Marubani mawili wa shirika la ndege la Air-France wamesimamishwa kazi baada ya kupigana katika chumba cha marubani ndege ikiwa hewani.
Wawili hao walilimana makonde wakipaisha ndege aina ya Airbus A320 kutoka Geneva, Uswizi kulekea Paris, Ufaransa, shirika la habari la Uswizi La Tribune limeripoti.
Wahudumu wa ndege waliokuwa wakipaa na ndege hiyo waliingilia baada ya kusikia kelele.
Mmoja wa wahudumu alibaki katika chumba cha marubani hadi pale ndege hiyo ilipotua salama.
Kwa mujibu wa La Tribune, shirika la Air-France limeambia kuwa kisa hicho hakikuathiri safari hiyo ya ndege.
Ndege ya Ethiopia 'yasahau' kutua baada ya marubani kulala fofofo
Mnamo Agosti 21, 2022, TUKO.co.ke iliripoti kuwa marubani wawili waliaminika kulala na kusahau kutua wakati wa safari ya kutoka Sudan kuelekea Ethiopia siku ya Jumatatu, Agosti 15,2022.
Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya safari za anga, Aviation Herald, tukio hilo lilitokea kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia Boeing 737-800 ambayo ilikuwa ikisafiri ikitokea jijini Khartoum kuelekea Addis Ababa.
Takwimu zilizothibitishwa na tovuti hiyo zinaonyesha kuwa ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kwa futi 37,000 ikijiendesha yenyewe na kushindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa Bole.
Udhibiti wa safari za anga haukuweza kuwafikia wafanyakazi wa ndege hiyo licha ya kujaribu mara kadhaa kuwasiliana nao.
Hata hivyo, kengele ilipigwa wakati ndege hiyo ilipokosa kutua kwenye barabara yake na kuendelea na safari. Ndege hiyo ilitua salama dakika 25 baadaye.
Wafanyakazi wa ndege hiyo wamesimamishwa kazi kwa muda huku uchunguzi zaidi ukifanywa.
Chanzo - Tuko News
0 comments:
Post a Comment