Friday, 20 January 2023

NABII MKUU DKT GEORDAVIE AGAWA MILIONI 100 KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMUNGE

...
Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya Upako ambaye pia ni balozi wa amani Dkt. Geordavie Kasambale akiongea na wafanyabiashara kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 100

Na Woinde Shizza , ARUSHA


Nabii mkuu wa kanisa la Ngurumo ya upako ambaye pia ni balozi wa amani Dkt Geordavie Kasambale amekabidhi hundi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati na kuwasaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko la Samunge lililopo kata ya mjini kati mkoani Arusha.


Akikabidhi hundi hiyo leo jijini Arusha katika soko la Samunge ,Nabii Mkuu amesema kuwa amewiwa kufanya hivyo baada ya kupata barua aliyoandikiwa ya kuhitaji msaada kwa ajili ya kukarabati na kusaidia wajasiriamali wenye mitaji midogo katika soko hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Nabii Mkuu akimkabidhi hundi hiyo mbunge wa Jimbo la Arusha mjini pamoja na muwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini


Amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 80 watagawiwa mtaji wajasiriamali wenye mitaji midogo na huku kiasi kilichobaki cha milioni 20 kikitumika kwa ajili ya kukaratabati soko hilo.

“Mimi huu msaada ninatoa sitafuti waumini sipo hapa kumbadilisha mtu dini nipo hapa kuwasaidia wananchi katika kuondokana na matatizo mbalimbali na asanteni sana kwa mabango na picha haya ni mahaba makubwa sana na asanteni kwa heshima yenu ya kunipa kuwa mlezi wa soko ila mniwie radhi tutakuwa tunashirikiana popote mnapohitaji msaada ila swala la kuwa mlezi sitaweza maana nina majukumu mengi sana”, amesema Nabii.
Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo akiongea na wafanyabiashara wa soko la Samunge

Amesema kinachomsukuma kusaidia jamii ni Mungu kwani awali alipoitwa kutumikia Mungu alipewa maono ya kueneza injili ya kinabii na aliifanya lakini Kwa Sasa Mungu alimwambia afanye injili kwa matendo na ndio maana ameanza kueneza matendo kama Moja ya kauli mbiu yake inavyosema maneno machache kazi kubwa zaidi.


Aidha amewataka Viongozi wa dini kutochukua sadaka tu wakati umefika wa kuanza kurudisha kile wanachokipata kwa wananchi ,ni wakati sasa kurejesha fadhila kwa jamii wawasaidie maana watu wanateseka ,hivyo ni vyema wakajitoa na kujitahidi kuwasaidia wenye uhitaji.


“Msaada huu nilioutoa ni baada ya kupokea barua yenu ya kuomba msaada na nimekuja kuwaunga mkono na kila mmoja anapaswa kutambua kuwa tunaposaidia jamii tutakuwa tumemsaidia pia Rais Samia Suluhu Hassan katika suala la maendeleo ,unajua serikali inasaidia wananchi wake lakini haiwezi kuwafikia wote hivyo ni vyema watu kama sisi tujifunze kujitoa na kuwasaidia wenye uhitaji. “amesema.


Naye Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa,kazi ya viongozi wa serikali ni kuwaheshimu viongozi wote wa dini na kuwapa heshima yao pamoja na kuheshimu kipawa walichopatiwa ,aliongeza kuwa Mungu tunaemuabudu ni mmoja sema majina tu ndio yanatofautiana hivyo ni vyema kila mmoja akaheshimu imani ya mwenzake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger