Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akizungumza katika Misa ya Dominika ya Matawi katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo.
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akiwa katika ibada fupi ya kubariki matawi katika uwanja wa shule ya msingi Bugoyi(A)kushoto ni katibu wake Pd.Deusdedith Kisumo.
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akibariki matawi ya waamini kupitia ibada maalum iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Bugoyi (A)
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akibariki matawi ya waamini kupitia ibada maalum iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Bugoyi (A)
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akitoa baraka za mwisho kwa waamini mara baada ya Misa ya Dominika ya Matawi katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo.
************
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameendelea kukemea tabia ya baadhi ya watu kutumia shida na matatizo ya wengine kama fursa ya kujinufaisha badala ya kuwasaidia.
Akizungumza kupitia Misa ya Dominika ya Matawi ambayo imefanyika leo Jumapili April 10, 2022 katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga,askofu Sangu amewataka wanaofanya vitendo hivyo kuacha kuwaongezea maumivu watu walioko katika mahangaiko ya namna mbalimbali na badala yake waongozwe na moyo wa utu, huruma na upendo na kuwasaidia kadri ya mahitaji yao .
"Na kamwe tusitumie shida na mahangaiko ya wengine kwa lengo la kujinufaisha,mfano zipo NGO’S nyingi sana ndani ya nchi yetu lakini ukiangalia kwa undani kabisa si kwa ajili ya watu wenye mateso na wenye mahangaiko na badala yake kinachowafikia walengwa ni asilimia ndogo ya raslimali zinazotolewa na wahisani,kiasi kikubwa kinatumika kwa ajili ya watu kujinufaisha kupitia shida zao”,amesema.
Askofu Sangu pia ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza Wakristo wote kuepuka dhuluma na kutokuwa chimbuko la mateso kwa wengine na badala yake wahakikishe wanakuwa chimbuko la matumaini na faraja kwa watu wenye shida.
Leo,Kanisa Katoliki kote ulimwenguni linaadhimisha Dominika ya Matawi ambayo ni kumbukumbu ya kupokelewa kwa Shangwe kwa Yesu Kristo mjini Yelusalemu,tukio lililofanyika siku chache kabla ya kukamatwa kwake,kuteswa na kufa msalabani na baadaye kufufuka siku ya tatu.
0 comments:
Post a Comment