Waziri Mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk Jilly Maleko (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kushoto), Mjumbe wa Bodi Benki ya CRDB Burundi, Kahumbaya Bashige (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fred Siwale (wa kwanza kushoto), na Menard Bucumi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi.
Benki ya CRDB inaonekana kuwa daraja muhimu la kukuza biashara na mahusiano ukanda wa katika Afrika Mashariki, hasa miongoni mwa nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Burundi.
Benki hiyo kwa sasa inatoa huduma katika nchi ya Burundi na inaelezwa kuwa katika robo ya tatu yam itazindua huduma zake kupitia kampuni tanzu huko Lubumbashi, jiji la pili kwa ukubwa baada ya Kinshasa, nchini DRC.
Kuanzishwa kwa kampuni tanzu hiyo kunaendana vyema na hatua za hivi karibuni ambapo nchi ya DRC imekubaliwa ombi lake la kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kufanya jumla ya nchi saba wanachama katika ukanda huu.
Waziri Mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni, alisema amefurahishwa kusikia kwamba Benki ya CRDB inafungua kampuni yake tanzu nchini DRC itakayokuwa na makao yake makuu mjini Lubumbashi na kutaka huduma hizo kusogezwa karibu na mpaka wa Burundi na DRC pia.
"Ninaiomba benki kufungua matawi karibu na mipaka ya Burundi na DRC, katika miji ya Uvira na Bukavu ili kuimarisha biashara," Bunyoni alisema hayo wakati alipotembelewa na ujumbe wa Benki ya CRDB ofisini kwake mwishoni mwa juma lililopita kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inayoipa benki hiyo.
Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Ally Lay na Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ambao waliambata Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt Jilly Mareko.
Madhumuni yalikuwa kwa wajumbe wa Kikundi cha Benki ya CRDB kufahamu msaada ambao benki hiyo inapata kutoka kwa serikali ya Burundi tangu wakati mkopeshaji alipofungua kampuni yake tanzu nchini Burundi mwaka 2012.
Katika mazungumzo yaliyofanyika, Benki hiyo ilimhakikishia Bunyoni kuendelea kushirikiana na serikali zote mbili za Burundi na Tanzania kufadhili miradi ya pamoja inayofanywa na nchi hizo mbili hususan mradi wa reli ya kisasa (SGR) na miradi mingineyo.
Waziri Mkuu huyo aliishukuru Benki ya CRDB kwa kusaidia kukuza uchumi wa Burundi kupitia uwezeshaji mkubwa inaoufanya nchini humo kwa kutoa mikopo inayogusa makundi mbalimbali ya wateja kuanzia kupitia watu binafsi, makampuni na hata serikali.
"Niwahakikishie kuwa serikali yetu inaunga mkono jitihada mnazozifanya katika kuinua uchumi wa Taifa letu la Burundi, na tupo tayari kushirikiana nanyi katika utekelezaji miradi mikubwa kwani baadhi yao inahusisha hata nchi zetu mbili za Tanzania na DRC," Bunyoni alisema.
Aliukumbusha ujumbe wa benki hiyo kuwa ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanzisha huduma za kibenki kupitia simu za mkononi nchini humo “SimBanking”, nakubainisha kuwa huduma hiyo imeleta mapinduzi makubwa nchini humo na kuwa kichocheo kikubwa katika kuongeza ujumuishi wa kifedha.
Pia aliishukuru Benki ya CRDB kwa uwezo wake wa kukusanya fedha kwenye masoko ya kimataifa bila masharti magumu kama ambavyo imekuwa ikifanywa na baadhi ya wakopeshaji kutoka nje ya Afrika.
"Pia ni muhimu kutambua kwamba benki hii kupitia programu yake ya mageuzi ya kidijitali imekuwa ikisaidia kurahisha miamala ya kibiashara ya kati ya Burundi na Tanzania kwa kuweka mifumo na miundo mbinu inayowezesha miamala ya kifedha kufanyika kwa urahisi ikiwamo malipo ya bandari na kodi mbalimbali zinazotozwa na serikali,” alioongezea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Laay, alimweleza Waziri Mkuu huyo kuwa benki hiyo imewekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali ili kuwawezesha wateja kuokoa muda na hata kupanua huduma za benki katika maeneo ambayo hayajafikiwa.
"Hii itasaidia Burundi katika utekelezaji wa ajenda yake ya kuongeza ujumuishi wa kifedha," Dkt Laay alisema na kuongeza:
"Ni katika muktadha huo benki sasa inasambaza huduma za CRDB Wakala wajulikanao kama ‘Turihose’ nchini humo, pamoja na kuhamasisha matumizi ya huduma za SimBanking, na huduma ya kibenki kupitia mtandao ‘Internet banking’ kwa wateja wake.”
Sambamba na miaka 10 ya Programu ya Maendeleo ya Taifa la Burundi, Mwenyekiti huyo alisema, benki hiyo inatarajia kuelekeza nguvu zake katika maendeleo ya sekta za kiuchumi kama vile kilimo, viwanda, miundombinu na makazi, na utalii ambazo ni muhimu katika kukuza ajira kwa vijana na kutengeza fedha za kigeni nchini humo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB alimweleza Waziri Mkuu Bunyoni kuwa kwa sasa benki hiyo inashika nafasi ya tatu kwa utoaji wa mikopo nchini Burundi baada ya miaka 10 ya kufanya kazi na asilimia 20 ya mikopo yake imetolewa katika sekta ya ili kusaidia Warundi wengi.
"Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, benki imeendelea kusaidia uchumi wa Burundi kwa kutoa bidhaa na huduma bunifu kwa makampuni, watu binafsi na taasisi wateja kupitia bidhaa za kuweka kuweka amana na mikopo," Nsekela alisema.
Hivi Karibuni ujumbe wajumbe wa viongozi wa Chemba za Biashara za nchi za Burundi, Misri, Zambia, Botswana, Rwanda, Ethiopia na Uganda ukiongozwa na Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR walitembelea makao makuu ya Benki ya CRDB na kupongeza mkakati wa benki hiyo wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Benki hiyo - ambayo imekuwa nchini Burundi tangu 2011 ina jumla ya matawi manne, matatu Bujumbura na moja katika mji wa Ngozi, mwaka huu Benki ya CRDB inatarajia kufungua tawi la tano katika Wilaya ya Gitega.
Akielezea matokeo ya kifedha ya kampuni tanzu ya Burundi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fred Siwale amesema mwaka jana walipata faida ya Shilingi bilioni 12.8 ikiwa niongezeko la asilimia 14 kulinganisha na faida ya Shilingi bilioni 11.1 iliyopatikana mwaka 2020.
Benki hiyo pia ilipata matokeo mazuri katika viashiria vingine vya utendaji; Jumla ya Risilimali imeongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 551.1 kutoka Shilingi bilioni 350 iliyorekodiwa mwaka 2020, wakati amana za wateja ziliongeka kwa asilimia 66 kufikia Shilingi bilioni 329.4 kulinganisha na Shilingi bilioni 198.6 iliyorekodiwa mwaka 2020.
Mikopo iliongezeka kwa asilimia 62 kutoka Shilingi bilioni 225 mwaka 2020 hadi Shilingi bilioni 598. Siwale alisema Benki hiyo imekuwa mlipakodi mkubwa kwa serikali ya Burundi pamoja na kutengeneza ajira kwa Warundi.
0 comments:
Post a Comment