Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akiendesha zoezi la uteketezaji wa mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku, uteketezaji huo umefanyika katika kiwanda cha Twiga Cement Jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Godwin Gondwe akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 14,2022 wakati wa zoezi la uteketezaji wa mifuko ya plastiki ambayo imekamatwa hivi karibuni. Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akisisitiza jambo huku akionesha baadhi ya mifuko ya plastiki ambayo leo Septemba 14,2022 wamefanikiwa kuiteketeza katika kiwanda cha Twiga Cement. Gari likishusha mzigo wa mifuko ya plastiki ambayo leo Septemba 14,2022 imeteketezwa katika kiwanda cha Twiga Cement Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka akikagua mifuko ya plastiki ambayo leo Septemba 14,2022 wameteketeza mifuko ya plastiki tani 44.4. Baadhi ya mifuko ya plastiki ikishushwa kwenye magari kwaajili ya kuteketezwa katika kiwanda cha Twiga Cement zoezi ambalo limefanyika leo Septemba 14,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeteketeza vifungashio tani 44.4 ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi, ambapo uteketezaji huo umefanyika katika kiwanda cha Saruji cha Twiga Cement Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika zoezi hilo ambalo limefanyika leo Septemba 14,2022 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Godwin Gondwe amesema katika tani 44.4 za mifuko ambayo imekamatwa na kuteketezwa, mifuko tani 41 zimekamatwa katika Wilaya ya Kinondoni.
Amesema wataendelea kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu kuhakikisha mifuko ya plastiki inaondoka katika mazingira ili kuokoa viumbe hai ambavyo vingeweza kuathirika na mifuko hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amesema uwepo wa vifungashio hivyo vinaathiri afya za binadamu na wanyama kwani kumekuwa na matumizi ambayo si sahihi hasa kufungashia chakula cha moto na kusababisha kumleta madhara ya kiafya kama saratani na magonjwa ya damu.
"Hivi vifungashio havitakiwi kuwa sokoni ndo maana tunachukua jukumu la kuteketeza ili kuwaonyesha wengine kwamba hivi vifungashio havipaswi kuwa kwenye mazingira kwasababu vikiingia kwenye mazingira vitaathiri ustawi wa jamii". Amesema Dkt.Gwamaka.
Aidha Dkt.Gwamaka amesema zoezi hilo linaendelea kwa mikoa mingine kukamata vifungashio hivyo, na amewataka wananchi kuacha mara moja kutumia mifuko ya plastiki ili kulinda afya zao na wanyama.
0 comments:
Post a Comment