Na Dotto Mwaibale
BAADA ya kimya cha muda mrefu, Mwimbaji wa Muziki wa Injili Nchini Tanzania, Stella Joel ameachia wimbo wa kuhamasisha maendeleo unaoitwa 'Tanzania ya Maendeleo'.
Mara ya mwisho Stella aliachia wimbo wa Hakuna Mwanamke mbaya alioshirikiana na malkia wa muziki wa Injili, Rose Muhando.
Stella ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) amesema, imefika hatua kwa wasanii kuhamasisha nyimbo zinazochochea maendeleo na kuisaidia jamii kutatua changamoto zake.
“Baada ya Tanzania kufikia uchumi wa kati nikaona ni vyema niweke hilo kwenye muziki, nyimbo za aina hii zinachangia sana kupiga hatua za kimaendeleo zaidi,” amesema Stella.
Stella amewashauri wanamuziki nchini kubadilisha mtizamo wao, kutojikita kwenye jumbe za mapenzi peke yake badala yake waangalie changamoto nyingi za kijamii kama masuala ya lishe, ukatili wa kijinsia na mengine.
0 comments:
Post a Comment