Monday, 17 August 2026

DAWASA YATETA NA WANAWAKE BONYOKWA, ULINZI MIUNDOMBINU YA MAJI YATAJWA

...

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imewakumbusha Jamii juu ya umuhimu wa kulinda miundonbinu ya Maji ili kujenga jumuiya inayothamini huduma ya Maji kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

Hayo yamesemwa kwenye tukio la Bonyokwa Women Gala 2026, lililoandaliwa na Diwani wa Kata ya Bonyokwa Tumike Malilo, Bonyokwa wilayani Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, iliyobeba kauli mbiu “Mwanamke Imara, Jamii Imara, Maendeleo Endelevu.” lililenga kuwawezesha wanawake kupitia elimu mbalimbali ikiwemo biashara na fursa za kiuchumi, huku likisisitiza nafasi yao katika kujenga jamii yenye maendeleo endelevu.

‎Mgeni rasmi katika tukio hilo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, aliwahimiza wanawake kutumia elimu walizopata katika kuboresha shughuli zao za kiuchumi. Amesisitiza umuhimu wa nidhamu, ubunifu na matumizi sahihi ya fursa, akiwataka pia wanawake kutumia fursa zinazoweza kujitokeza wakati wa mashindano ya AFCON kwa kugeuza mahitaji yanayoongezeka kuwa fursa za kiuchumi.

‎Kwa upande wa DAWASA, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Everlasting Lyaro, amewaomba wanawake wa Bonyokwa kuwa mabalozi wa huduma za maji kwa kutoa taarifa mapema kuhusu changamoto mbalimbali za kihuduma ikiwemi mivujo na changamoto nyingine zinazojitokeza katika maeneo yao.

‎Amesema taarifa zinazotolewa kwa wakati zinawezesha DAWASA kuchukua hatua haraka, huku akiwakumbusha wananchi kutumia kituo cha huduma kwa wateja 181, kinachopatikana bure saa 24.

‎Lyaro amesema DAWASA inaendelea kushirikiana na wanawake na jamii kwa ujumla katika kuboresha huduma za maji, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.

Ndugu Swaumu Kinindi ameishukuru DAWASA kwa kuwafikia wananchi na kuwapatia elimu, akisema amepata ufafanuzi kuhusu bili ya maji na sasa anaelewa vizuri huduma hiyo.‎

‎Tukio hilo limekuwa sehemu ya jitihada za kuimarisha uhusiano kati ya DAWASA na jamii, huku wanawake wakihimizwa kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya maji na kutoa taarifa za changamoto mapema. DAWASA imeeleza kuwa ushirikiano na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha huduma za maji zinaendelea kuboreshwa na kufikika kwa ufanisi zaidi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger