Dkt. Faustine Ndugulile Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Kanda ya Afrika
Na Dotto Kwilasa.
Hatimaye mshindi kinyang'anyiro cha nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Kanda ya Afrika apatikana .
Mbunge wa Kigamboni Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile ndiye aliyeibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika leo Jumanne, tarehe 27 Agosti 2024 mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo na kuwashinda wagombea wengine watatu kutoka Senegal, Niger na Rwanda
Katika uchaguzi huo Dkt. Ndugulile amewashinda wagombea wengine watatu kutoka Senegal, Niger na Rwanda na hivyo kuitendea haki nafasi hiyo kwa kuwa Mara baada ya kuanza kazi rasmi, Tanzania kama nchi itapata nafasi pia ya kujitangaza kimataifa.
Ikumbukwe tu kuwa zoezi la uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika umefanyika kupitia Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afya Afrika chini ya Shirika la Afya Duniani.
Kabla ya kushinda uchaguzi huo Dkt. Ndugulile aliweka wazi vipaumbele vyake kuwa ni kuhakikisha Watu wanapata haki ya kupata huduma bora za afya; Kuboresha utayari wa nchi za Afrika katika kukabiliana na majanga ya magonjwa ya mlipuko, Kuimarisha uwajibikaji ndani ya WHO kanda ya Afrika pamoja kuimarisha mawasiliano baina ya nchi wanachama katika masuala ya Afya.
0 comments:
Post a Comment