Saturday, 19 December 2020

MKURUGENZI UTPC : ULINZI NA USALAMA KWA WAANDISHI WA HABARI BADO NI TATIZO

...
Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa Clabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Abubakar Karsan akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya ulinzi na usalama yaliyofanyika Dodoma

Na Dinna Maningo, Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Abubakar Karsan amesema kuwa ulinzi na usalama wa waandishi wa habari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi bado ni tatizo kwani yamekuwa yakishuhudiwa matukio mbalimbali yanayowakumba waandishi wa habari.

Karsan aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya ulinzi na usalama wa Mwandishi wa habari yaliyotolewa kwa baadhi ya waandishi kutoka vyama 28 vya waandishi wa habari Tanzania Bara na Visiwani,yaliyofanyika katika ukumbi wa Royal Village Hotel mkoani Dodoma.

Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya umuhimu na mbinu mbalimbali za kujilinda wapokuwa kazini ili kuwa salama.

"Ni mara chache mimi kushiriki moja kwa moja kwenye mafunzo ya waandishi hii ni mara yangu ya tatu,zamani wakati tunafanya kazi vitisho kwa waandishi vilikuwa vidogo lakini kadri miaka inayokwenda vitisho na vifo kwa waandishi vinaongezeka.

" Baadhi ya waandishi wamekumbana na matatizo ya ana kwa ana mtu anakushambulia hadharani,wengine wanapewa vitisho,kutukanwa,kupigwa,kunyang'anywa na kuharibiwa vitendea kazi licha yakwamba ni haki ya mwandishi kikatiba kuandika na kutoa taarifa"alisema Karsan.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa waandishi hao watapata elimu ili kujua namna ya kujikinga anapokuwa anatekeleza majukumu yake,aliwataka waandishi kuwa makini wanapokuwa wanaandika habari kupitia mitando ya kijamii.

"Kuna waandishi wanaandika habari kwenye intaneti au kwenye kopyuta akimaliza hakumbuki kufuta au kufunga mtandao anaotumi kuandika habari matokeo yake watu wanasoma aliyoyaandika na hivyo kuwa hatarini tujitahidi kutunza siri za kazi zetu.

Aliongeza"Tunaokwenda baa tuwe makini msinywe pombe na glasi za baa tembea na glasi yako,usizoee kwenda baa au kwenye hoteli hiyo hiyo kila wakati ni hatari kwa usalama wako,na tuwe makini na wapenzi wetu wengine wanatumwa kutuchunguza,tuache kuchongeana na tusisemane wenyewe kwa wenyewe tunaumizana" alisema Karsan.

Ofisa Pdogramu-Mafunzo,utafiti na Machapisho wa UTPC  Victor Maleko aliwataka waandishi wa habari wanapopata matatizo kwenye eneo wanalofanyia kazi kutoa taarifa kwa waratibu wao wa vyama vya waandishi kwakuwa taarifa hizo zinawasaidia kufahamu yanayoendelea na kuyashughulikia kwa wakati.

Mkufunzi wa mafunzo hayo ya ulinzi na usalama Charles Kayoka ambaye ni mhadhiri kutoka chuo kikuu Dar es Salaam Idara ya sanaa akifundisha masomo ya uhakiki wa film na utunzi alisema kuwa licha ya waandishi kuwa na vitambulisho vya kazi lakini hawapewi ushirikiano wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kazi

"Tunalipa sh 50,000 kupata press Card lakini bado ukienda kwenye ofisi  unaombwa barua ya mwajiri wako mara uombwe barua ya Mkurugenzi" alisema Kayoka.

Kayoka amewataka waandishi kuwa makini kwenye kazi zao kwani Mwandishi kufahamu jambo lolote ni hatari kwake kwakuwa si wote watakaofurahishwa na jambo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa Clabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Abubakar Karsan akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya ulinzi na usalama yaliyofanyika Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa Clabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Abubakar Karsan akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya ulinzi na usalama yaliyofanyika Dodoma
Mwezeshaji Charles Kayoka akitoa mafunzo ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari
Mwezeshaji Charles Kayoka akitoa mafunzo ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger