Tuesday 3 January 2023

MAMA ADAIWA KUWATEKA NA KUWAUA WATOTO WAKE BAFUNI MKESHA WA MWAKA MPYA

...

Mama wa watoto wawili waliouawa katika Kijiji cha Kerwa eneo la Kikuyu nchini Kenya usiku wa mkesha wa mwaka mpya, amekamatwa.

OCPD wa Kikuyu, Catherine Ringera alisema kuwa uchunguzi uliofanywa unamhusisha mama huyo na vifo vya watoto hao.

 "Kulingana na ile statement zimeandikwa na hata kulingana sisi vile tuliangalia, vidole zote zinaelekezwa kwa mama," alisema Ringera.

 Ringera alisema kuwa watatafuta maagizo ya korti kumzuia mama huyo zaidi ili kukamilisha uchunguzi wa mauaji hayo ya kutisha.

OCPD alisema walipata simu ya mwanamke huyo ambayo ilikuwa na skrini iliyovunjika na ujumbe ambao alimtaka mume wake amlipe madeni yake. 

Ringera aliongeza kuwa wamekusanya sampuli kutoka eneo la tukio ikiwa ni pamoja na vitabu vitakavyosaidia kuwakamata waliohusika katika mauaji hayo. 

Mwanamke huyo atafikishwa kortini leo, Jumanne, Januari 3 akisubiri uchunguzi zaidi wa polisi. 

Baba watoto anasemaje?

 Baba ya watoto hao Paul Gaitho, ambaye ni mchinjaji alisema alipata simu ya kutatanisha kwamba watoto wake wawili walikuwa wametekwa nyara na watu wasiojulikana. 

Alisema kwamba aliacha kazi yake akifuatana na marafiki zake na kukuta watoto wake tayari walikuwa wameuawa na kutupwa bafuni; mmoja akiwa amefungwa kamba ya kiatu, na mwingine ametupwa kwenye ndoo ya maji. 

"Niliambiwa watoto wamekuwa hijacked. Nilitoka na marafiki zangu tukaenda hadi kwa nyumba. Nilikuta kama watoto washauawa," alisema Gaitho.

Mama huyo anaripotiwa kuwa pekee yake na watoto ndani ya nyumba wakati shambulio hilo linalodaiwa kutokea. 

Alikimbia umbali wa kilomita mbili ambapo alimfahamisha jirani yake kwamba alishambuliwa na hakujua waliko watoto wake.

CHANZO - Tuko news
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger