Kendwa na Kiwani wilayani humo.

Ilidaiwa watu hao pia waliteketeza migomba na mikarafuu mali ya viongozi hao na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdallah aliyefika kujionea uharibifu huo alisema: “Sijui sababu ni nini, ila huenda ni kutokana na siasa chafu zinazoendelea hapa.”

Alilitaka Jeshi la Polisi na askari alioongozana nao katika ziara hiyo kufanya uchunguzi haraka ili kuwabaini na kuwakamata watu waliohusika na vitendo hivyo. “Wala msisubiri baada ya miezi 20 ndipo mkaanza kuchukua hatua,” alisema.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkoani Pemba, Mohamed Salim aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya Abdalla, alikiri kuwapo kwa hujuma na kuwatuma askari katika vijiji hivyo kufanya doria.
Share:

Freeman Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Wakamatwa.....Alipo Zitto Kabwe Bado ni Utata

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wakati Polisi ikimshikilia kwa saa mbili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mkoani Mwanza, jeshi hilo limefuta kongamano la kujadili Bajeti ya Serikali lililoandaliwa na ACT Wazalendo jijini Dar es Salaam huku kiongozi wake, Zitto Kabwe akisakwa.

Jeshi hilo lilizuia mkutano wa hadhara wa Chadema uliokuwa ufanyike wiki iliyopita mjini Kahama ambako lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wafuasi wa chama hicho, katika kile kilichoelezwa kulikuwa na dalili za uvunjifu wa amani.

Jeshi hilo pia lilizuia msafara wa viongozi wa chama hicho kuingia katika ofisi zake za Shinyanga walipokuwa wakielekea Mwanza.

Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ilieleza kuwa mbali na Mbowe, jeshi hilo pia lilikuwa linawashikilia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita.

Wengine ni Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka na viongozi wengine na wanachama wa chama hicho waliokuwa wanashikiliwa katika kituo cha Polisi Nyakato, jijini Mwanza.

Makene alisema tangu asubuhi ya jana, Mbowe na viongozi wenzake walikuwa wakizunguka katika maeneo kadhaa ya jijini Mwanza kuwasalimia wananchi katika ‘vijiwe’ mbalimbali kabla hawajakamatwa.

Alisema, “Hadi sasa (saa 11 jioni) hakuna maelezo ya kushikiliwa kwao.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kubainisha kuwa waliachiwa bila kufunguliwa kesi yoyote.

“Walikutwa Igoma Sokoni wakizungumza na wananchi. Mikutano ya namna hii imezuiwa. Wamefungua kesi mahakamani, hivyo hakuna haja ya kufanya tofauti mpaka itakapohukumiwa,” alisema Msangi.

Alifafanua kuwa jeshi hilo halina uhasama wowote na Chadema au chama kingine chochote na "hatuwezi kukiingilia kinapofanya mikutano yake ya ndani au hotelini. Kilichozuiwa ni mikutano ya hadhara.”

Wakati Msangi akisema hayo, kongamano la ACT Wazalendo ambalo lilitakiwa lifanyike jana kuanzia saa 7:00 mchana kwenye Ukumbi wa Jengo la LAPF; Millennium Towers, Kijitonyama lilizuiwa na polisi.

Tangu mapema asubuhi, askari polisi walitanda katika eneo la ukumbi huo kuzuia kongomano hilo.

Ukumbini hapo, waandaaji walisema hakuna anayeruhusiwa kuingia kwani wamepewa maelezo ya kuufunga baada ya tukio lililoandaliwa kuahirishwa.

Zaidi ya viti 210 vilikuwa vimepangwa kwa ajili ya kongamano hilo na mmoja wa viongozi wa ukumbi huo alionekana akiondoa mabango yaliyokuwa yanautambulisha mkutano huo wa ACT.

Viongozi watatu wa ukumbi huo walikataa kueleza kinagaubaga juu ya sakata hilo, lakini taarifa za jumla zilisema mkutano umezuiwa.

Mmoja wa watumishi wa ukumbi huo, alisema: “Tuliandaa kila kitu, ila shughuli imeahirishwa. Ukumbi unatakiwa kufungwa. Hautatumika kwa leo.”

Ilipofika saa 5:00 asubuhi, Msemaji wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis alisema chama kinafanya mkutano wa dharura kwenye ofisi zake za makao makuu na baadaye kingezungumza na waandishi wa habari.

Saa 8:00 mchana, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mghwira akiwa na viongozi wenzake, isipokuwa Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe alikuwa mbele ya kamera za wanahabari akifafanua kilichotokea kwa wanachama, wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla.

Alisema ilipotimu saa 4:00 asubuhi walipewa taarifa na mwenye ukumbi kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemjulisha kuwa chama hicho hakina kibali cha kuendesha kongamano hilo na kwamba kisiruhusiwe kufanya hivyo.

“Huku ni kufifisha demokrasia. Wapigania haki za kiraia wasimame imara na vyama vya upinzani katika kuilinda,” alisema Mghwira.

Wakati kongamano hilo likizuiwa, kuna taarifa za kukanganya juu ya alipo Zitto baada ya kudaiwa alikuwa anasakwa na polisi tangu juzi.

Taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya kiongozi huyo kuitwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na kuhojiwa juu ya kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara zinazokosoa utendaji wa Serikali na kupinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.

Baadaye jioni, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa alitoa taarifa kuwa Zitto ametoweka na hajulikani alipo. Hiyo ilikuwa ni baada ya askari kanzu kumtafuta kwa muda kwa saa kadhaa.

“Zitto amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu. Askari wanalinda nyumbani kwake tangu jana (juzi) usiku. Hivi sasa ametoweka, hatujui alipo. Lolote litakalompata, Jeshi la Polisi litajibu,” alisema Mtemelwa.

Awali, Mghwira alipoulizwa imekuwaje kuhusu Zitto alijibu kuwa mkutano ulikuwa wa dharura ndiyo maana viongozi wote hawakuwapo.
Share:

Utendaji wa Mkuu wa Wilaya Wakwaza Madiwani Morogoro

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamesa hawajaridhishwa na utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, John Henjewele kushughulikia migogoro ya ardhi inayoendelea wilayani humo.

Waliyasema hayo katika mkutano na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi wilayani humo.

Diwani wa Mbigiri, Juma Rajab alisema amejaribu  kufika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya kuhoji uhalali wa mashamba kuendelea kushikiliwa na wawekezaji hewa ambao hawayaendelezi, lakini hapati ushirikiano.

Diwani wa Kata ya Makole, Anfas Kaunda alimueleza Lukuvi kuwa kuna shamba namba 35 lililopo Kijiji cha Mambeya ambalo lilifutiwa hati na kurejeshwa serikalini tangu 1984, lakini hadi leo halijakabidhiwa kwa kijiji.

Akizungumza  baada ya mkutano, Henjewele alisema diwani huyo ana mgogoro na wananchi wake ambao amewakodisha mashamba ya Serikali kwa gharama kubwa.
Share:

Ruby na Aslay wa Yamoto Band ni couple mpya mjini

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Harmonize na Jacqueline Wolper tupisheni kidogo, sasa ni zamu ya Ruby na Aslay wa Yamoto Band.
image
Imekuja kama surprise kwa wengi na kama wasemavyo waswahili ‘penzi ni kikohozi kulificha huliwezi’ ndege hao wawili mahabuba wamejimwayamwaya hadharani kuoneshana jinsi wanavyopendana na mashallah, wamedhamiria kweli!
Ni wikiendi iliyomalizika ndipo uwepo wa couple hiyo ulifahamika lakini tofauti na nyingi ambazo huanza kwa tetesi, wawili hao hawakutaka kungoja bali wao wenyewe kuufunulia ulimwengu hisia za mioyo yao.
Haweshi kupostiana na kumwagiana jumbe tamu tamu!
Tazama post zao hapo chini.
image
image
image
image
image
image
Share:

The Wait is Over: Hii ni ratiba ya kutoka kwa Collabo za Diamond na P-Square na Papa Wemba mwezi huu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mashabiki wa Diamond na wapenzi wa muziki wa Bongo Flava kwa ujumla sasa wanaweza kukaa mkao wa kula kwasababu collabo za staa huyo walizokuwa wakizingoja kwa hamu hatimaye zitaachiwa hivi karibuni.
image
DIAMOND F/ P-SQUARE
Huu ni wimbo wa Diamond aliowashirikisha mapacha maarufu zaidi Afrika, Peter na Paul Okoye wa kundi la P-Square. Video ya wimbo huo ilifanyika April 24 nchini Afrika Kusini. Na sasa hitmaker huyo kupitia post yake ya Instagram amewaeleza mashabiki wake kuwa collabo hiyo inatoka ‘soon.’
image
Wimbo huo unatoka ikiwa ni takriban mwaka mmoja sasa kundi la P-Square halijaachia wimbo wake mpya. Wimbo rasmi wa mwisho wa kundi hilo la nchini Nigeria kutoka ulikuwa ni Collabo waliomshirikisha Don Jazzy. Miezi ya hivi karibuni wawili hao waliingia kwenye mgogoro wa kifamilia uliopelekea kuondolewa kwa kaka yao Jude kama meneja wao wa muda mrefu.
Mgogoro wa wawili hao ulipelekea kuwepo kwa kila dalili za kundi hilo kuwa limevunjika huku kila mmoja akianza kuwekeza nguvu zake kwenye miradi binafsi. Kwahiyo Diamond ana collabo kubwa mkononi mwake itakayoitikisa Afrika nzima huku kiu ya sauti za Peter na Paul wakiwa pamoja tena zikiifanya kuwa ‘collabo ya dhahabu.’
Kingine kwa watu waliobahatika kuiona video ya ngoma hiyo wanasema ni video kali itakayomweka Diamond level nyingine.
Na huenda staa huyo ameitengenezea timing nzuri zaidi ya kuiachia itakayoangukia kwenye msimu wa tuzo za BET mwishoni mwa mwezi huu. Kwa kuachia collabo kubwa kama hiyo katika msimu huo, anajitengenezea sababu ya kuwa msanii anayestahili kuishinda tuzo ya Best International Artist: Africa mwaka huu.
PAPA WEMBA F/ DIAMOND
image
Wiki tatu kabla mauti hayajamkuta Papa Wemba kwa kuanguka jukwaani na kufariki wakati akitumbuiza mjini Abidjan, Ivory Coast, April 24, muimbaji huyo mkongwe aliingia studio kurekodi wimbo na Diamond. Tarehe ambayo Papa Wemba alifariki, ndiyo ambayo Diamond alikuwa location kushoot video ya wimbo aliowashirikisha P-Square.
Kwahiyo ni bahati na heshima kubwa kwa staa huyo wa Tanzania kufanikiwa kushirikishwa na mwanamuziki huyo nguli aliyekuwa na sauti ya aina yake wiki chache kabla ya kifo chake.
Kupitia akaunti ya Instagram ya marehemu Papa Wemba ambayo bila shaka inaendelea kusimamiwa na watu wake wa karibu, imetangazwa kuwa wimbo huo utatoka June 24. Wimbo huo utakuwepo kwenye ile ambayo ingekuja kuwa album yake mpya, From Generation to Generation.
Kama zitatoka katika wiki zitakazofuatana, basi collabo hizi zitamfanya Diamond ateke vichwa vya habari vya Afrika na kumuongezea ukubwa wake unaoendelea kukua kila siku kwenye muziki wa Afrika.
Share:

Video: Master J asema zamani bei ya kurekodi wimbo ilikuwa tsh 1 milioni lakini sasa hivi ni tsh 30,000

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Master J amesema soko la watayarishaji wa muziki nchini limeshuka ambapo zamani amedai walikuwa wanarekodi wimbo mmoja kwa tsh 1 milioni tofauti na sasa ambapo amedai ngoma moja inarekodiwa kwa tsh 30,000. MasterJ
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Master J amesema hali hiyo imefanya maisha ya watayarishaji wengi wa muziki kuwa chini.
“Sisi tulianza kwa kulipwa tsh 5,000, 10,000 mpaka tukafikisha tsh milioni 1 kwa kila nyimbo lakini sasa hivi nasikia bei zimeshuka mpaka 60,000,” alisema Master J.
Aliongeza, “Kwam hiyo kwa maproducer game siyo zuri lakini kwa wasanii game zuri sana. Wakati sisi wakati ule tulianza kwa tsh 5000, 10000 mpaka sasa hivi ni tsh 30,000 maana tsh 60,000 


Share:

Sunday, 12 June 2016

MPYA: Serikali yawasaka waliopotosha ajira za walimu

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Prof Faustine Kamuzora - Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Makatibu wakuu wa wizara za Mawasilino, Elimu na TAMISEMI nchini Tanzania wamezitaka mamlaka husika ikiwemo ya jeshi la polisi kumbaini mtu aliyesambaza taarifa walizodai ni za upotoshaji zinazosema kuwa ajira za ualimu kwa mwaka 2015-2016 zimesitishwa.
Wakizungumza kwa pamoja leo jijini Dar es salaam makatibu hao wamesema taarifa hizo zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zina lenga kuleta chuki baina walimu hao na serikali, jambo ambalo ni lazima wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Faustini Kamuzora amesema wizara yake imeanza kulifanyia kazi suala hilo na itahakikisha aliyehusika kusambaza taarifa hizo za uongo anabainika na kuchukuliwa hatua.
Amesema sheria ya makosa ya mitandao ndiyo itatumika katika kumtafuta na kumkamata huku akisisitiza kwa watumiaji wa mitandao kuitumia teknolojia hiyo kwa malengo mazuri na sio vinginevyo.
Share:

BREAKING NEWS:Taarifa ya ACT- Wazalendo Kuhusu Kupotea Kwa Zitto Kabwe Tangu Jana Jioni

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA UMMA
Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku.
Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali gani. Askari kanzu wanalinda nyumbani kwake na kwa watu wake wa karibu. 
Sisi kama chama tunaliambia jeshi la Polisi kuwa lolote litakalotokea kwa Kiongozi wetu wao watajibu kwa umma.
 
Msafiri Mtemelwa,
Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo
Share:

Wabunge Waionya Serikali

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

WABUNGE wameonesha wasiwasi kuhusu kupunguzwa kwa fungu la fedha katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na kuonya kuwa huenda hatua hiyo ikampunguzia Rais John Magufuli kasi ya utumbuaji majipu, anayoifanya kwa wabadhirifu wa fedha za umma au kuua kabisa utaratibu huo.

Wabunge hao walionesha wasiwasi huo kwa nyakati tofauti bungeni mjini hapa Dodoma, wakati wakichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2O16/17 inayoanza kutekelezwa Julai mosi, mwaka huu.

Miongoni mwa wabunge hao ni wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), aliyeeleza kuwa, kupunguza fedha katika ofisi hiyo ni kumkwamisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya kazi yake kwa ufanisi na tija.

Kwa mujibu wake, kumkwamisha huko pia ni dalili ya kuukumbatia ufisadi kwa sababu ofisi hiyo ya CAG ndio inayofanya kazi ngumu na kubwa ya kuwafichua mafisadi nchini, hivyo inahitaji kujitosheleza kibajeti na kuepuka kuhitaji msaada kutoka kokote kwingine.

“Kitendo cha kuminya fungu la ofisi ya CAG kwa kupunguza kiasi cha fedha inachopewa kutoka shilingi bilioni 74 kwa mwaka wa fedha unaoisha hadi shilingi bilioni 44 kwa mwaka mpya wa fedha unaoanzia Julai Mosi, ni kuifanya ofisi hiyo ishindwe kuyabaini majipu (wabadhirifu, mafisadi),” Lugola alisema.
Share:

Wanafunzi 316 Waliofukuzwa Chuo Kikuu cha St. Joseph Wafungua Kesi Mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa kibali cha kufungua kesi ya uwakilishi, kwa wanafunzi wanne, waliofukuzwa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kwa madai ya kutokuwa na sifa za kudahiliwa kwenye vyuo vikuu.

Jaji Eliezer Feleshi alitoa kibali hicho baada ya wanafunzi hao kuwasilisha maombi ya kibali cha kuwakilisha wenzao mahakamani pamoja na kusitisha masomo wakati kesi ya msingi ikiendelea kusikilizwa.

Wanafunzi hao, walisimamishwa masomo baada ya kutolewa amri ya Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako kwamba kutokana na tatizo la ufundishaji wa Stashahada ya Elimu (Sayansi, Hisabati na Teknolojia) wanafunzi wote wanatakiwa kurejea nyumbani.

Akiwasilisha maombi ya wanafunzi hao, Wakili Emmanuel Muga aliomba wanafunzi 316 waliofukuzwa chuo, wapewe kibali cha kufungua kesi ya uwakilishi pia Mahakama itoe amri ya kusitisha masomo wakati wa usikilizwaji wa kesi.

Akitoa uamuzi, Jaji Feleshi alisema Mahakama imekubali ombi hilo, isipokuwa la kusimamishwa masomo wanafunzi wote na kufafanua kuwa “masomo yataendelea kusimama kwa wanafunzi 316 waliosimamishwa”.

Aidha alisema wanafunzi hao wanatakiwa kuwa na wawakilishi wanne tu, badala ya 316, kwa sababu idadi yao ni kubwa. Baada ya uamuzi huo, Wakili Muga aliwataja wanafunzi wanne watakaowawakilisha wenzao mahakamani hapo kuwa ni Innocent Peter, Ramadhan Kipenya, Oswald Mwinuka na Faith Kyando.

Jaji Feleshi alisema Mahakama imetoa kibali na itapanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi baada ya walalamikaji hao kufungua kesi yao. 
Katika madai yao, wanafunzi hao wanadai fidia ya miaka mitatu waliyokaa chuoni hapo dhidi ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) iliyowakilishwa na Wakili Rose Lwita na Judith Misokia na Chuo cha Mtakatifu Joseph, kikiwakilishwa na wakili Jeromah Msemwa.
Share:

CHADEMA, CCM Watofautiana Kuhusu Naibu Spika, Dk Tulia Ackson

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wakati Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Mbeya ikiutaka uongozi wa Bunge kuwachukulia hatua kali wabunge wa upinzani wanaosusia vikao vya Bunge, Chadema, Kanda ya Magharibi, imemtaka Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kujitafakari upya kama anafaa kuendelea na nafasi hiyo.

Kwa nyakati tofauti, viongozi wa CCM na Chadema walitoa kauli hizo ikiwa ni siku ya 12 tangu wabunge wa upinzani kususia vikao vinavyoendesha na Dk Tulia.

CCM walisema kitendo kinachofanywa na Chadema kinachochea siasa za kibaguzi badala ya kufanya kazi ya kutunga sheria ya kusimamia Serikali kwa maslahi ya wananchi.

Katibu wa Siasa Itikadi na uenezi Mkoa wa Mbeya, Bashuru Madodi aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa kitendo kinachofanywa ni kinyume cha maadili na mwongozo wa nchi na kumpongeza Dk Tulia kwa msimamo wake wa kuliongoza Bunge bila kujali ubabaishaji wa wabunge wa upinzani.

“Kitendo cha wabunge kutoka nje wakati wa vikao na kupiga soga ni utovu wa nidhamu na kutoheshimu kiti cha spika na hivyo wajiulize bungeni walikwenda kwa maslahi ya wananchi au la? ”alihoji.

Madodi alisema pia halmashauri kuu inalaani vikali matamko yanayotolewa ya wabunge wa upinzani ya kuzunguka nchi nzima kufanya siasa za kuwahadaa wananchi kuwa wameonewa bila kutambua kuwa wao ni chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kutozingatia na kufuata kanuni na taratibu za Bunge.

Kadhalika alisema ni vyema Bunge kufanya maamuzi ya kutowalipa posho wabunge watakaokuwa wakishindwa kuhudhuria vikao vyake.

“Uongozi wa Bunge usitetereke kwa vitendo vya ubabaishaji wa vyama vya upinzani na uendelee kuchukua hatua stahiki dhidi ya wabunge wanaoendelea na vitendo vya utovu wa nidhamu badala ya kuwasilisha kero za wananchi waliowachagua,” alisema.

Kaimu Katibu CCM Mkoa wa Mbeya, Lobe Zongo alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ya kurejesha nidhamu ya utendaji wa kazi serikalini hali itakayosaidia uchumi wa nchi kusonga mbele na kurejesha nidhamu.

 “Haya yote ni matunda ya Rais wa awamu ya tano kwa kweli anastahili pongezi kwa uwajibikaji na utendaji wa kazi kwa watendaji ndani ya chama na serikalini,” alisema.

Katibu wa Chadema Kanda ya Magharibi, General Kaduma alimlaumu Tulia akidai hana uchungu na wananchi kwa kuwa hakuchaguliwa kwa kupigiwa kura kama walivyokuwa manaibu waliomtangulia.

 Kaduma alidai Naibu spika huyo amevunja kanuni za Bunge na kuwadhalilisha wabunge wa upinzani kwa kushiriki kuondoa vipengele muhimu katika hotuba ya waziri kivuli wa mambo ya ndani, Godbles Lema.

Katibu huyo ambaye amechukua nafasi ya aliyekuwa Katibu wa Chadema Kanda hiyo, Christopher Nyamwanji, aliitaka Serikali kuingilia kati uamuzi uliotolewa na Kamati ya Maadili ya Bunge akidai hayakuwa sahihi.

“Mchango wa wabunge waliozuiliwa kuingia bungeni ni mkubwa katika Bunge hili la bajeti ila utakosekana kutokana na uamuzi uliochukuliwa na naibu spika ambao kimsingi unaminya demokrasia nchini,” alidai.

Pia, alikemea kitendo cha Jeshi la Polisi kuzuia mikutano na kutumia silaha za moto kutawanya umma akisema kinasababisha uvunjifu wa amani.

Amelitaka jeshi hilo kuacha kufanya kazi kwa maslahi ya CCM na badala yake wawe walinzi wa amani nchini kwa kufanya kazi bila upendeleo.

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Tabora, Francis Msuka alisema wajibu wa kufanya mikutano ya siasa nchini ni wa muda wote kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Alisema kumekuwa na matukio ya viongozi wa Chadema kunyanyaswa na Jeshi la Polisi huku viongozi wake ngazi ya vijiji wakifanyiwa mizengwe ili wasitimize majukumu yao kikamilifu.
Share:

Serikali Yatangaza Vita Dhidi ya Majambazi na Watu Wanaojihusisha na Mauaji

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni ametangaza vita dhidi ya majambazi na watu wanaojihusha na mauaji.

Alisema Serikali imelazimika kutangaza vita hivyo baada ya kutokea matukio 41 yaliyohusisha mauaji ya kinyama tangu Januari hadi mwezi uliopita.

“Serikali ipo kazini, sasa inatangaza vita dhidi ya watu wanaojihusisha na ujambazi, watakaobainika hakika wataangamizwa hatuwezi kukubali watu wazidi kupoteza maisha pasipo na sababu za msingi,” alisema Masauni.

Waziri huyo alitembelea Msikiti wa Rahman Mtaa wa Utemini Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana, Mwanza na kusema matukio hayo yanapaswa kutokomezwa na kukemewa kwa nguvu zote.

 “Mauaji hayo yalikuwa ya kutisha hivyo ilikuwa ni lazima watuhumiwa wakamatwe, hata hao waliokimbia wanapaswa kutiwa mbaroni,” alisema.

Pia, alionya tabia ya baadhi ya polisi kujihusha na vitendo vya uhalifu na kupoteza imani na uaminifu kwa wananchi.

 Aliwataka polisi wanaofanya vitendo hivyo kuacha na badala yake wapambane na wahalifu.

Masauni alisema nia ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa utulivu, hivyo haitakubali watu wachache kuvuruga amani iliyopo

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema vyombo vya usalama vipo imara kwani baadhi ya wahalifu wameuawa na wengine kukamatwa na wanaendelea kuhojiwa.

Mjumbe wa baraza la masheikh Wilaya ya Nyamagana, Saidi Darwesh alisema tukio la mauaji ya msikitini limesababisha hofu kwa waumini, hususan kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kwani wengine hawaendi msikitini kuswali.

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Utemini, Jukael Kiula alisema wakazi wa Kata ya Mkolani wamejitolea kujenga kituo cha polisi katika mtaa huo ili kudhibiti uhalifu unaotokea mara kwa mara. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika mauaji hayo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa pole askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na majambazi wakati wa mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika mapango ya utemini, jijini Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi ya Mabatini, jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Share:

Wapinzani Wataka Wabunge wa CCM Wasioongea Bungeni Nao Wanyimwe Posho

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwafutia posho wabunge wa CCM  wanaofika kwenye vikao vya Bunge hilo na kukaa kimya bila kuchangia jambo lolote hata kwa maandishi kwa maelezo kuwa hawafanyi kazi.

Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, ambaye ni Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), alitoa pendekezo hilo jana bungeni mjini hapa muda mfupi kabla ya kuwasilisha maoni ya Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusu hotuba ya Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali katika mwaka wa Fedha 2016/17.

Hotuba hiyo ya Bajeti iliwasilishwa bungeni Juni 8, mwaka huu na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango. Silinde alisema; 
“Kabla ya kutoa maoni ya Kambi ya Upinzani, ninaomba niweke sawa taarifa zinazopotoshwa na kiti cha Naibu Spika kuhusu posho na kueleza kuwa sisi ndio kila wakati tumetaka posho ziondolewe na kupelekwa kwenye shughuli za maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikisuasua kutekeleza jambo hilo.”

Kwa mujibu wa Silinde, suala kwao sio posho kwa sababu hata wakati wa Bunge la Katiba kila Mbunge wa upinzani aliacha Sh milioni 30. 
Akizungumzia wabunge wa CCM wakaa kimya, Silinde alisema wapo na wanapokea posho kama kawaida ilhali hakuna kazi yoyote wanayoifanya na kwamba umefika wakati sasa Bunge liongeze umakini zaidi kwa kuwadhibiti wabunge wa aina hiyo kwa kuwakata posho za vikao.

Alipendekeza kuwa Hansard (kitabu cha taarifa rasmi za Bunge) zitumike kuwabaini kwa sababu wapo na wanajulikana. 
Hata hivyo, kabla ya kueleza suala hili, Silinde alivunja utaratibu kwa kumtaja Naibu Spika kwa jina ‘Kiti cha Spika’ badala ya Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lililosababisha alazimishwe kutumia busara kuheshimu kiti hicho na hatimaye kutii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu), Jenister Mhagama, ndiye aliyesimama kuomba mtoa hoja (Silinde), aheshimu utaratibu wa Bunge hilo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger