Wednesday 21 August 2024

WAKULIMA WA MWANI, WAFUGAJI WA MAJONGOO BAHARI NA WANENEPESHAJI KAA JIJI LA TANGA WAPEWA MBINU MPYA

...

Zaidi ya vikundi 21 vya wakulima wa mwani, wafugaji wa majongoo bahari na wanenepeshaji Kaa Jiji la Tanga wamepatiwa elimu ya kilimo na ufugaji bora wa mazao ya Bahari.

Akizungumza lengo la utoaji wa elimu hiyo mratibu kutoka chuo cha mipango ya maendeleo vijijini Dr. Bonamax Mbasa amesema utafiti uliofanywa na chuo cha mipango na UNDP ulibaini wakulima na wafugaji hawana uelewa wa kutosha wa kile wanacho kifanya ndiyo sababu zao hilo kushindwa kupanda thamani na kuleta tija kwa wanavikundi na jamii iliyopo.

"Tumeona tulete elimu hii ili iwape ujuzi utakao wasaidia wakulima na wafugaji wa mazao ya baharini kuondokana na ukulima wa mazoea"alisema Dr. Mbasa.

Aidha Dr. Mbasa amesema kwa sasa upo umuhimu mkubwa wa kuweka makaushuo pamoja na mashine ya kusaga unga wa mwani ili kusaidia kuongeza ubora kwa zao la mwani.

Naye mwakilishi kutoka UNDP Veronica  Sigala akaelezea mradi wa Bahari ni Maisha unavyofanya kazi na kuhakikisha wakulima na wafugaji wa mazao ya baharini wanapata faida kutokana na kazi zao.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger