Thursday 1 August 2024

HUDUMA ZA AFYA KUTOLEWA MAONESHO YA NANENANE DODOMA

...



Na Mwandishi wetu, Dodoma

Wizara ya Afya pamoja na ldara na Taasisi zake inashiriki Maonesho ya Wakulima Nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika Viwanja vya nanenane Nzunguni Dodoma.

Huduma mbalimbali za Afya zinatarajiwa kutolewa katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na Elimu ya Afya kuhusu Mtindo bora wa Maisha ,umuhimu wa mazoezi, lishe,vipimo vya uwiano uzito na urefu, afya ya akili, vipimo vya Virusi vya UKIMWI,uchunguzi wa awali Saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti,Dawati la Elimu ya Afya na Uhamasishaji jamii, Elimu ya Afya ya Mazingira,Elimu ya Afya kuhusu Tiba Asili na Elimu ya Afya kuhusu Malaria na magonjwa mengine mbalimbali.

Viongozi wa Wizara ya Afya akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Utawala Wizara ya Afya Bi.Fatma Kalovya,Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Simon Nzilibili, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Englibert Kayombo, Bi. Grace Msemwa , Mratibu wa Mabadiliko ya Tabia katika Jamii Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Evance Simkoko Afisa Afya Wizara ya Afya wamewasili katika banda la Wizara ya Afya kujionea Maandalizi yanavyoendelea.

Maonesho ya Nanenane kitaifa yamefunguliwa rasmi leo tarehe 1,Agosti, 2024 Jijini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa hadi Agosti 8,2024 ambapo Huduma mbalimbali za Afya zitatolewa bila malipo hadi tarehe 10, Agosti, 2024.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger