Monday, 23 January 2023

MKUDE AFANYA ZIARA MGODI WA MWADUI KUFAHAMU HATUA ZILIZOCHUKULIWA TANGU BWAWA LA MAJI TOPE LIBOMOKE...."FIDIA ILIPWE MAPEMA, UZALISHAJI UANZE"

...

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akiangalia maji tope akiwa juu ya tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude ametembelea Mgodi huo ili kufahamu hatua gani zimechukuliwa tangu Bwawa hilo la Maji Tope lilipobomoka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo kwa kufunikwa na tope Novemba 7,2022.


Mkude ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu amefanya ziara hiyo katika Mgodi wa Almasi wa Mwadui leo Jumatatu Januari 23,2023 akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati ya Usalama Mkoa wa Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Sabinus Chaula na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda.


Mkude amesema ziara hiyo imelenga kutaka kufahamu hatua gani zimefikiwa baada ya kupata janga la kubomoka kwa kingo za bwawa la Maji Tope katika Mgodi Almasi wa Mwadui tangu Novemba 7,2022 ikiwa ni miezi kadhaa sasa imepita.

“Leo nimefanya ziara ya kujiridhisha kwamba ni hatua gani zimefikiwa, Wenzetu wa Mgodi wa Williamson Diamond Limited wamechukua hatua mbalimbali kwanza za kuwanusuru wananchi waliokutwa na matope katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya mashamba.

Hatua ya pili waliyofanya ni kuwapatia huduma zote muhimu wananchi waliothirika na janga hilo ikiwemo za afya, elimu kwa watoto waliokuwa wanasoma na kwa watu waliokosa makazi sasa hivi wote wamehifadhiwa kwenye nyumba za kupanga ambapo wamepangishiwa na Mgodi wa Mwadui mpaka hali yao itakapokuwa sawa wengine wanaendelea kupata huduma ya chakula tangu Novemba 7,2022”,ameeleza Mkude.
Muonekano wa tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi.

Amebainisha kuwa hatua zaidi zilizochukuliwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu la kutafuta eneo mbadala la kuishi ambalo ni salama kuliko lile wananchi walikuwa wanaishi ambapo eneo limepatikana katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge lenye ukubwa wa Hekari 400.

“Tumefika kwenye eneo hili na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ametueleza ukubwa wa eneo kuwa ni la hekari 400 ambazo kwa kweli wananchi walioathirika na tope zitawatosha wao makazi na kilimo kwa sababu eneo lina rutuba, lilikuwa eneo la serikali na halina mgogoro wowote”,amesema Mkude.

“Natumia fursa hii kuushukuru Mgodi wa Williamson Diamond Limited kwa kutimiza yale yote ambayo walielekezwa na serikali kwa kuweka miundo mbinu ya kuhifadhi maji tope yasizagae tena na mengine, lakini pia namshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu kwa kutafuta eneo mbadala ambalo kwa kweli ni matumaini yangu hapa utaanza mji ambapo wananchi watapata huduma zote za msingi, shule zipo,kituo cha afya kipo, maji yapo, miundombinu ya barabara nitamsisitiza Mkurugenzi aiweke na umeme n.k”,ameongeza Mkude.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula akionesha eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu

Mkude ameusisitiza Mgodi wa Williamson Diamond Limited  suala la kulipa fidia kulipeleka haraka zaidi, akieleza kuwa amebaini kwamba bado hatua ya kufanya Tathmini haijakabidhiwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali hivyo kuelekeza ndani ya wiki mbili wawe wamefikisha taarifa hizo ili zirudi mapema waweze kulipa fidia kwa wananchi.

“Hivi karibuni Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa mkoani Shinyanga alitamka wazi kwamba tuchukue hatua ili kuhakikisha wananchi waliopatwa na janga hili la Maji tope wanalipwa mapema kadri inavyowezekana na ndiyo maana nimefanya ziara hata wiki moja haijapita, nimefanya ziara ili kujua hatua gani kwanza zimechukuliwa na nimegundua kuwa bado Mthamini Mkuu hajapata Nyaraka ili kuzisaini, Mgodi nimewapa wiki mbili hili ikamilike”,amesema Mkude.


Mwenyekiti huyo wa kamati ya uchunguzi wa kubomoka kwa bwawa la maji tope amefafanua kuwa suala la ujenzi wa nyumba watakaohitaji nyumba litatumia utaratibu utakaofaa, hivyo ameusisitiza Mgodi kufanya haraka na kutia umuhimu kwa maisha ya watu waliopatwa na janga hilo.

“Pia tumezungumza kwa undani sana kuhusu maendeleo ya Mgodi, siyo tunaangalia tu upande wa fidia na ubinadamu ni pamoja na kuendelea kufanya kazi kama kawaida. Mgodi kwa kweli ulisimama shughuli zake, tumesisitiza pia kuna maeneo ya mbadala au ujenzi wa bwawa jipya uendelee kwa kasi zaidi, hilo tumelifanya na tumekubaliana na wamesema kati ya miezi mitatu hadi mitano watakuwa wamekamilisha ujenzi wa bwawa na shughuli za uzalishaji zitaanza”,ameongeza Mkude.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda  akielezea hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka.


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda amesema tangu bwawa la maji tope lilipobomoka kingo Novemba 7 mwaka 2022, licha ya kuendelea na taratibu za tathmini ili wananchi walipwe fidia pia wameendelea kutoa huduma zote za kibinadamu kwa waathirika wa tope hilo kwa kuwapatia chakula, malazi na huduma zingine za elimu na afya na kwamba nyumba watakazowajengea wananchi zitakuwa bora.

“Jumla ya kaya 171 zitalipwa fidia, kati ya hizo kaya 46 tutazijengea makazi na tunaendelea kuzipatia huduma ya chakula kaya 50 zenye watu 286 mpaka pale watakapopata fidia na kupata makazi”,amesema Mwenda.
Mchoro unaoonesha hatua zilizochukuliwa na Mgodi wa Mwadui baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka

Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo amesema wamejenga kuta na kuweka matuta ya kuzuia tope lisiendelee zaidi kwenda kwenye makazi ya watu pamoja na kutengeneza mifereji ya kuchepusha maji yaliyokuwa yanaingia kwenye bwawa la New Almasi walilokuwa wanalitumia wananchi kwa huduma za kijamii na wanaendelea na ujenzi wa bwawa jipya.

“Tumejenga tuta kwenye bwawa la maji tope lililobomoka lakini pia tumekarabati bwawa la New Almasi ambalo lilikuwa linatumiwa na wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali ambalo lilijaa tope kwa kuliwekea tuta”,ameongeza Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo Shagembe Mipawa.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula amesema halmashauri hiyo imetenga eneo la halmashauri lenye ukubwa wa hekari 400 kwa ajili ya wananchi walioathiriwa na maji tope huku akisisitiza kuwa eneo hilo ni salama na halina mgogoro wowote na huduma za kijamii zinapatikana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude  akizungumza leo Jumatatu Januari 23,2023 wakati akipokea taarifa ya hatua zilizochukuliwa tangu Bwawa hilo la MajiTope lilipobomoka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo kwa kufunikwa na tope Novemba 7,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude  akizungumza leo Jumatatu Januari 23,2023 katika mgodi wa Mwadui.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda  akielezea hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akifafanua kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akifafanua kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akifafanua kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo Shagembe Mipawa akielezea kuhusu hatua zilizochukuliwa na Mgodi huo baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Mchoro unaoonesha hatua zilizochukuliwa na Mgodi wa Mwadui baada ya Bwawa la Maji Tope kubomoka
Juu ya tuta lililojengwa kudhibiti maji tope yasisambae kwa wananchi
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akiangalia maji tope akiwa juu ya tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi
Muonekano wa tuta lililojengwa kuzuia maji tope katika bwawa la New Almasi yasisambae kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati akitembelea mgodi wa Mwadui, aliyevaa miwani ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui (Williamson Diamond Limited) Mhandisi Ayoub Mwenda
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akiangalia mtaro/mfereji unaochepusha maji yaliyokuwa yanaingia kwenye bwawa la New Almasi walilokuwa wanalitumia wananchi kwa huduma za kijamii 
Afisa Mahusiano Mgodi wa Williamson Diamond Limited Bernard Mihayo akionesha mfereji unaochepusha maji yaliyokuwa yanaingia kwenye bwawa la New Almasi walilokuwa wanalitumia wananchi kwa huduma za kijamii 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu, eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu, eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kuvunjika kingo za Bwawa la Maji Tope katika Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Sabinus Chaula akionesha eneo ambalo waathirika wa maji tope watajengewa nyumba/makazi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger