Monday 24 June 2024

MTATURU AISHAURI SERIKALI KUONDOA URASIMU KWENYE BIASHARA

...


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amechangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023 huku akiainisha maeneo manne ya msisitizo kwa serikali ili kuweza kuongeza mapato kupitia sekta ya biashara.

Akichangia Juni 24,2024, Bungeni Jijini Dodoma Mtaturu ametaja eneo la kwanza kuwa ni biashara na kuishauri serikali kuondoa urasimu uliopo ili kuweza kukuza biashara.

Amesema katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ya mwaka 2020/2025,Sekta ya biashara imetajwa kwa msisitizo mkubwa sana kupitia Ibara ya 49 ukurasa wa 60.

“Ibara hiyo imeeleza kuwa CCM inatambua kwamba biashara ni chanzo cha mapato na hivyo kitaendelea kuelekeza serikali kuimarisha biashara ya ndani nan je ya nchi,na imeahidi katika kipindi cha miaka mitano Chama kitahakikisha mchango wa sekta ya biashara kwenye pato la Taifa unaendelea kuimarika,

“Ninataka kukumbusha kwenye eneo hili kwamba sekta ya biashara ikisimamiwa vizuri inaweza kuongeza mapato ya nchi na fedha ambazo leo tuna changamoto kwenye miradi,tukiweza kuwekeza vizuri tutaweza kufanya miradi yetu vizuri,

Amesema katika biashara kuna urasimu mkubwa ambapo mtu akitaka kuwekeza kwenye biashara ni lazima aache kazi nyingine zote ili ashughulikie.

“Taasisi zetu zinazosimamia utoaji wa vibali zitazamwe upya ,ninaamini tukitazama kwenye eneo hilo itasaidia uwekezaji,leo Mh Rais wetu analeta wawekezaji nchini lakini ili mtu awezek uanzisah kampuni inamchukua mwezi mzima,sasa kwa hali hii unategemea wapi kodi itapatikana wakati mtu hajaanzisha biashara,

“Nikupe mfano mmoja leo mtu akitaka kujenga hoteli ya ghorofa hata ikianza ghorofa moja, mbili anaanza kupewa vikwazo kwamba kuna watu wazima moto nao wanataka fedha sasa tunakwenda wapi,

Suala la pili ni miundombinu ambayo ni uti wa mgongo wa biashara nchini na katika eneo hili ameomba serikali kujenga barabara ili kurahisisha sekta ya usafirishaji ikiwemo kusimamia ujenzi wa madaraja.

Amesema kunapokuwa na usafirishaji wa bei nafuu utasaidia kupunguza ushuru wa bidhaa mbalimbali na hivyo kuiomba serikali isimamie mpango wak ujenga barabara na kuongezewa nguvu ili kuhakikisha nchi inafunguka zaidi.

“Nitoe ombi kwenye eneo hili la barabara hatujafanya vizuri kwenye barabara ya za EPC+H,tulisainiwa mkataba toka mwaka jana mpaka tunavyoongea leo mwezi wa sita mwingine barabara hazijaanza ,barabara zenye urefu wa kilomita 2,035,kuna barabara ile ya kutoka Singida-Kwamtoro –Kiblash Tanga yenye kilomita 460 haijaanza kufanya kazi,wananchi wale tunawaambia nini,

Mtaturu ametaja eneo la tatu kuwa ni ardhi ambayo ndio msingi katika ujenzi wa Taifa lakini kuna migogoro mingi na hivyo kuomba bajeti hiyo ikajibu changamoto ambazo zipo kwa wakulima na wafugaji nchini.

“Leo hii watu wakitaka kutumia ardhi unaambiwa hii ardhi ni ya mtu fulani amechukua heka zaidi ya 1,000,heka zaidi ya 2,000 peke yake, watu wanaotaka kuwekeza katika nchi yetu wanakosa maeneo,hatujapima ardhi yetu tupime sasa na kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao ndio utaondoa migogoro katika nchi hii,”amesema.

Mtaturu ametaja eneo la nne kuwa ni kilimo ambacho ni uti wa mgongo na kinaajiri wananchi zaidi ya asilimia 65.

“Ibara ya 35 ya Ilani ya CCM ukurasa wa 33 unasema kilimo kitaendelea kuwa mhimili wa Taifa letu, niombe sana jitihada zinazofanyika tunaziona uwekezaji wa mbolea ya ruzuku ,tumeona kwenye mbegu na utaalam mbalimbali ,tuendelee kuongeza uwezo wa wale watumishi wa kilimo ambao wapo kwenye maeneo yetu wakiwemo maafisa ugani

Mbali na mambo hayo manne amegusia pia uzalishaji wa sukari eneo ambalo amesema ni lazima serikali iingilie kati na kuweza kusimamia.

“Hatuwezi kuacha soko huria kwa jambo ambalo ni muhimu kwa wananchi,kilicholetwa hapa tupitishe ili NFRA waweze kununua sukari kwa niaba ya serikali na watanzania,leo hatuwezi kuona watu wanazunguka wanaitumia siasa sukari hatuwezi kukubali,

“Serikali makini na kiongozi makini anaposikia changamoto ni lazima atafute njia ya kutatua ambayo mojawapo ni hii ambayo tunayo sasa hivi ya kuweza kumonopoly soko la sukari ili kuwafanya watanzania wawe salama,sukari leo ni kila kitu ndio maisha,”.amesema.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger