Monday, 16 January 2023

WANAWAKE LAKI MOJA, MASHIRIKA YAGEUKA MBOGO MAUAJI YA WANAWAKE SHINYANGA...."NI UPUUZI MKUBWA KUSEMA NILISIKIA TU AKIPIGA KELELE"

...
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi, Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Mercy Shirima akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani.

Na Kadama Malunde & Elizabeth Cosmas - Malunde 1 blog

Taasisi ya Wanawake Laki Moja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Shinyanga yamelaani matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yanayoendelea mkoani Shinyanga na nchi kwa ujumla huku wakiitaka jamii kupaza sauti kupinga vitendo hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Januari 16,2023 katika Ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe amesema Taasisi hiyo inasikitika kuona vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea kutokea katika jamii.

“Tumekuwa tukipata taarifa na kuhusu matukio ya kikatili ikiwemo wanawake kuuawa kwa kupigwa na waume zao, matukio haya yanatokea kwenye maeneo yetu lakini jamii haitoi ushirikiano kuripoti matukio kwa wakati vitendo vya ukatili vikifanyika”,amesema Ndagiwe.

“Wananchi wamekuwa wakishuhudia matukio ya ukatili lakini wanakaa kimya, hawatoi taarifa. Ni upuuzi mkubwa kusema ‘Nilisikia akipiga kelele’ inasaidia nini sasa wakati mtu tayari ameshapoteza maisha, ungepaza sauti hayo mambo yasingetokea, wanawake wasingeuawa”,ameeleza Ndagiwe.

Mwenyekiti huyo wa Wanawake Laki Moja ameomba viongozi wa serikali za mitaa kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kuwa mstari wa mbele kutokomeza matukio ya ukatili kwani baadhi yao hawafanyi kazi ya ulinzi na usalama ipasavyo.

“Viongozi wa ngazi za juu hawana tatizo, tatizo ni viongozi wa huku chini ambao ni wenyeviti wa vitongoji, vijiji, mitaa baadhi yao wanalegalega katika suala la ulinzi na usalama wa wanawake na watoto, wengine wanadiriki kumaliza kesi kienyeji kwa kupeana pesa badala ya kupeleka kesi kwenye vyombo vya kisheria”,ameongeza Ndagiwe.

Amewashauri wanandoa kuvunja ukimya wanapofanyiwa au kuona dalili za kufanyiwa ukatili kwa kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali na Dawati la Jinsia na Watoto ili kukomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives amesema Mauaji ni ukiukwaji wa haki za binadamu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha wanawake na watoto wanalindwa.

“Wanandoa mkishafikia hatua ya kuambizana kuuana hiyo ni hatua mbaya sana. Ukitishiwa kuuawa usinyamaze kwani ipo siku atatimiza anachokisema. Pia tunaomba viongozi wa dini waendelee kupaza sauti kutoa elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia katika jamii”,amesema Mbugani.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na serikali katika kutokomeza vitendo vya kikatili huku akiwahamasisha wananchi kutoa ushahidi kwenye kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia badala ya kupeana pesa kumaliza kesi hizo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani akizungumza na Waandishi wa Habari leo Januari 16,2023.
Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani akizungumza na Waandishi wa Habari 
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi akizungumza na Waandishi wa Habari 
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Bi. Leah Daudi akizungumza na Waandishi wa Habari 
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Mercy Shirima akizungumza na Waandishi wa Habari 
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Mercy Shirima akizungumza na Waandishi wa Habari 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Laki Moja, Bi. Anascholastica Ndagiwe (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Bi. Paschalia Mbugani.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger