Thursday 7 April 2022

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AHUDHURIA MAZISHI YA SPIKA WA BUNGE LA UGANDA

...

Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson akiaga mwili wa Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah katika Viwanja vya Kololo, Jijini Kampala nchini Uganda.

Marehemu Jacob alifariki dunia Machi 20, 2022 nchini Marekani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kufariki Spika huyo wa Bunge la Uganda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa na japo kifo chake kimeacha sintofahamu kutokana na taarifa kuwa alipewa sumu, taarifa ambayo imethibitishwa na baba yake Nathan Okori.

“Najua wote mliokuja hapa kwenye kuomboleza taarifa za kifo chake siyo nyepesi kuzipokea kwasababu najua hakufa kwa kifo cha kawaida aliwekewa sumu",alisema Okori
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger