Nchi za Tanzania Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimeanza mchakato wa kumtafuta mtaalamu atakayesimamia ujenzi wa reli ya kisasa kwa vipande vya Uvinza Msongati na Gitega.
Hii inakuja siku chache tangu nchi hizi zisaini makubaliano ya awali kuhusu kuanza mchakato wa kutafuta fedha kwa wahisani zitakazofanikisha ujenzi huo.
Haya yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati Kapteini Dioudone Dukundane wakati wa mahojiano maalum na wanahabari.
0 comments:
Post a Comment