Monday, 21 December 2020

Picha : TCRA YAENDESHA MAFUNZO YA KANUNI ZA UTANGAZAJI KWA VITUO VYA UTANGAZAJI KANDA YA ZIWA

...
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji Kanda ya Ziwa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imeendesha warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji vilivyopo Kanda ya Ziwa zikiwemo Runinga (Televisheni), Redio na Mitandao ya Kijamii ‘Online Tv na Blogs’ ili kuongeza uelewa kwa watangazaji na wasimamizi wa vituo vya utangazaji. 

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Desemba 21,2020 katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Tanzania jijini Mwanza ambapo walioshiriki mafunzo hayo ni Wahariri, Wakuu wa vipindi (Programme Managers), Watozi (Programme Producers) na Wanasheria kutoka vyombo vya utangazaji. 

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaongezea uelewa Watangazaji na Wasimamizi wa Vituo vya Utangazaji kuhusu Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazaji katika Redio na Televisheni) za mwaka 2018,Kanuni za sheria sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Habari za Mtandaoni);2018 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2020 na Kanuni za Kielektroniki na Posta (Leseni).

Mhandisi Mihayo amevitaka vyombo vya habari kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji ili kuepuka kujiingiza katika matatizo na kuendelea kushirikiana na TCRA.

"Ninapata tabu sana ninapoona chombo cha habari kinafanya makosa,naombeni mzingatie sheria na kanuni zilizowekwa, msijiingize kwenye matatizo", alisisitiza Mhandisi Mihayo. 

Mhandisi Mihayo pia amewasihi Viongozi wa Makundi ya Mtandao wa Kijamii wa 'Whatsapp  Group' kuhakikisha wanasimamia magroup ipasavyo  ili kuepuka maudhui yasiyofaa.

"Ukianzisha Group la Whatsapp wewe ndiyo kila kiranja wa group, hakikisha unachunga wanachama wako. Wewe Admin ndiyo unawajibika kwenye magroup",amesema Mihayo.

 Katika hatua nyingine Mhandisi Mihayo ukikosea kuchapisha habari mtandaoni unatakiwa kuondoa habari hiyo ndani ya masaa mawili.

Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka amesema kila kituo cha utangazaji kinatakiwa kuzingatia masharti ya leseni zao.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kisaka amesema TCRA haihusiki na utoaji Leseni kwa Mitandao ya Instagram, Whatsapp,Twitter na Facebook bali kwenye Blogs na Youtube kwa sababu zinatoa huduma za kihabari.

"Sisi TCRA hatutoi leseni kwenye mitandao ya Facebook, Twitter wala Instagram kwa sababu mitandao hii iliundwa kwa ajili ya kupeana taarifa mitandao hii. Licha ya kwamba hatutoi leseni lakini TCRA inasisitiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ikiwemo kutotukana. Hizi ambazo hazipewi leseni ni lazima zizingatie sheriaUkifanya hivyo utashughulikiwa kama mhalifu mwingine",amesema Mhandisi Kisaka. 

"Tunatoa leseni kwa Blogs na Youtube kwa sababu ina sifa za habari. Ukifanya kosa kwenye blogs na Youtube zilizosajiliwa na TCRA utashughulikiwa na TCRA, tunakushughulikia kama mtoa huduma ya maudhui mtandaoni , ukifanya makosa kwenye social networks ambazo hazijasajiliwa TCRA utashughulikiwa na Polisi",ameongeza Mhandisi Kisaka.

Aidha Mhandisi Kisaka amewataka watoa huduma za habari mtandaoni kuwa makini wanapotoa habari mtandaoni kwa kuhakikisha wanapima kile wanachotaka kukichapisha kama kina manufaa kwa jamii.

 "Jipime mwenyewe unapotoa maudhui mtandaoni, lengo la maudhui unayotoa ni nini kwa jamii?. Unapotoa habari mtandaoni unatakiwa kuwa makini sana. Lazima uwe Objective hata kama unafanya habari mtandaoni",ameongeza.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifungua mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji vilivyopo Kanda ya Ziwa zikiwemo Runinga (Televisheni), Redio na Mitandao ya Kijamii ‘Online Tv na Blogs’ leo Jumatatu Desemba 21,2020 katika ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Tanzania jijini Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji Kanda ya Ziwa. Kulia ni Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji Kanda ya Ziwa.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akitoa mada kuhusu Kanuni za Utoaji Leseni, Kanuni za Maudhui ya Redio na Televisheni, Kanuni za Maudhui ya Habari Mtandaoni kwenye warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji vilivyopo Kanda ya Ziwa zikiwemo Runinga (Televisheni), Redio na Mitandao ya Kijamii ‘Online Tv na Blogs’ ili kuongeza uelewa kwa watangazaji na wasimamizi wa vituo vya utangazaji. Kushoto ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akisisitiza Vituo vya Utangazaji kuzingatia Kanuni za Utangazaji.
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka  akizungumza kwenye warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji vilivyopo Kanda ya Ziwa zikiwemo Runinga (Televisheni), Redio na Mitandao ya Kijamii ‘Online Tv na Blogs’ ili kuongeza uelewa kwa watangazaji na wasimamizi wa vituo vya utangazaji.

Wahariri,wakuu wa vipindi (Programme Managers), Watozi (Programme Producers) na Wanasheria kutoka vyombo vya utangazaji Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye warsha ya mafunzo ya Kanuni za Utangazaji kwa vituo vya utangazaji iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger