Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi
Amewataka wadau mbalimbali kuchangia timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu Tembo Warriors ili ifanikiwe kushinda mashindano Kombe la Dunia na imekuwa fahari ya Tanzania na kuwa mfano wa kuigwa na Nchi zingine kuwa Watu Wenye Ulemavu wanaweza kila kitu.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Katambi katika mkutano wa mwisho wa kuhimiza na kuagana kuelekea kambi itakayo wekwa Nchini Uturuki kwa maandalizi ya shindano la kidunia.
Aidha ameeleza kuwa serikali inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja na watu wenye Ulemavu na imetoa zaidi ya Milioni mia moja na hamsini kuhakikisha timu inachukua Kombe la Dunia.
Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu iko bega kwa bega nao, huku akitoa zaidi ya Shilingi Milioni mbili kwa Team kuwa chachu ya kuhimiza wadau mbalimbali kuisaidia timu hii ya watu Wenye Ulemavu kuimarika Kimataifa na kuleta heshima ya Taifa.
“Tunawaomba wadau mbalimbali taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali tuwasaidie wafike mbali maana ukiwasaidia Watu Wenye ulemavu ni umefanya dua, ni sala, ni Ibada na ni sadaka zaidi ya zaka”, alisema mhe.Katambi.
Katambi akaongeza kusema kuwa Mhe. Rais anawapenda sana watu wenye Ulemavu kafanya mengi ikiwemo kufufua vyuo zaidi ya 6 vya Watu wenye ulemavu kwa Tshs bilioni 3, Kuzalisha mafuta maalumu Nchini kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi, kutoa mikopo kwa mtu mmojammoja, kukutana nao Ikulu kuwasikiliza na kuitambua Jumuiya Band ya Watu wenye ulemavu pamoja na kuhakikisha kuwa anasimamia asilimia 3% ya ajira wapewe hawa watu wenye ulemavu, Ujenzi miundombinu rafiki, kupunguza kodi na Ugawaji Vifaa wezeshi, Sasa tunabadilisha Sera na Sheria kwa faida ya Makundi haya maalumu na muhimu.
"Nitahakikisha Watu wenye Ulemavu wanapewa haki zao ni lazima na sio hisani wala hidaya.Mungu atubariki sote!", alisema mhe.Katambi.
0 comments:
Post a Comment