




**************************
Wananchi wa Makambako wameshauriwa kutumia huduma za mawasiliano kujiimarisha kiuchumi ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika Gulio la wiki lililofanyika katika eneo la Soko Kuu la Makambako Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John amesema mawasiliano yamerahisisha upatikanaji wa fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.
Mhandisi Asajile amesema katika Ulimwengu wa sasa taarifa nyingi za uboreshaji wa huduma, biashara, masoko na kilimo zinapatikana mtandaoni na kuwataka wananchi wa makambako kutumia fursa hizo.
Ametoa mfano wa taarifa za uboreshaji wa kilimo, upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimo na misitu pamoja kutangaza bidhaa katika masoko ya ndani na ya kimataifa kuwa zinaweza kupatikana mtandaoni na kuwasihi wananchi badala ya kutumia mitandao kufanya mambo yasiyo na faida wajielekeze katika maeneo hayo ya msingi
Huu ni muendelezo wa kampeni ya kuelimisha umma juu ya matumizi bora na salama ya huduma za mawasiliano ijulikanayo kama kwea kidijitali inayoendeshwa na TCRA nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment