**********************
Sindi Mzamo, Rais wa circle of global business women (CGBW), amesema Rais wa Tanzania Samia Suluhu ni Champion wa Utalii Afrika aungwe mkono. Aliyasema hayo jijini Johannesburg Afrika kusini wakati akihutubia Mkutano wa Wanawake katika Utalii Kusini mwa Afrika (WITSA).
Alisema Rais Samia ameonesha mfano kwa Wanawake. Pamoja na kuwa na kazi nyingi pamoja na changamoto za kurekodi maporini lakini alisimame kidete kuhakikisha hili swala linafanikiwa na linafanikiwa.
Naye Balozi wa Utalii Nchini Tanzania Nangasu Warema ambaye alitumia Wasaa huo kuwaonesha Filamu ya Royal Tour, amewataka Viongozi na Watanzania wote kwa ujumla wao, popote pale Wanapopata nafasi ya kuzungumza kwenye Mikutano ya kimataifa, Wasiache kuizungumzia Filamu ya Royal Tour kwa manufaa ya Nchi ili kuongeza Utalii Nchini.
Rais Samia Suluhu Hassan, alizindua filamu ya Tanzania, The Royal Tour katika jumba la makumbusbo la Guggenheim 89th Avenue jijini New York, nchini Marekani tarehe 18 Aprili 2022.
Dhumuni la Mkutano huu ilikuwa ni kupena fursa zilizopo katika Utalii wa Afrika pamoja na kuangalia njia bora ya kutatua changamoto zilizopo ili Wanawake washiriki ipaswavyo katika Utalii
Balozi wa Utalii Nchini Tanzania Nangasu Warema
0 comments:
Post a Comment