Mwili wa Marehemu Asantina Sebastian ambaye alifariki juzi kwenye hospitali ya Aghakan jijini Dar es salaam alikokuwa akipokea matibabu ukiingizwa kaburini wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Madale Mivumoni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Leo Septemba 17, 2022.
Waombolezaji mbalimbali Ndugu, Jamaa na marafiki wameshiriki Katika mazishi ya mwili wa marehemu Asantina Sebastian Katika nyumba yake ya milele, “Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe Amen”.
Familia ya Marehemu Asantina Sebastian ikiwa na huzuni kubwa Katika mazishi ya mpendwa wao aliyepumzishwa Leo.
Mwili wa Marehemu Asantina Sebastian ukiingizwa kwenye kaburi na waombolezaji.
Waombolezaji mbalimbali wakiwa katika mazishi hayo.
Wadau mbalimbali wa Madale wakishiriki Katika mazishi hayo katikati ni John Badi mmoja wa wanakundi la kijamii la Wadau Madale.
Ibada ya mazishi ikiendelea nyumbani.
Stephen Kazimoto Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Madale kwa Kawawa ambaye ni mmoja wa viongozi wa kundi la kijamii la Wadau Madale akitoa salam zake za rambirambi Katika msiba huo.
0 comments:
Post a Comment