Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ukiongozwa na kauli mbiu 'Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora'.
Miongoni mwa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo ni Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mkoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliofanyika leo Ijumaa Agosti 9,2024 Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk amesema mkutano huo umelenga kupeana taarifa mbalimbali za maandalizi kwa ajili ya kuanza rasmi kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari.
“Lengo la kukutana na wadau hawa ni kupeana taarifa za uwepo wa zoezi hili na kuwapitisha katika vifaa na mifumo ya uandikishaji pamoja na kuona namna zoezi litakavyofanyika vituoni. Tume imekutana na wadau ili kupeana taarifa juu ya maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na maandalizi hayo pamoja na mambo mengine yanajumuisha uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura, uboreshaji wa majaribio, ununuzi wa vifaa na ushirikishwaji wa wadau”, amesema Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk.
Amefafanua kuwa, kwa kuzingatia Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, wapiga kura 5,586,433 wapya wanatarajiwa kuandikishwa sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/20 na kwamba wapiga kura 4,369,531 inatarajiwa wataboresha taarifa zao.
"Kwa Mkoa wa Shinyanga, Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 209,951 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ya wapiga kura 995,918 waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambapo Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869. Wapiga kura 594,494 inatarajiwa wataondolewa kwenye daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye daftari, hivyo baada ya uboreshaji, inatarajiwa kuwa Daftari litakuwa na jumla ya wapiga kura 34,746,638",amesema.
"Vituo 40,126 vya kuandikisha wapiga kura vitatumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2024 ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga kuna vituo 1,339 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 122 katika vituo 1,217 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20",ameongeza Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu).
Tume tayari imeanza zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo uzinduzi ulifanyika mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 na mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo Ijumaa Agosti 9,2024 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga kwa ajili Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga
0 comments:
Post a Comment