Monday, 21 December 2020

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya

...


 KUPATIKANA NA BHANGI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SAAMOJA KANANDI [30] Mkazi wa Ndola – Mbalizi akiwa na bhangi gramu 380.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 20.12.2020 majira ya saa 19:30 usiku huko Mtaa wa Mshikamano, Kata ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni mchoma mahindi alificha kete za Bhangi kwenye kifungashio cha Mkaa na kuuza kwa wateja wake angali anauza mahindi. Upelelezi unaendelea.

KUKAMATWA MTUHUMIWA WA KOSA LA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUIBA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia RASHID KINDOLE [21] Mkazi wa Mkunywa – Madibira Wilaya ya Mbarali kwa tuhuma za kupatikana na mali za wizi baada ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 20.12.2020 majira ya saa 14:30 mchana huko Kijiji cha Mkunywa, Kata ya Madibira, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya katika misako inayoendeshwa na Jeshi la Polisi maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

Baada ya kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na mali za wizi ambazo ni:-

    Music Power Mixer 01,
    Camera aina ya Canon 01,
    TV aina ya Arborder 01,
    TV aina ya Sundar 01,
    TV aina ya Ceanic 01 na
    Betri 02 za Solar N12 aina ya Sundar.

Mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kuhusika na matukio mawili ya kuvunja nyumba usiku na kuiba katika Kijiji cha Mkunywa – Madibira Wilaya ya Mbarali. Upelelezi unaendelea.

Imetolewa na:

[ULRICH O. MATEI -SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger